Najua kabisa umeshaweka malengo na mipango ambayo unatakiwa kuifanyia kazi. Na pia umeshajua uanzie wapi ili uweze kufikia kile unachokitaka. Lakini siku zinakwenda na hakuna cha tofauti unachofanya. Tatizo nini?
Unapanga kuanzia kesho nitaanza kufanya kitu fulani kwenye maisha yangu au kwenye kazi yangu au kwenye biashara yangu. Lakini kesho inapofika unapata visababu ambavyo vinakufanya uendelee kusogeza kesho. Kama hutastuka mapema utakuja kujikuta muda umekwenda na hujafanya chochote ambacho ulikuwa umepanga kufanya.
SOMA; Kama Hujali sana Juu Ya Kitu Hiki Katika Maisha Yako, Sahau Kuhusu Mafanikio.
Kikubwa kinachokufanya moaka sasa unaahirisha mambo ni kukosa mbinu muhimu ya kupambana na tabia hiyo.
Leo hapa utajifunza mbinu tatu muhimu.
Kwanza; anza kufanya jambo, kikwazo kikubwa kinaanzia pale unapoendelea kuahirisha. Mara nyingi unajiona kwamba ni afadhali kutofanya jambo kwa sasa ila ukweli ni kwamba unapoteza. Anza kufanya na yote unayohofia yatapotea yenyewe.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Pesa Zako Na Kuwa Tajiri.
Pili ondokana na kelele au mazingira yatakayokusumbua. Hakuna changamoto kubwa kwenye ulimwengu wa sasa kama usumbufu. Sasa hivi tuna simu ambazo zinauwezo wa kukuunganisha na dunia masaa 24 kwa siku na siku saba kwa wiki. Kuna mitandao ya kijamii ambayo inavutia sana kutembelea. Hizi zote ni kelele kwako na unahitaji kuziepuka la sivyo utaendelea kuahirisha mambo yako muhimu.
Tatu; tumia kauli shawishi kukusukuma kufanya zaidi. Pale unapopanga kufanya jambo kuna wazo linakujia kichwani kwamba sio lazima sana kufanya leo, kwani bado muda upo na unawez akufanya hata na kesho. Kauli hii inapokujia jua kwamba ndio unatakiwa uendelee kufanya jambo hilo. Yaani pale unapjisikia kuahirisha jambo ndio unatakiwa uendelee kulifanya haraka zaidi.
SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.
TAMKO LA LEO;
Najua kwamba tabia ya kuahirisha mambo imekuwa inanirudisha nyuma na nisipokuwa makini itakuwa kikwazo kikubwa kwangu kufikia malengo niliyojiwekea. Kuanzia leo nitaanza kufanya jambo mara moja pale ninapopanga kufanya na nitaondokana na usumbufu wowote ambao utaweza kunifanya nifikirie kufanya nilichopanga. Pia pale nitakapopata wazo kwamba naweza kufanya kesho, hapo ndio nitakazana zaidi ili niweze kufanya leo.
Tukutane kwenye ukurasa wa 70 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment