Kuanzia mwaka huu 2015 umeanza tayari tumemaliza siku 60 na leo ni siku ya 61.
Kama kuna mabadiliko yoyote uliyokuwa umepanga kufanya kwenye mwaka huu unahitaji mpaka sasa uwe umeshaanza kuona matunda mazuri.
Kama mpaka sasa hakuna matunda yoyote mazuri unayoona kwenye mabadiliko yako, ni labda hufanyi kwa kiwango cha kutosha au kuna makosa makubwa unayofanya na yanayokuzuia kufurahia matunda ya mabadiliko yako.
SOMA; Jambo Moja La Kushangaza Kuhusu Maisha.
Leo ni siku muhimu kwako kukaa na kufanya tathmini kubwa ya siku 60 za mwaka huu umezitumiaje mpaka sasa.
Kama umekuwa ukifanya mabadiliko kwenye kazi zako je umeanza kuna matunda mazuri, je watu wameanza kuona ubora wa kazi zako? Je viwango vya kazi unazofanya kinakuwa bora?
Kama mwaka huu ulipanga kuboresha biashara yako, je umeshaanza kuona mabadiliko kwenye biashara yako? Umeshaanza kuona ongezeko la wateja? Umeshaanz akuona ongezeko la faida?
Kama hutachukua muda wa kujipima unaweza kuona mambo yanakwenda vizuri ila utakapofika mwisho wa mwaka ukashindwa kuonesha ni kipi umekamilisha mwaka huu.
Fanya zoezi hili muhimu leo na lirudie kila baada ya siku 60. Kumbuka kurudia baada ya muda huo kwa sababu huenda sitakukumbusha tena.
SOMA; Hiki Ni Kitu Unachotakiwa Kufanya Kila Siku...
TAMKO LA LEO;
Leo nafanya tathmini ili nijue kama kweli mabadiliko niliyotaka kufanya mwaka huu yanafanyika kweli na kama nimeanza kuona matunda. Najua nisipoweka utaratibu huu naweza kuona mambo yako vizuri ila mwisho wa mwaka nikajikuta hakuna kikubwa nilichokamilisha.
Tukutane kwenye ukurasa wa 62 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment