Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, March 11, 2015

Hii Ndio Hatari Kubwa Ya Zama Hizi Tunazoishi..

Kama ulisoma historia wakati upo shuleni utakuwa unakumbuka kwamba binadamu amepitia vipindi vingi sana mpaka kufikia hapa tulipo sasa.

Kwanza kabisa binadamu alianza kwa kula mizizi na majani, baadae akawa anawinda, baadae akaanza kulima ikaendelea hivyo mpaka sasa maisha yanaonekana kuwa bora zaidi.

Binadamu tumepitia zama nyingi sana. Tumepita zama za mawe ambapo mawe ndio yalikuwa kifaa muhimu cha kufanyia kazi, zikaja zama za chuma, baadae mapinduzi ya viwanda na sasa tupo kwenye zama za taarifa.

SOMA; Kauli KUMI Za Marcus Aurelius Zitakazokufanya Uyaone Maisha Kwa Utofauti.

Katika kila zama kulikuwepo na hatari zake. Zamani sana katika zama za mawe binadamu alikuwa na hatari kubwa yakuliwa na wanyama wakali kama simba. Baadae zikaja hatari nyingine za magonjwa hatari, zikaja hatari nyingine za kuyumba kwa uchumi na kadhalika. Hapo ulipo huna hofu yoyote ya kuliwa na simba, lakini kuna simba wengine wakali ambao wanakunyemelea kila siku.

Hatari ya zama hizi ni nini basi?

Zama hizi zina hatari kubwa kuliko zama zote zilizopita. Na hatari hii ni mbaya sana kwa sababu watu hawaijui kama ni hatari. Hatari hii inatokana na faida ya zama hizi pia ambayo ni TAARIFA.

Taarifa imekuwa hatari sana kwenye zama hizi za taarifa. Sasa hivi unaweza kupata taarifa masaa 24 kwa siku siku saba kwa wiki na mwaka mzima. Tatizo kubwa ni kwamba taarifa hizi ziko hasi sana na ziakukatisha tamaa, kukujaza hofu na kukurudisha nyuma.

SOMA; Unataka Kuiona Dunia? Vua Miwani…

Zama hizi tumekuwa na vifaa ambavyo vinatuwezesha kupata taarifa popote pale tulipo, hata kitandani. Vifaa hivi ni simu zenye uwezo mkubwa au kwa jina lingine smartphones. Hizi zimetuunganisha na mitandao mingi sana ambayo wka silimia 90 haina manufa amakubwa kwetu. Lakini tumeng’ang’ania vitu hivi na vinaendelea kuturusisha nyuma.

Unahitaji kujichunguza sana ni aina gani ya tarifa unazopokea kila siku. Ni aina gani ya mitandao unayotembelea kila siku. Maana kila kinachoingia na kukaa kwenye akili yako wka muda mrefu ndio kinatokea kwenye maisha yako.

Jilinde na hatari hii kubwa. Jua ni taarifa gani utahitaji kuchukua na zipi unahitaji kuziepuka.

Nakutakia siku njema.

SOMA; SIRI YA 42 YA MAFANIKIO; Mtazamo Wako Utapima Mafanikio Yako.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment