Jambo moja la kushangaza kwetu binadamu ni kwamba kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na kuna vitu ambavyo hatuwezi kufanya.
Vitu ambavyo tunaweza kufanya ni vile vitu ambavyo tumekuwa tunafanya kila siku, au tunaona watu wengine wakiwa wanavifanya. Hii inatupa imani kwmaba vinawezekana kufanyika na tunaweza kuvifanya bila ya tatizo.
SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.
Kwa upande wa pili kuna vitu ambavyo hatuwezi kufanya. Vitu hivi vimegawanyika katika makundi mawili, ila hatuyajui. Kundi la kwanza ni vitu ambavyo ni kweli kabisa hatuwezi kuvifanya kutokana na kukosa baadhi ya vitu tunavyohitaji. Na kundi la pili ni vitu ambavyo hatuwezi kuvifanya kwa sababu hatujawahi kufanya au hatujawahi kumuona mtu akivifanya.
Asilimia 99 ya vitu tunavyoona hatuwezi kufanya vipo katika kundi la pili, yaani tunaona hatuwezi kufanya, sio kwa sababu haiwezekani kabisa, ila kwa sababu hatujawahi kufanya au hatujamuona mtu mwingine anafanya.
SOMA; Njia KUMI Za Kuboresha Maisha Yako Ya Kibiashara.
Badili sasa mtizamo wako kuhusu vitu ambavyo unafikiri huwezi kufanya. Unapopata wazo lolote, badala ya kuliua kwa kusema hii haiwezekani au siwezi kufanya, sema nawezaje kufanya kitu hiki? Kwa kujiuliza swali hili unaipa akili yako nafasi ya kuchambua na kama unajiamini utapata majibu mengi sana ya jinsi unavyoweza kufanya.
Kitu unachoweza kufanya bila ya kujali hali yako ni kile ambacho unaamini unaweza kufanya.
Kitu usichoweza kufanya ni kile ambacho unaamini huwezi kufanya. Ni hivyo tu.
SOMA; Vitu VITATU Vinavyoathiri Kipato Chako Na Jinsi Ya Kukiongeza.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwmaba hatua ya kwanz aya kuwez akufanya kitu ni kuamini kwamba kinawezekana kufanyika, naweza kukifanya. Kuanzia sasa kila nitakapopata wazo la kuboresha kazi au biashara zangu sitasema haiwezekani ila nitajiuliza itawezekanaje? Swali hili litafungua akili yangu na kunipa majibu mengi zaidi.
Tukutane kwenye ukurasa wa 79 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment