Wenye busara walipata kusema maneno haya mazuri sana;
Kama zana pekee uliyonayo ni nyundo, basi kila kinachokuja mbele yako kitaonekana kama msumari.
Umeielewa vizuri kauli hiyo? Kama hujaielewa tafuta mtoto mdogo halafu mpe nyundo akae nayo tu na uone atakuwa anafanya nini. Atagonga kila kitu.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)
Sawa najua wewe huna nyundo tu na pia najua tukikupa nyundo hutagonga kila kitu. Ila umekuwa unafanya kosa hili karibu kila siku kwenye maisha yako.
Fikiria ni matatizo mangapi ambayo umeshakutana nayo kwenye maisha yako, je umekuwa unajaribu kuyatatuaje? Ni hatua zipi ambazo umekuwa unachukua pale unapokutana na changamoto?
Kama utakuw amuwazo na nafsi yako utaona kwamba umekuwa unatatua matatizo yako yote kwa aina moja ya kufikiria. Umekuwa ukipambana na changamoto zako zote kwa mbinu moja.
Bado unashangaa kwa nini matatizo hayaishi, au kwa nini changamoto zinakushinda? Ni kwa sababu unatumia nyundo tu, una aina moja ya mawazo ya kutatua matatizo yako. Una mbinu moja ya kupambana na changamoto zako na hivyo umekuwa ukishindwa na kama utaendelea kuitumia utaendele akushindwa.
SOMA; Hatua TANO Za Kuongeza Uzalishaji Wako Ili Kufikia Mafanikio.
Anza kupata mawazo tofauti tofauti kwenye tatizo unalokutana nalo. Badala ya kufikiria wewe ndio upo kwenye tatizo hebu fikiria kama usingekuwa kwenye tatizo hilo, ungemshauri nini aliyepo kwenye tatizo hilo? Kama ingekuwa wewe sio muathirika wa tatizo hilo je ungelichukuliaje? Aina hizi tofauti za kufikiria zitakupatia picha kubwa itakayokusaidia kuchukua hatua nzuri.
Unapokutana na changamoto kabla hujairukia na kuanza kuitatua kaa chini kwana na ufikirie mbinu gani inafaa kwa changamoto hiyo. Jua nini chanzo cha changamoto hiyo. Jua ni kwa kiasi gani inakuathiri. Na jua wengine waliokutana na changamoto hiyo walitumia njia gani wakashindwa na walitumia njia gani wakafanikiwa kupambana nayo.
Njia muhimu kabisa ya kupata mawazo tofauti, ya kupata mbinu tofauti ni kujifunza, kusoma. Jifunze kutokana na makosa yako mwenyewe, jifunze kutoka kwa wengine pia. Na muhimu zaidi soma kila siku.
SOMA; Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.
TAMKO LA LEO;
Najua kuna zana nyingi nazoweza kutumia kutatua matatizo yangu, kupambana na changamoto zangu. Sitatumia tena zana moja ambayo nimezoea kuitumia kila siku, kwa sababu kila tatizo, kila changamoto ina utofauti wake na inahitaji mbinu tofauti. Nitajifunza na kujisomea kila siku ili niweze kuongeza zana zangu za kuniwezesha kufanikiwa kwenye maisha.
Tukutane kwenye ukurasa wa 80 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment