Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, March 14, 2015

UKURASA WA 73; Unaweza Kwenda Umbali Mrefu Kiasi Gani?

Unaweza kwenda umbali mrefu kiasi gani? Kwenye kazi yako, biashara yako na hata maisha yako?

Unaweza kufanya kazi bora kiasi gani? Unaweza kufanya kazi nyingi kiasi gani? Unaweza kuonesha upendo wako kwa kiasi gani?

Huwezi kujua umbali unaoweza kwenda kwenye jambo lolote unalofanya kama hujawahi kwenda mbali zaidi. Yaani kama umeshazoea kwenda hatua kumi tu kila siku, utaanzakufikiria kwamba uwezo wako ni hatua kumi. Ila hakuna aliyekuambia huo ndio uwezo wako wote, kwa sababu tu umezoea umeshaona ndio hivyo.

SOMA; UKURASA WA 30; Nenda Hatua Ya Ziada…

Ili kujua ni umbali gani hasa unaoweza kwenda, unahitaji kwenda mbali zaidi. Ili kujua ni ubora kiasi gani wa kazi unaweza kufanya unahitaji kufanya kazi bora zaidi na zaidi. Ili kujua ni kazi kiasi gani unaweza kuzalisha, unahitaji kuzalisha zaidi na zaidi.

Chochote unachotaka kuboresha nenda zaidi, na jisukume mpaka hatua ya mwisho. Mara moja moja kwenye kazi, biashara au maisha yako jaribu kufanya kitu ambacho hujawahi kufanya. Ndio kitakupa hofu, kitakuweka kwenye nafasi ya kushindwa, ila fanya na utajifunza mambo mengi sana ambayo hujawahi kupata nafasi ya kujifunza.

SOMA; Kuwa Kawaida Ni Kupoteza Muda Wako Na Siri Moja Ya Mafanikio Mwaka 2015

TAMKO LA LEO;

Nitahakikisha najua ni umbali gani naweza kwenda kwenye jambo lolote ninalofanya. Na ili kujua umbali huu nahitaji kwenda zaidi ya nilivyozoea. Nahitaji kufanya zaidi ya nilivyozoea kufanya. Nahitaji kufanya kitu ambacho sijawahi kufanya, ili kujifunza zaidi juu ya uwezo wangu na hata ukomo wangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 74 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment