Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, March 5, 2015

UKURASA WA 64; Nusa Mabadiliko.

Kitu kimoja ambacho naweza kukuhakikishia ni kwamba mabadiliko yanatokea kila siku. Sina haja ya kukushawishi sana hili maana wewe mwenyewe unaona, labda iwe umeamua kutokuona kwa makusudi.

Kama unahitaji nikukumbushe kidogo, fikiria makampuni kama ya posta, simu za mkononi, maktaba na mwengine mengi yanaelekea wapi kibiashara. Yanakufa kwa sababu kuna njia rahisi sana za kufanya haya mambo sasa hivi.

Vile vile makampuni kama ya magazeti, tv, redio na mengine yanafuatia kwenye kufa, maana sasa hivi watu wana njia rahisi sana ya kupata habari kuliko zamani.

SOMA; Mabadiliko Yanaanzia Hapa...

Hali hii haishii hapa tu, inakuja mpaka hapo ulipo, kwenye kazi unayofanya na hata biashara unayofanya. Kila siku kuna mabadiliko yanayotokea ambayo yanafanya maisha yawe rahisi zaidi na hivyo kuiweka kazi yako au biashara yako hatarini. Zamani wakati machaguo yalikuwa machache kuna kampuni ambazo zilikuwa na ufahari sana. Ila sasa hivi kampuni hizo zinakutana na changamoto kubwa inayohatarisha uwepo wao.

Ili kuhakikisha mabadiliko yanayoendelea hayakuachi wewe katika hali mbaya kuwa mtu wa kunusa mabadiliko.

Unawezaje kunusa mabadiliko?

Hatua ya kwanza kabisa ni kujua vizuri kile unachofanya, kama ni biashara ijue vizuri sana kwa kila eneo. Kama ni kazi ijue vizuri, Kuwa mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea kuhusu biashara yako au kazi yako. Na unapoanza kuona mambo yanakwenda tofauti na yanavyotegemewa jua kuna mabadiliko yanakuja.

SOMA; NENO LA LEO; Chagua Kitu Hiki Kizuri…

TAMKO LA LEO';

Haijalishi ni mafanikio kiasi gani nimefikia, sitolala bali nitaendelea kunusa mabadiliko. Nitahakikisha mabadiliko yoyote yanayotokea nayajua kabla na nitajiandaa nayo ili yasiniache katika hali mbaya. Kitu pekee ambacho ninajua hakibadiliki ni mabadiliko, yataendelea kuwepo kila siku.

N;B Niliahidi kutoa zawadi ya kitabu kuhusu mabadiliko, bado nakumbuka na bado kitabu hakijakamilika. Naweka juhudi zangu kuhakikisha kitabu hiki utaweza kukisoma leo, mwaka kesho, miaka kumi ijayo na hata miaka ishirini ijayo na bado ukapata mbinu za kukuwezesha kuenda vizuri na mabadiliko yanayotokea kila siku.

SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Mabadiliko Kwenye Maisha.

Tukutane kwenye ukurasa wa 65 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment