Katika moja ya changamoto kubwa sana ambayo watu wanaipata na inawazuia kufikia mafanikio ni kushindwa kutangaza kazi zao.
Na hii inakwenda sana kwa wale ambao wanafanya kazi binafsi.
Kwa mfano kama unapika mandazi matamu sana, ila anayejua kuhusu mandazi hayo ni wewe na familia yako tu, je nafikiri unabiashara hapo?
Hata kama una kitu kizuri kiasi gani, kama watu hawajui kipo hawawezi kukifikia.
Kuna ile dhana kwamba kizuri chajiuza na kibaya chajitangaza, nakutangazia kuanzia leo kwamba sio kweli, na usiamini tena usemi huu.
Dunia ya sasa ina kelele nyingi sana, ni vigumu sana watu kujua kama upo kama hutowatangazia na wakajua kinapatikana wapi.
Kwa kazi yoyote unayofanya hakikisha unaitangaza kwa wale watu ambao wanafaa kuwa wateja wako.
Tahafhari ni kwamba usijaribu kutangaza kwa kila mtu, maana wengine hawawezi kuwa wateja wako na wewe huna muda wa kupoteza kwa kila mtu.
TANGAZA KAZI YAKO, NENDA KIFUA MBELE UKIJIVUNIA KAZI YAKO. JINSI UTAKAVYOKUWA NA HAMASA NA KAZI YAKO, NDIVYO UNAVYOWEZA KUWASHAWISHI WENGI ZAIDI.
ILA KAMA UNAONA AIBU, UNASUBIRI WATU WAJUE WENYEWE UNAJICHIMBIA SHIMO LAKO MWENYEWE, MAANA HAWATAJUA.
0 comments:
Post a Comment