Katika jambo lolote unalofanya kwenye maisha, kuna watu watakuwa wanashindana na wewe, hata kama hawashindani wanajipanga kukushinda.
Kama unafanya biashara, wakati wewe unakazana usiku na mchana kukuza biashara yako, kuna watu wanakazana usiku na mchana kukuondoa kwenye biashara hiyo.
Kama unafanya kazi na ukawa na cheo kuna watu wanakazana usiku na mchana kukuondoa wewe kwenye cheo hiko. Hata kama huna cheo, nafasi yako ya kazi tu kuna vijana hawana ajira na wanakazana sana kuipata.
SOMA; UKURASA WA 54; Kufa MTUPU….
Sasa ufanyeje ili uweze kushinda ushindani huu mkali kiasi hiki? Je na wewe ushindane? Ukiingia kwenye mashindano umekwisha.
Kumbuka kwenye mbio za panya, hata anayeshinda anabaki kuwa panya. Hivyo wewe ukiingia kwenye mashindano utaishia kuwa kama hao unaoshindana nao hata kama utawashinda.
Badala ya kukazana kushindana, kazana kuwa bora. Tumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako, tumia vipaji ulivyo navyo, tumia ubunifu wako kuifanya kazi yako au biashara yako kuwa bora zaidi. Kuwa bora kiasi kwamba kila anayeguswa na kazi yako anatamani kuendele akufanya kazi au biashara na wewe.
Hii ndio njia pekee salama itakayokuvusha kwenye dunia hii yenye fujo nyingi.
SOMA; UKURASA WA 14; Kataa Kupokea Chochote Kizuri, Na Kubali Hiki…
TAMKO LA LEO;
Sitahangaika kushindana na wale wanaotaka kuniangusha. Nitakazana kuwa bora sana katika hiki ninachofanya. Nitahakikisha kila anayekutana na hiki ninachofanya ananufaika sana. Najua kwa njia hii hakuna ushindani utakaoweza kunifikia.
Tukutane kwenye ukurasa wa 64 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment