Moja ya magonjwa ambayo yamewahi kuisumbua sana dunia ni ugonjwa wa ukoma.
Huu ni ugonjwa ulioua watu wengi sana na kuacha wengine wakiwa kwenye hali mbaya sana.
Changamoto kubwa ya ugonjwa huu ni kwamba ulikuwa wa kuambukizwa. Yaani ukikaa na mtu mwenye ukoma na wewe unapata ugonjwa huu.
Kwa hiyo njia kubwa ya kujikinga na ugonjwa huu ilikuwa ni kujitenga na watu wenye ugonjwa huu.
Kwa bahati nzuri sana ugonjwa huu umetokomezwa kabisa duniani.
Ila kwa bahati mbaya sana kuna ukoma mpya umeingia duniani. Ukoma huu unaua watu wengi sana lakini wengi bado hawajaujua.
Ukoma huu ni mawazo hasi.
Mawazo hasi yamekuwa yanawarudisha watu wengi sana nyuma.
Yamekuwa yakizima ndoto nzuri za watu na hata kuharibu maisha yao kabisa.
Mawazo hasi yanasambaa kwa kasi kuliko hata ukoma, hasa kwenye ulimwengu huu ambao mawasiliano yamekuwa rahisi sana.
Jiepushe na ugonjwa huu kwa kukagua kila wazo unalopokea kabla ya kuliingiza kwenye akili yako na kuliufanyia kazi.
Epuka sana mawazo hasi, ni sumu kubwa kwa mafanikio yako.
0 comments:
Post a Comment