Swali; je unahitaji mipango mingapi ili kutangaza kushindwa?
Jibu; Inategemea na nini unachotaka. Kama unajaribu tu kufanya kitu unahitaji mpango mmoja tu na ukishashwindwa huo unaweza kutangaza kushindwa na ukaachana na malengo yako.
Ila kama unataka kushinda, unataka kupata mafanikio, kama unachotaka ni mafanikio tu na sio kingine, basi mipango unayohitaji haina namba na haina kikomo.
Ukishaweka malengo yako, weka mipango ya kufikia malengo hayo. Na kama mpango wa kwanz aukishindwa, weka mpango mwingine mara moja. Na kama mpango huu pia utashindwa weka mpango mwingine tena. Na kama mpango huu wa sasa utashindwa pia, weka mpango mwingine haraka sana.
Yaani kwa kifupi hakuna kikomo cha mipango mingapi unahitaki kuweka ndio ufanikiwe.
Unakumbuka Thomas Edison alijaribu mara ngapi mpaka akaweza kugundua taa ya umeme? Zaidi ya mara elfu kumi. Sasa hebu niambie wewe unayewaambia watu kwamba umejaribu ukashindwa ni mara ngapi ulizojaribu? Kama ni chini ya elfu kumi ni afadhali ukanyamaza kwa sababu bado hata hujavunja rekodi.
SOMA; UKURASA WA 47; Kuwa Na Subira, Hakuna Unachopoteza.
TAMKO LA LEO;
Kama mpango nilionao sasa utashindwa kunifikisha kwenye malengo yangu, nitaubadilisha na kuweka mpango mwingine. Kama mpango huo nao utashindwa, nitaweka mwingine. Na kama huu nilioweka utashindwa kunifikiasha kwenye mafanikio, sina shaka, nitaweka mpango mwingine tena. Nitajifunza kwenye kila mpango utakaoshindwa na kutengeneza mpango bora zaidi, lakini sitoacha lengo langu kubwa.
SOMA; UKURASA WA 07; Uvumilivu Ni Nguzo Muhimu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 66 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
SOMA; TABIA ZA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Kuweka Kipaumbele Kwenye Maisha Yako.
0 comments:
Post a Comment