Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, January 7, 2015

UKURASA WA 07; Uvumilivu Ni Nguzo Muhimu.

Japo umeshaamua kuchukua hatamu ya maisha yako na kukubali wewe pekee ndio unayeweza kubadili maisha yako…

Japo umeshaweka malengo na mipango ambayo unaifanyia kazi ili mwaka huu uwe wa tofauti kwako…

Japo umeshachagua kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kujua kwamba kazi ni muhimu sana…

Bado mafanikio hayatatokea mara moja tu. Yaani sio kwamba ukishafanya mambo hayo mafanikio yanakuja kwa uhakika. Ingekuwa rahisi hivyo kila mtu angekuwa amefanikiwa.

Pamoja na juhudi kubwa utakazofanya, njia hii ya kuelekea kwenye mafanikio ina changamoto na vikwazo vingi sana. Unaweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na bado usione mabadiliko. Unaweza kufanya kila kitu kwa uangalifu akaja mtu mwingine akavuruga kila kitu. Ndivyo maisha yalivyo.

Sasa ni kitu gani kitakachokuvusha kwenye kipindi kama hiki? UVUMILIVU, Hakuna kitakachokuwezesha kuvuka matatizo na changamoto zaidi ya uvumilivu. Unatakiwa kuwa mvumilivu ndio uweze kupata kile unachokitaka.

Hata wahenga walisema, MVUMILIVU…..

TAMKO LA LEO.

Najua ya kwamba safari yangu ya kuelekea kwenye mafanikio sio rahisi. Njiani nitakutana na matatizo na vikwazo mbalimbali vitakavyoweza kunikatisha tamaa. Lakini kwa kuwa nimedhamiria kubadili maisha yangu na kufikia mafanikio makubwa sitokubali matatizo au vikwazo vinirudishe nyuma. nitakuwa MVUMILIVU mpaka dakika ya mwisho. Ni heri nife nikiwa ninapambana kuliko kuishi maisha ambayo siyafurahii.

Tukutane kwenye ukurasa wa nane kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment