Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, January 4, 2015

UKURASA WA 04; Unacho Kila Unachohitaji Ili Kufanikiwa.

Kama ningekuwa na mtaji, basi ningeanzisha biashara kubwa sana na sasa hivi ungekuta nimeshafanikiwa.

Kama ningekuwa najuana na watu waliofanikiwa wangenipa connection na mimi ningeshatoka

Kama ningezaliwa kwenye familia yenye uwezo kama John ungekuta na mimi sasa hivi nina nyumba, gari na biashara kubwa.

Kama bosi wangu asingekuwa na roho mbaya, ningekuwa nafanya kazi vizuri na ningefanikiwa sana.

Kama serikali isingeongozwa na mafisadi, maisha yangekuwa bora sana.

Hizi ni baadhi ya kauli ambazo umekuwa unazitumia kila mwaka kujihalalishia kwa nini husongi mbele.

Swali, tokea umeanza kutumia kauli hizi ni kipi kimebadilika kwenye maisha yako? Je umepata connection? Je umepata mtaji? Je wazazi wako wamekuwa matajiri? Je bosi wako amebadilika? Na je serikali imekuletea maisha uliyotaka?

Kama jibu ni ndio, hongera, ila kama jibu ni hapana basi acha kupoteza muda kwa kutumia visingizio ambavyo huwezi kuvibadili.

Unacho kila unachohitaji ili kuweza kufikia mafanikio.

Elimu uliyonayo inakutosha kabisa, cha muhimu ni kujua ni jinsi gani unaweza kuitumia.

Mtaji wa biashara huna, ila cha msingi sana kwenye biashara sio mtaji, bali ile nia ya dhati ya kufanya biashara. Kama unayo kweli ndani ya muda mfupi tu utasimamisha biashara yako na kuifanyia kazi.

Soma; Biashara tano unazoweza kuanza kufanya bila ya mtaji.

Kila kitu unachohitaji unacho, hali ngumu unayopitia ndio iwe chachu kwako kufikia mafanikio makubwa. Kama bosi wako anakusumbua, hathamini kazi yako, unapata kipato kidogo hii ndio inabidi ikupe wewe hasira ya kwenda kujiajiri.

Soma; Sehemu tano unazoweza kupata mtaji wa kuanzia biashara.

Usilalamikie vitu ambavyo huwezi kuvibadili, tumia ulivyonavyo ili kuleta mabadiliko kwenye maisha yako kwa mwaka huu 2015.

TAMKO LA LEO

Ninacho kila ninachohitaji ili kuanza safari ya mafanikio. Nitatumia hali yangu ngumu kama kichocheo cha mimi kufanya jitihada zaidi ili mwaka huu 2015 uwe wa mabadiliko makubwa kwangu. Kuanzia leo sitotumia tena visingizio ambavyo siwezi kuvibadili.

Tukutane kwenye ukurasa wa tano kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment