Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, January 15, 2015

UKURASA WA 15; Afya Yako Ni Kitu Muhimu Sana.

Katika vitu muhimu sana kwenye maisha yako, cha kwanza ni afya yako.

Haijalishi una malengo na mipango mizuri kiasi gani kama afya yako ni mbovu hutaweza kufika popote.

Na kama kwenye kipigania malengo yako, umeisahau afya yako, unaweza kushindwa kufurahia kile unachokipata hasa unapokuwa na afya mbovu.

Kwa mfano utakuwa na furaha gani kama utapata fedha nyingi unazotaka halafu ukawa unaumwa ugonjwa ambao unajua hauwezi kutibika?

Chochote unachofanya hakikisha afya yako ni kipaumbele cha kwanza. Maana kwa wewe kuwa na afya ndio utaweza kufanya kile unachotaka kufanya.

Na kulinda au kutengeneza afya yako unahitaji kufanya mambo matatu tu;

1. Kula vizuri, usipunguze sana na usizidishe.

2. Fanya mazoezi

3. Jikinge na magonjwa yaambukizwayo.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba afya yangu ni kitu muhimu sana. Najua pia kama sitajali afya yangu, siwezi kufurahia malengo nitakayofikia. Kila siku nitakuwa makini kujenga na kulinda afya yangu kwa kula vizuri, kufanya mazoezi na kujikinga na magonjwa yanayoambukizwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa kumi na sita hapo kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment