Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, January 13, 2015

Maisha Sio Rahisi Lakini Ni Mazuri Kama Hivi...

Maisha ni magumu, angalau hakuna anayeweza kulipinga hili.
Maisha yatakuwa rahisi lini?
Hayatakuwa rahisi, unafikiri ukipata kazi maisha yatakuwa rahisi, ndio zinaibuka changamoto nyingine nyingi.
Unafikiri ukiongeza kipato maisha yatakuwa rahisi ila ukweli ni kwamba changamoto ndio zinazidi...
Sasa kama maisha sio rahisi na hayatakuwa rahisi uzuri wake uko wapi?
Uzuri wa maisha upo kwenye kufurahia hapo ulipo. Ndio hapo ulipo sasa kwa unachofanya ndio unaweza kufurahia maisha.
Ukifikiria jana ilishapita na haitarudi tena.
Ukifikiria kesho huna uhakika nayo.
Hivyo leo hii, hapo ulipo ndio pa kufurahia maisha na maisha yatakuwa mazuri kwako.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment