Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, January 3, 2015

Ukurasa Wa 03; KIFO…(Umuhimu Wake Na Jinsi Unavyoweza Kukitumia Kufikia Mafanikio)

Kuna siku utakufa, ndio unalijua hili ila kuna kitu kimoja hujajifunza kuhusiana na kifo chako.

Leo kwenye ukurasa wa 03 wa kurasa 365 za mwaka 2015 utaandika kitu kimoja kikubwa unachoweza kujifunza kutokana na kifo.

Baada ya muda utakufa na utakuwa umekufa kwa muda mrefu sana kuliko muda ulioishi. Kwa mfano kama umeishi miaka 80 utakuwa umekufa kwa zaidi ya miaka milioni ijayo.

Hii ina maana kwamba muda tulionao hapa duniani ni mdogo sana.

Pia ina maana kwamba tuna maisha mamoja tu hapa duniani.

Hii inatakiwa itusukume kuishi maisha haya kwa ukamilifu wake. Na pia katika muda huu mfupi titakaoishi hapa duniani tuweze kugusa maisha ya watu wengine, ili tutakapoondoka tuache kumbukumbu nzuri.

SOMA; Hiki ndio Kitatokea miaka 100 ijayo.

Kujua kwamba utakufa inabidi ikusukume wewe kutumia muda wako vizuri wakati bado unaishi.

kwa mfano njia nzuri ya kutumia hii ni kila siku kuamka na kufikiria kama leo ingekuwa siku yako kuishi ungefanya jambo gani? Kama kuna mtu ulimkosea utamuomba msamaha, kama kuna mtu hujampigia simu muda mrefu utafanya hivyo. Sasa anza kufanya haya leo na maisha yako yatakuwa bora.

Pia chukulia kila mtu unayekutana naye kama anaenda kufa, yaani kila mtu unayeongea naye fikiria dakika chache baada ya kukutana na wewe atakufa. Je utamuonesha umuhimu gani, je utamjali kiasi gani? Hivi ndivyo unavyotakiwa kufikiria kila mara na utajikuta ukifanya yaliyomema wakati wote.

Kwa kumalizia kifo kisikuzuie wewe kufanya mambo makubwa. Usije ukasema hata kama nikifanya bado nitakufa, la fanya kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Kama wote waliotutangulia wangekuwa na mawazo ya aina hii dunia ingekuwa sehemu mbaya sana kuishi.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba siku moja nitakufa, lakini kabla ya siku hiyo nitaishi maisha yako kwa ukamilifu kadiri ya uwezo wangu. Nitaishi kila siku kama siku yangu ya mwisho, nitamjali kila mtu kama vile anaishi siku yake ya mwisho na kila siku nitapambana ili kuacha kumbukumbu nzuri nitakapoondoka.

Tukutane kwenye ukurasa wa nne kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment