Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, January 16, 2015

UKURASA WA 16; Jijengee Utaratibu Wa Kila Siku.

Sehemu kubwa ya mambo unayofanya kila siku unafanya kutokana na tabia ambayo tayari umeshajijengea. Kwa mfano unapoamka asubuhi huenda huwa unasafisha kinywa chako, hii ni tabia uliyoijenga kwa muda mrefu sana na hivyo hutumii nguvu yoyote kuifanya. Yaani huanzi kufikiria kama usafishe kinywa au la, ukiamka tu mpja kwa moja unaelekea kusafishwa kinywa.

Sasa na kazi zako unazozifanya ambazo ni muhimu sana kwako kufikia mafanikio zijengee utaratibu ambao utakujengea tabia ya kufanya kazi zako bila hata ya kufikiria. Kwa mfano kama unataka kujijengea tabia ya kusoma kila siku basi jiwekee utaratibu wa kila unapoamka asubuhi kitu cha kwanz akufanya ni kusoma. Mwanzoni itakuwa vigumu ila baadae itaanza kuwa kawaida kwako.

Anza kujijengea tabia ambazo zitakufanya ufanye mambo yako bila ya kujiuliza mara nyingi.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia leo nitaweka tabia ya kufanya mambo yangu muhimu kwa muda fulani au katika utaratibu fulani ambao utanijengea tabia ya kuweza kufanya bila hata ya kufikiria sana.

Tukutane kwenye ukurasa wa kumi na saba hapo kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment