Hakuna ubishi kwamba binadamu ni viumbe wa kuhukumu. Kila mmoja wetu kwa wakati tofauti anahukumu wengine iwe ni kimya kimya au wazi wazi. Tonatofautiana tu viwango.
Chochote utakachofanya watu watakuhukumu,
Ukifanya vizuri watasema unajifanya mjuaji, ngoja uporomoke, na watadhubutu kukwambia muda sio mrefu utaanguka.
Ukifanya vibaya watakusema wewe ni mzembe, hujitumi, hujui unachofanya.
Kwa kujua hili sasa, usiumizwe na hukumu za viumbe hawa.
Ili kuepuka madhara ya hukumu za viumbe hawa, shikilia mambo haya matatu;
1. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa, hakikisha unakuwa bora zaidi kwa kile unachofanya.
2. Kuwa muaminifu, tekeleza unachoahidi.
3. Kuwa muadilifu, usimfanyie mwingine kile ambacho usingependa kufanyiwa.
Ukishikilia misingi hii mitatu waache waongee mpaka wapasuke, wewe endelea kusonga mbele.
Kuelewa kwa undani zaidi misingi hii mitatu soma makala hii niliyoandika kwenye FIKRA PEVU;
http://www.fikrapevu.com/misingi-mitatu-muhimu-ya-kujijengea-mwaka-2015/
Nakutakia kila la kheri.
0 comments:
Post a Comment