Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, January 21, 2015

#HADITHI_FUNZO; Aliyenusurika Kufa Kutokana Na Tabia Yake Nzuri.

Kulikuwa na mtu mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda cha kutengeneza mabarafu.

Siku moja jioni watu wakiwa wameshajiandaa kuondoka kulitokea tatizo na hivyo ikadibi arudi kulishughulikia. Alipomaliza kushughulikia tatizo lile alikuwa ameshachelewa, milango ilikuwa imefungwa na taa zimezimwa.

Alikuwa amenasa ndani ya kiwanda kile na hakukuwa na mwanga wala hewa. Na pia kwa baridi iliyokuwepo ni hakika kwamba asingefika asubuhi yake, lazima angekufa.

SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

Masaa yalienda huku akiwa ameshakata tamaa,  mara akasikia mtu anafungua milango.

Alishngaa sana nakuona kwamba huu ni muujiza kwake.

Alipoangalia alikuwa ni mlinzi ameingia na tochi yake na akamsaidia kutoka nje.

Wakati wanatoka mtu yule alimuuliza mlinzi walijuaje kwamba yupo ndani kule? Nani alimwambia?

Mlinzi alimjibu hakuna aliyeniambia, kiwanda hiki kina wafanyakazi wapatao 50, lakini ni wewe pekee ambaye huwa unanisalimia asubuhi na kuniaga jioni . Leo asubuhi ulinisalimia, ila jioni sikusikia ukiniaga hivyo nilipata wasiwasi utakuwa humu ndani.

Hakuwahi kufikiri kwamba tabia ndogo tu ya kusalimia mtu ingeweza kuokoa maisha yake.

Tunajifunza nini hapa?

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo unaweza kuvifanya kuwajali wengine, usipoteze chochote na pia siku moja vikakusaidia sana. Usipuuzie vitu hivi, huwezi kujua ni siku gani utahitaji msaada kwa vitu hivi.

MUHIMU; Kama una hadithi yoyote ambayo unaona watu wanaweza kujifunza tafadhali nitumie kwa wasap +255 717 396 253, hata kama ipo kwa kiingereza nitumie nitaiandaa vizuri na kuwashirikisha wengine. Isiwe ndefu sana.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment