Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, January 2, 2015

UKURASA WA 02; Malengo.

Timu za Simba na Yanga zilicheza mpira kwenye uwanja wa taifa, katika mechi hii magoli yaliondolewa. Unafikiri ni nani aliibuka mshindi kwenye mchezo huu?

Nahodha mmoja alipewa meli na aelekee popote meli itakapoenda. Hakupewa uelekeo wala ramani wala kituo anachotakiwa kufika. Aliambiwa akae tu kwenye meli na itakapomfikisha ndio hapo hapo atakuwa amefika. Unafikiri nahodha huyu aliishia wapi?

Kijana mmoja alikwenda porini kuwinda ndege, mara akakutana na kundi kubwa la ndege, kwa tamaa akataka kuwinda kundi lote kwa jiwe moja, unafikiri alipata ndege wangapi?

Kama simba na yanga zitacheza uwanjani bila ya kuwepo kwa magoli hatuwezi kuhesabu nani kashinda.

Kama nahodha ataingia kwenye chombo bila ya uelekeo ataishia kupotezwa na upepo.

Kama utajaribu kuwinda kundi zima la ndege utaishia patupu, yaani bila ya ndege hata mmoja.

Hivi ndivyo maisha yako yatakavyokwenda kama utaishi bila ya malengo.

Malengo yanakupa uelekeo, yanakupa kipimo na yanakuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

Kama mpaka sasa hujaweka malengo ya mwaka 2015, fanya hivyo, kama umeshaweka pitia makala hii; jambo moja muhimu la kufanya ili uweze kuboresha zaidi malengo yako.

Kujifunza zaidi kuhusu malengo soma makala hizi za MALENGO.

Neno la kujiambia kwenye ukurasa huu; Naweka malengo yangu haya ambayo nitayafanyia kazi kwa mwaka mzima. Sitakubali kufanya kitu chochote ambacho hakipo kwenye malengo yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa pili kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

 

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment