Njia mbili za kutengeneza fedha zaidi kwa mwaka huu 2015.
Tunakubaliana wote kwamba fedha ni muhimu. Na haijalishi sasa hivi unazo kiasi gani, bado unahitaji zaidi kwa sababu gharama za maisha zinapanda kila siku.
Kama upo Tanzania, mwaka huu 2015 kuna njia kuu mbili za kupoata fedha zaidi.
1. Njia ya kwanza, ANZISHA BIASHARA AU KUZA BIASHARA YAKO.
Kama bado hujaingia kwenye biashara ingia sasa. Kama ulishaingia ikuze zaidi. Hii ni njia nzuri ya kuongeza kipato chako.
Changamoto za njia hii;
i. Utahitaji kufanya kazi zaidi ya unavyofanya sasa.
ii. Utahitaji kufikiri tofauti na unavyofikiri sasa
iii. Utahitaji kuacha kujumuika na watu wengi unaojumuika nao sasa.
2. Njia ya pili; JITOE UFAHAMU,
Njia ya pili unayoweza kutumia kupata fedha zaidi mwaka huu ni kujitoa ufahamu, kumtafuta mwanasiasa ambaye unaona ana kiu kubwa ya kushinda uchaguzi. Mwambie maneno mazuri atakayotaka kusikia, mpambe, jiite mtabiri, watabirie wote watakaompinga kifo. Anzisha ukurasa wake kwenye mtandao, onesha kazi zake, mpambe na jitahidi kuwa mnafiki unavyoweza ili akuone kweli unafanya kazi.
Changamoto za njia hii;
i. Nafasi hizo ni chache,
ii. Baada ya uchaguzi utu wako umeisha labda usubiri tena miaka mitano ijayo.
iii. Ukishatumika umeisha, na hata imani ya wengine kwako itashuka sana.
Nakushauri utumie njia ya kwanza kwa sababu ndio itakayokuletea uhuru wa kweli.
Kama unataka kujifunza zaidi jinsi ya kutumia njia ya kwanza karibu huku www.kisimachamaarifa.co.tz
N:B Ajira itaendelea kukupatia kipato unachopata sasa maana ongezeko la mshahara halipo kwenye maamuzi yako.
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
0 comments:
Post a Comment