Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, January 4, 2015

Hii Hapa Ni Njia Rahisi Ya Kujitolea Uvivu Mwaka Huu 2015

Mara nyingi huenda umekuwa mtu wa kuahirisha mambo.
Unaweka mipango yako vizuri ila inapofikia utekelezaji unaahirisha na kusema utafanya baadae au utafanya kesho.
Sasa kuna dawa moja ya kuondoa kabisa uvivu huu.
Fikiria hivi, ambao ndio ukweli;
Wakati wewe umelala kuna mwenzako anapiga mzigo ili kufanikiwa.
Wakati wewe unakula kuna wenzako wanatokwa jasho ili kuboresha maisha yao.
Wakati wewe unapiga umbea na kusengenya kuna wenzako wanafikiria ni wapi wawekeze ili wapate faida zaidi.
Wakati wewe unafuatilia msanii maarufu ana skendo gani, msanii huyo yuko studio anarekodi wimbo ambao utampa umaarufu zaidi.
Chochote unachofanya jua kuna wenzako wanapambana kuboresha maisha yako.
Hivyo acha kupoteza muda, amka sasa na anza kuboresha maisha yako.
2015 uliyokuwa unaisubiri ndio hii hapa, usijipe tena sababu.
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Tafadhali Washirikishe wengine..

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment