Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, January 8, 2015

UKURASA WA 08; Nidhamu Ndio Nguzo, Ukiikosa Utaanguka.

Moja ya vitu muhimu unavyotakiwa kuwa navyo ili uweze kufikia mafanikio ni nidhamu. Kwa kuwa na nidhamu(hasa nidhamu binafsi) utaweza kuweka malengo na mipango yako mwenyewe na kisha kuweza kuitekeleza.

Ukikosa nidhamu utajikuta unashindwa kutekeleza kile ulichopanga mwenyewe na mwishowe ukashindwa kufanikiwa.

Mwaka huu 2015 amua kujijengea nidhamu binafsi, amua nguzo yako kubwa iwe ni nidhamu. Jiheshimu mwenyewe, ukisema nitafanya jambo fulani hakikisha unalifanya kweli. Pia waheshimu wengine na wafanyie kile ambacho ungependa kufanyiwa wewe.

Mtu mwenye nidhamu anawez akuanzia chini kabisa na kukua hatimaye kufikia mafanikio makubwa. Mtu ambaye hana nidhamu hata akianzia juu kiasi gani anaishia kuanguka.

Usikubali wewe kuwa mmoja wa wale ambao wataanguka vibaya kutokana na ukosefu wa nidhamu.

TAMKO LA LEO;

Najua kwaba nidhamu ndio nguzo kuu ya kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yangu. Najua ukosefu wa nidhamu utanifanya nianguke haraka sana. Hivyo kuanzia leo nitajijengea nidhamu binafsi kwa kuheshimu na kutekeleza yale niliyopanga kufanya. Pia nitajiheshimu na kuheshimu wengine.

Tukutane kwenye ukurasa wa tisa kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment