Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, January 8, 2015

Hakuna Anayejua Anachofanya, Na Huo Ndio Uzuri Wa Maisha.

Huenda kuna wakati ambao unafika na unahisi hujui ni kitu gani unafanya kwenye haya maisha. Na mara nyingi hutokea pale unapokumbana na changamoto au matatizo. Hali hiyo inaweza kukufanya hata ukate tamaa.

Leo nina habari nzuri kwako, haupo mwenyewe, binadamu wote hakuna anayejua anachokifanya hapa duniani. Yaani hakuna mwenye uhakika na kile anachokifanya. Tunaishi maisha ya kujaribu na kukosea, unajaribu hiki unakosea unajaribu kingine tena mpaka unapatia.

Watu wanazaliwa, wengine wanakufa wakiwa wadogo kabisa, wengine wanakufa wakiwa vijana na wengine wanakufa wakiwa wazee.

Watu wanaanza kusoma wengine wanafeli kwenye ngazi za awali kabisa, wengine wanafeli kwenye ngazi za juu wengine hawafeli kabisa.

Wakati mwingine yule aliyefeli anakuja kuwa na mafanikio kuliko aliyefaulu.

Watu wanapendana, wanachumbiana, wanaoana kwa harusi kubwa na siku chache baadae wanaachana.

Hivyo ndivyo maisha yalivyo, hakuna anayejua anachofanya.

Fanya kile unachokifanya kwa juhudi na maarifa, fanya kila linalowezekana upande wako japo haitakufanya uondokane kabisa na changamoto za maisha.

Furahia maisha yako.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment