Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, March 22, 2015

UKURASA WA 81; Achana Na Ubishi, Hautakusaidia Lolote.

Ukishaamua ni kitu gani ambacho unataka kufanya kwenye maisha yako, basi hapo ndio unafunga mjadala. Usijiingize kwenye ubishi kuhusiana na kile unachofanya.

Kama umeshaamua kwamba wewe utakuwa mjasiriamali, anza kufanya ujasiriamali, jua kabisa mpaka unakufa wewe utakuwa mjasiriamali. Kuanza kuingia kwenye ubishi kama mjasiriamali anazaliwa au anatengenezwa hakutakusaidia lolote. Kuanza kuingia kwenye ubishi kwamba kama kweli utaweza kufanikiwa kwenye ujasiriamali au la hautakusaidia chochote.

SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.

Waache wasiojua matumizi ya muda wao waendelee kubishana, wewe tumia muda huo kufanya kile unalichopanga kufanya.

Kama kuna kitu hujui, jifunze.

Kama kuna mahali unakwamba omba msaada, angalia wengine walifanyaje.

Usiingie kwenye ubishi, iwe na mtu au na nafsi yako mwenyewe. Usianza kujiuliza kama maamuzi uliyofanya ni sahihi au la. Jua kwamba hayo ndio maisha uliyochagua kuyaishi na anza kuyaishi haraka sana.

Muda wako ni mfupi sana na una vitu vingi vya kufanya, una vitu vingi vya kujifunza na una watu wengi wa kuwahudumia.

Epuka ubishi ambao hautakuongezea maarifa zaidi, au fursa zaidi au fedha zaidi. Asilimia 99 ya ubishi unaingia hapo, achana nao.

SOMA; Mambo KUMI Ya Kufanya Ili Usiishi Maisha Ya Majuto.

TAMKO LA LEO;

Nimeshaamua kitu ambacho ninakitaka kwenye maisha yangu. Sitarudi tena nyuma na kuanza kujihoji kama nilifanya maamuzi sahihi au la. Sitoingia kwenye mabishano kama naweza au la. Nitatumia muda wangu vizuri kufanya kile ambacho nimechagua kufanya na nina hakika nitafikia mafanikio makubwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 82 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment