Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, March 13, 2015

NENO LA LEO; Kuwa Unachotaka Kuwa, Sema Unachojisikia Kusema, Kwa Sababu…

Be who you are and say what you feel, because those who mind don't matter, and those who matter don't mind. -Dr. Seuss

Kuwa yule unayetaka kuwa na sema kile unachojisikia kusema, kwa sababu wale watakaojali sana sio wa muhimu kwako na wale ambao ni wa muhimu kwako hawatajali sana.

Katika maisha yako ni rahisi sana kujishawishi uishi maisha ambayo huyapendi ili tu kuwapendeza watu wengine. Hii ni dhuluma kubwa sana kwako binafsi. Usiache kufanya kile unachopenda kufanya au kusema kile unachopenda kusema kwa sababu tu unahofia watu watakuchukuliaje.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Kama utafanya kitu ambacho ni muhimu kwako na mtu akachukia au hata kuamua kuwa mbali na wewe basi juamtu huyo hakuwa muhimu kwako na hata ungefanya nini usingeweza kumlazimisha aw muhimu.

Mtu ambaye ni muhimu kwako ataheshimu maamuzi yako hata kama hakubaliani nayo. Hii ni kwa sababu anakujali na vitu vodogo vidogo haviwezi kumuondolea yeye kukujali wewe.

Ishi maisha yako, utawajua ni wapi ambao ni muhimu kwako na ni wapi ambao wapo wapo tu.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Hizi Ndio Siri 21 Za Mafanikio

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment