"In giving advice, seek to help, not please, your friend." – Solon
Katika kutoa ushauri, toa ushauri utakaosaidia na sio ushauri utakaomridhisha rafiki yako.
Hii ni changamoto kubwa sana hasa pale rafiki yako anapokosea. Mara nyingi utaogopa kumwambia kwa sababu unafikiria anakuchukuliaje.
Au rafiki anakuomba ushauri na kwa maelezo yake kuna kitu anapendelea kufanya na wewe unaona kitu hiko ni kikwazo kwake je upo tayari kumwambia aache kitu hiko? Hapo unajua kabisa kwamba kumwambia aache kitu hiko utaumiza hisia zake.
SOMA; TAFAKARI; Unachagua Upande Upi?
Ni bora kutoa ushauri ambao utamsaidia rafiki yako hata kama utamuumiza kuliko kumpa ushauri wa kumridhisha halafu baadae akapata matatizo zaidi. Atajua hukumshauri vizuri na atakuona wewe sio rafiki mwema kwake.
Nakutakia siku njema.
0 comments:
Post a Comment