Kuna wakati ambao unakuwa na matatizo mengi sana kwenye maisha yako na kufikiri kwamba kama ungekuwa kama mtu fulani huenda usingekuwa na matatizo.
Labda huna kazi, unafikiri kama ungekuwa na kazi kama watu unaowaona wana kazi basi maisha matatizo yako yangekwisha.
Labda wewe ni mfanyakazi wa kawaida na unafikiria kwamba kama ungekuwa bosi basi matatizo yako yote yangeisha.
SOMA; Njia Mbili Za Uhakika Za Jinsi Ya Kupata Fedha.
Au unafanya biashara na kuona biashara yako haiendi vizuri, unafikiria kama ungekuwa unafanya biashara wanazofanya wengine basi matatizo yako yangekwisha…
Unaweza kufikiria hivi utakavyo, lakini ukweli ni kwambaaa
Kila mtu ana matatizo.
SOMA; USHAURI; Umuhimu Na Jinsi Ya Kutofautisha Biashara Na Maisha Ya Kawaida.
Unaweza kuona ukiwa na kazi hutakuwa na matatizo, lakini wafanyakazi wengi sana wana matatizo kuliko hata ambayo unayo wewe.
Unaweza kuona bosi wako hana matatizo, ila ukweli ni kwamba anaweza kuwa na matatizo makubwa kuliko uliyonayo wewe.
Unaweza kuona biashara za wengine hazina matatizo kama unayopata wewe, ila ukipewa biashara hizo unawez akukimbia kabisa.
Kwa kuw akila mtu ana matatizo kwa hiyo tufanyeje sasa?
Fanya hivi, acha kuangalia nani hana matatizo, acha kuangalia matatizo yako sana na anza kuangali ni jinsi gani unaweza kuboresha maisha yako, ni jinsi gani unaweza kuyatyumia matatizo yako kuwa bora zaidi.
SOMA; Hizi Ndio Siri 21 Za Mafanikio
TAMKO LA LEO;
Najua kwamba kila mtu ana matatizo. Naweza kuona kwamba watu fulani hawana matatizo kama mimi ila nikipewa maisha yao nitashindwa kuyaendesha. Nitawekeza nguvu zangu kuboresha maisha yangu kila siku na kuangalia ni jinsi gani naweza kuyatumia matatizo ninayopitia kufaidika zaidi.
Tukutane kwenye ukurasa wa 18 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment