Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, March 15, 2015

UKURASA WA 74; SAMEHE…

Labda tuseme kuna mtu amekuudhi sana kwenye maisha yako, amekufanyia jambo baya sana kiasi kwamba maisha yako yameharibika sana, una haki ya kumchukia, si ndio?

Labda tuseme mtu huyu alifanya jambo ambalo lilikupa hasara kubwa sana kwenye maisha. Au kuharibu maisha yako sana. Au hata kujaribu kuondoa uhai wako, ila kwa njia moja au nyingine ukapona.

SOMA; Fanya Mambo haya matatu kuwa na maisha bora na yenye furaha.

Una haki ya kumchukia mtu huyu, kuwa na kinyongo naye na wakati wowote unapomuona kuchukia. Una haki kabisa ya kukataa kukutana nae, na hata kutokutaka kushirikiana nae tena. Au hata kutoongea nae hata kama ataomba msamaha.

Unaweza kuona hili ni suluhisho kwako au una haki ya kufanya hivi, ila leo nakuambia kwamba unafanya makosa makubwa sana kwenye maisha yako.

Wewe ndiye unayeendelea kuumia kwa hali hiyo ya kuwa na kinyongo. Wewe ndiye unayeshindwa kufanya mambo yako vizuri kwa sababu ya kujiwekea kinyongo. Wakati kwa upande wa pili mwenzako anaendelea na maisha yake.

SOMA; NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Msamaha

SAMEHE mtu yeyote ambaye umemuwekea kinyongo mpaka sasa. Ondoa kabisa kinyongo kwenye moyo wako na endelea na maisha yako. Hata kama hutaki kushirikiana nae tena, usiendelee kuweka kinyongo. Msamehe kwa yote aliyofanya na endelea na maisha yako.

Kwa kufanya hivi utakuwa umenunua uhuru ambao uliupoteza kwa kuweka kinyongo.

TAMKO LA LEO;

Leo hii nawasamehe wote ambao wamewahi kunikosea kwenye maisha yangu(wataje majina). Naondoa vinyongo vyote ambavyo nilikuwa nimeweka na sasa nimekuwa mtu huru. Sitakuja kuweka tena kinyongo kwenye maisha yangu. Mtu anaponikosea naachana nae na kuendelea na maisha yangu. Muda wangu ni wa thamani sana kuupoteza kwa kushikilia vinyongo vya watu ambao hawanijali.

SOMA; UKURASA WA 68; Furaha Ya Leo Ni Kikwazo Maisha Yako Yote…

Tukutane kwenye ukurasa wa 75 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment