Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, March 1, 2015

UKURASA WA 60; Je Una Ujasiri Huu?

Katika maisha yetu ya kila siku tunafanya maamuzi mbalimbali. Maamuzi mengine yanakuwa makubwa na magumu, na maamuzi mengine yanakuwa madogo na rahisi.

Mara nyingi watu hufanya maamuzi makubwa na magumu wakiamini kwamba kuna watu nyuma yao ambao watamsaidia pale mambo yatakapokuwa magumu zaidi.

SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Ugumu Wa Kufanya Maamuzi.

Ni kweli, hili ndio lengo kubwa la kuishi kwneye jamii, kuwa na ndugu na marafiki, ili kusaidiana.

Lakini je una ujasiria wa kufanya maamuzi ambayo utayasimamia hata kama watu wote hawatakuwa upande wako? Kama watu wote watakuacha na maamuzi yako, je na wewe utayakimbia au utaenelea kuyasimamia?

Kama una ujasiri huu utaweza kufikia mafanikio makubwa. Kama huna ujasiri huu utaishia kutangatanga na maamuzi mpaka maisha yako yatakapofika ukingoni.

Kama unaona maamuzi unayotaka kufanya ni makubwa sana na kama usipopata wa kukusaidia yatakuwa na madhara makubwa sana kwako ni heri usifanye maamuzi. Maana wale unaowategemea sana watakuangusha, tena kwenye wakati ambao unawahitaji sana.

SOMA; UKURASA WA 44; Usiondoe Macho Kwenye Zawadi…

TAMKO LA LEO;

Nina ujasiri wa kufanya maamuzi ambayo nitayasimamia katika hali yoyote ile hata kama dunia nzima itakuwa kinyume na mimi. Mimi ndio najua umuhimu wa maamuzi hayo na sitakubali kuyasaliti. Nategemea watu wanisaidie katika maamuzi hayo, ila hata wakiniacha nitaendelea kukomaa mpaka nitakapopata kile ninachotaka.

Tukutane kwenye ukurasa wa 61 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; NENO LA LEO; Jinsi Unavyoweza Kufikia Ndoto Zako…

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment