Tunaishi kwenye jamii ambazo kila mtu anaweza kutoa ushauri kwenye jambo lolote lile. Usipokuwa makini unaweza kuchukua ushauri ambao sio mzuri na ukakuingiza kwenye matatizo makubwa au kukupotezea muda.
Kuna ushauri ambao ni wa bure, ambao unatolewa na kila mtu. Hiki ni kitu hatari sana, usikimbilie kuufuata, utaumia.
SOMA; USHAURI ADIMU; Chukua Ushauri Kwa Mtu Huyu Tu, Achana Na Wengine Wote.
Aina za ushauri huu ni kama; biashara fulani inalipa kweli, ona fulani kaanza kuifanya juzi juzi tu na sasa hivi ana mafanikio. Ubaya wa ushauri huu utapew ana mtu ambaye hafanyi hiko anachokushauri na wala hajachukua muda kuchunguza na kujua ni hatua gani mtu huyo amepitia mpaka akapata mafanikio hayo. Unapopata ushauri kama huu usikimbilie kufanya, bali chukua muda wako kufanya utafiti wa kile ulichosikia, asilimia 80 ni uongo.
SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.
Kuna ushauri kutoka kwa watu ambao wanafanya kitu, au wamefanya utafiti wa kutosha kuhusu kitu fulani. Hawa ndio watu ambao unatakiwa kusikiliz ana kuchukua ushauri wao. Na hata utakapouchukua bado huwezi kuutumia moja kwa moja, utahitaji kuangalia ni jinsi gani unaweza kuboresha zaidi na kulingana na uwezo wako na mazingira yako.
Usitegemee ushauri wowote utakaopokea utafanya kazi kwa silimia 100, wewe una nafasi kubwa sana ya kuufanya ushauri huo ufanye kazi. Usiwe mvivu wa kufikiri, kupanga na kutekeleza mipango yako. Hakuna ushauri utakaoweza kufanya kazi kwako kama wewe hutafanya kazi.
Pamoja na kupata ushauru mzuri, bado unahitaji kufanya kazi kubwa sana ya kuufanya ushauri huo ukuzalishie matunda mazuri.
SOMA; NENO LA LEO; Ushauri Bora Unaoweza Kutoa Kwa Rafiki Yako.
TAMKO LA LEO;
Najua suahuri wa bure una gharama kubwa sana kama nitauchukua biala ya kufanya utafiti na kuona nitautumiaje. Ushauri wowote nitakaopokea kutoka kwa watu, nitaufanyia utafiti kwanza na kuona ni jinsi gani naweza kuutumia vizuri. Najua hakuna ushauri unaoweza kufanya kazi kwa asilimia 100, hivyo nafasi yangu ni kubwa sana kwenye kufanyia kazi ushauri.
Tukutane kwenye ukurasa wa 77 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment