Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, March 15, 2015

Matumizi Mawili Ya Mbegu Za Mahindi.

Kama una mbegu za mahindi, unaweza kufanya vitu viwili tu na mbegu hizo.
Unaweza kuzila, yaani kufanya chakula. Na unaweza kula kama ugali, makande, au hata mahindi ya kukaanga. Ni chanzo kizuri sana cha wanga, na nguvu kwenye mwili.
Jambo la pili unaloweza kufanya na mbegu hizi za mahindi ni kuzipanda na kuzipa huduma nzuri kisha zikazaa mbegu nyinhi zaidi na ukapata mahindi mengi zaidi.
Mbegu unazo sasa, unazipandaje?
Mbegu uliyonayo ni hiyo shilingi elfu moja ambayo unanunua nayo soda kila siku.
Mbegu uliyonayo ni hilo saa moja unalotumia kufuatilia habari, kubishana na kufanya mambo ambayo hayana faida kwako.
Mbegu unazo nyingi sana, je unaamua kuzitumiaje? Kula sasa hivi upate raha, utamu wa soda, utamu wa mitandao au utawekeza ili baadae upate zaidi?
Uchaguzi ni wako, hakuna anayekushikia fimbo.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment