Inapokuja kwneye kazi, biashara au jambo lingine tunalofanya ili kutengeneza kipato, mara zote huwa kuna kuwa na jambo moja la ziada la kufanya.
Kwa mfano kama umesema leo utafanya vitu fulani vitatu, utakapomaliza kufanya vitu hivyo utaona kuna kitu kingine cha ziada cha kufanya.
SOMA; Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia Malengo Yako Kwa Haraka.
Ukiwa unatembelea mitandao ya kijamii, facebook, instagram, twitter, na hata wasap. Kuna kitu kimoja cha ziada cha kuangalia, kuna picha moja ya ziada ya kuangalia, kuna kundi moja la ziada la kuangalia.
Tatizo kubwa haliishii hapa kwenye kitu cha ziada cha kuangalia, bali linakuwa kubwa pale kitu hiki kimoja cha ziada, kinazaa kitu kingine na kingine na kingine.
Ulifikiri kitu hiki kimoja cha ziada unachotaka kufanya kingechukua dakika tano, unashangaa nusu saa imepita, mara saa moja imepita na bado unafanya kitu kile ulichofikiri ni cha ziada. Na kwa bahati mbaya sana kitu hiki cha ziada sio muhimu sana na kingeweza kusubiri.
SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo.
Hasara kubwa zaidi ya kitu hiki cha ziada tunachotamani kufanya inakuja pale kinapotumalizia muda wetu wa kupumzika, muda wa kuwa na wale tunaowapenda na muda wa kufanya mambo ambayo ni muhimu zaidi kwetu.
Ili kuondokana na hali hii, kwanz akuwa na ratiba ya vitu unavyotaka kufanya kwenye siku na vifanye hivyo tu. Pili jua kwmaba sio lazima ufanye kila kitu na vitu vingine vinaweza kusubiri. Tatu kuwa na muda maalumu wa kutembelea mitandao ya kijamii na heshimu muda huo, yaani usizidishe hata dakika moja.
SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwmaba vitu vya kufanya huwa haviishi. Kila wakati nitakuwa na jambo moja la ziada ambalo nitahitaji kulifanya. Mara nyingi jambo hili sio muhimu sana na linanipotezea muda. Nitaepuka hali hii kwa kuwa na ratiba ninayoiheshimu na kuwa na muda maalumu wa kutembelea mitandao ya kijamii.
Tukutane kwenye ukurasa wa 88 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment