Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, March 18, 2015

UKURASA WA 77; Kama Watu Hawakupingi Unakosea Sana.

Kwenye kazi au biashara unayofanya, au hata maisha unayoishi kuna kipimo rahisi sana cha kuweza kujua kama unachofanya ni cha tofauti au ni cha kawaida.

Kipimo hiko ni muitikio wa watu kwa kile unachokifanya. Kama kila mtu anakubaliana na wewe kwa kile unachofanya na jinsi unavyofanya basi utakuwa unafanya makosa makubwa sana. Utakuwa unafanya kitu ambacho ni cha kawaida sana kwao na hivyo hakitawafanya hata wajali.

SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

Lakini kama watu watakupinga, watakuambia haiwezekani, watakupa ushahidi wa waliojaribu wakashindwa, watakupa hata historia ni jinsi gani haiwezekani basi hapo furahia sana maana unaanza kufanya jambo ambalo sio la kawaida.

Na uzuri wa kufanya jambo ambalo sio la kawaida ni kwamba unaleta mabadiliko makubwa, unapata mafanikio makubwa na unawasaidia wengi zaidi.

Kumbuka jambo tunalozungumzia ufanye hapa lisiwe kinyume na sheria au taratibu za kawaida za maisha ya binadamu. Kwa kifupi lisiwe na madhara kwa watu au eneo unalofanyia.

SOMA; NENO LA LEO; Furahia Kupingwa…

Kufanya jambo jipya, ambalo halijazoeleka kunahitaji ujasiri mkubwa sana. Ni ujasiri huu ndio unaoweza kukutenga na wale ambao hawataweza kufikia mafanikio makubwa. Kama na wewe umekosa ujasiri huu mtaendelea kuwa pamoja, hamuendi mbali na mnaendelea kurudishana nyuma.

Kama unataka kuamini huna jambo kubwa na la tofauti unalofanya kwenye maisha jaribu moja kati ya haya, jaribu wka wiki moja tu halafu utaona muitikio wa watu ukoje.

1. Kama umeajiriwa, wahi kazini mapema sana kabla ya watu wengine wote. Fanya kazi zako kwa makini na kamilisha kwa wakati, mapumziko yakiisha rudi kwenye kazi yako haraka. Watu wakiwahi kuondoka, ongeza muda kidogo, yaani kuwa wa mwisho kuondoka. Kukitokea jambo lolote linalohitaji msaada kuwa wa kwanz akujitolea. Fanya hivi na utaona ni jinsi gani watu watakavyokupinga na kukusema vibaya, japo hujaingilia maisha yamtu yeyote.

2. Kama unatumia pombe na una marafiki ambao huwa unakunywa nao, waambie wewe hunywi tena pombe, ukikutana nao agiza maji, au juisi na baada ya muda omba ruhusa ya kuondoka ili uwahi kufanya mambo yako mengine. Utaona jinsi ambavyo watakupinga, japo ni marafiki zako na unalolifanya ni jema kwa maisha yako.

3. Kama unafanya biashara, fanya kwa utofauti, toa huduma za kipekee kwa wateja wako, hakikisha hawezi kuzipata popote. Zungumza nao vizuri, unacheka nao, unawasiliana nao. Halafu utaona wafanyabiashara wengine watakavyokupinga, na wengine kudiriki kusoma unatumia uchawi.

Fanya zoezi moja hapo kwa wiki moja tu, halafu uone muitikio wa watu ukoje. Halafu ukikamilisha wiki moja, ongeza nyingine na nyingine na nyingine mpaka huo utakapokuwa utaratibu wako wa maisha, na watu watazoea tu, na wakishazoea inakuwa ni kawaida, itabidi utafute kingine cha kufanya ambacho watu hawajazoea.

SOMA; UKURASA WA 40; Amua Kuwa Wewe…

TAMKO LA LEO;

Najua kabisa kwamba kama ninafanya jambo la tofauti ambalo watu hawajalizoea nitapingwa na kukatishwa tamaa. Hivyo kipimo changu cha kujua kama ninachofanya ni cha tofauti ni muitikio wa watu. Kama jambo lolote ambalo nafanya hakuna hata mmoja anayepinga au kushangazwa, basi ni jambo la kawaida sana na nitaachana nalo.

Tukutane kwenye ukurasa wa 78 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment