Kwa masikitiko makubwa sana naomba kukuambia kwamba bado hujapata muda wa kuishi. Na kama hutachukua hatua mapema basi utajikuta mpaka siku unakufa hujapata muda wa kuishi.
Kuna usemi maarufu unasema kwamba maisha ni kile kinachoendelea wakati wewe unaweka mipango mingine.
SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.
Huu ni ukweli kabisa. Tumekuwa watu wa kuweka mipango tukiamini kwamba mpango huu ukikamilika basi ndio tutaanza maisha yetu vizuri. Ukiwa shuleni unafikiria nikimaliza tu masomo na kuanza kazi basi maisha yangu yatakuwa mazuri. Ukimaliza shule na kupata kazi unasema nikishaoa/olewa na kuwa na familia yangu basi maisha yangu yatakuwa mazuri sana. Unapooa/olewa unasema nikishamaliza kulea watoto maisha yangu yatakuwa viuzuri.
SOMA; NENO LA LEO; Hiki Ndio Chanzo Cha Nguvu Zako.
Unaendelea kusogeza maisha mbele kama vile kuna siku moja utaamka na mipango yote uliyoweka ikawa imetekelezwa.
Ukweli ni kwamba maisha hayaendi hivyo. Hakuna siku ambayo utakuwa umemaliza mipango yako yote. Na kwa bahati mbaya sana mipango hii inaendelea kuongezeka kila siku.
Kumbuka maisha ni sasa, maisha ni hapo ulipo. Pata muda wa kuishi maisha yako. Pata muda wa kuyafurahia kwa hapo ulipo na hivyo ulipo. Furahia kila wakati wa maisha yako kwa sababu huna wakati mwingine, unaweza kufa kesho, nani ajuaye?
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)
TAMKO LA LEO;
Nitahakikisha napata muda wa kuishi. Najua ni rahisi sana kukosa muda huu kama nitakuwa naweka maisha baada ya mipango yangu. Pamoja na mipango mizuri niliyojiwekea, maisha ni sasa hata kabla sijakamilisha mipango hii.
Tukutane kwenye ukurasa wa 25 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment