Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, March 11, 2015

UKURASA WA 70; Jua Kwa Nini Unafanya Unachofanya..

Kila mtu anajua NI NINI anachofanya. Hata kama hakimpi faida au hakina manufaa kwake ila anajua anachofanya. Na kama mtu hajui anachofanya basi anaweza kuwa na matatizo makubwa zaidi.

SOMA; NENO LA LEO; Akili Ndogo, Akili za Kawaida Na Akili Kubwa.

Baadhi ya watu wanajua JINSI YA KUFANYA wanachofanya. Ni baadhi na hawa wanapata faida kiasi ukilinganisha na wale ambao hawajui jinsi ya kufanya. Baadhi ya watu, na huenda ni wengi hawajui jinsi ya kufanya kile wanachofanya. Kwa mfano mtu anaweza kujua wkamba anafanya biashara, ila hajui mbinu bora za kufanya biashara hiyo ili afikia mafanikio makubwa sana.

Kuna watu wachache sana, na hapa namaanisha wachache kweli, ambao wanajua KWA NINI wanafanya kile wanachofanya. Hawa ni watu ambao wanapata mafanikio makubwa sana na wanakwenda hatua ya ziada. Hawa ni watu ambao wanaleta mabadiliko makubwa sana, wanakuwa viongozi na wanaheshimika sana.

SOMA; Kitu Kimoja Unachohitaji Ili Kufanikiwa Kama Unaanzia Chini Kabisa.

Kama na wewe unataka kuleta mabadiliko, unataka kufanikiwa sana na unataka kwenda hatua ya ziada, jua kwa nini unafanya kazi au biashara unayofanya. Jua ni kitu gani kinakusukuma kutoka kitandani asubuhi na kwenda kwenye shughuli zako, uksihakijua hiki hakun chochote ambacho kinaweza kukuzuia kupata kile unachotaka.

Kwa taarifa tu; fedha haiwezi kuwa kwa nini unafanya unachofanya.

TAMKO LA LEO;

Najua kwa nini nafanya kazi au biashara ninayofanya. Hiki ndio kinachonisukuma kufanya zaidi hata pale ninapokutana na vikwazo au changamoto. Sitokata tamaa, sitorudi nyuma mpaka nitimize lengo langu la KWA NINI nipo hapa duniani.

SOMA; Hivi ndivyo unavyoweza kununua Hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

Tukutane kwenye ukurasa wa 71 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment