Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, March 8, 2015

UKURASA WA 67; Kama Huwezi Kufanya Miaka 50 Acha..

Jambo lolote ambalo unafanya au unataka kufanya hakikisha utakuwa tayari kulifa kwa miaka hamsini ijayo.

Yaani upo tayari kufanya jambo hilo bila ya kuchoka au kukata tamaa kwa miaka hiyo hamsini.

Kwa nini miaka hamsini?

Kwanza mafanikio hayatatokea haraka kama ambavyo wengi wanakudanganya au utakavyofikiria. Mafanikio yatakuchukua muda mrefu kidogo kuweza kuyafikia.

SOMA; Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.

Pili mafanikio hayatatokea mara moja kama ajali. Bali mafanikio yanatokana na mambo madogo madogo unayofanya kwa kurudia rudia kila siku. Hivyo unahitaji muda mrefu wa kufanya hiko unachofanya ndio uweze kuona matokeo unayotarajia.

Tatu, unahitaji kupenda kile unachokifanya ndio uweze kufikia mafanikio, sasa kama utakuwa tayari kufanya kitu miaka hamsini utakuwa unakipenda kweli. Na unapopenda unachofanya, unafanya kazi kwa juhudi zaidi, unakuwa na maarifa zaidi na utakuwa na ubunifu mkubwa.

SOMA; Sheria 12 Kwa Wanaoanza Biashara Kutoka Kwa Bilionea Mark Cuban.

Hivyo jichunguze je hiko unachofanya sasa uko tayari kukifanya kwa miaka hamsini ijayo? Kama haupo tayari anza kufikiria ni kitu gani upo tayari kukifanya kwa muda huo.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia leo nitafanya kitu ambacho nipo tayari kukifanya kwa miaka 50 ijayo. Sitababaishwa na vitu vya muda mfupi kwa sababu najua mafanikio yanahitaji muda, uvumilivu na ubunifu. Nitaendelea kufanya kile kinachoniletea mafanikio kila siku bila ya kukata tamaa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 68 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment