Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, March 24, 2015

UKURASA WA 83; Unahitaji Kuwa Sahihi Au Kuwa Na Furaha?

Kuwa sahihi na wakati huo huo kuwa na furaha ni kama vitu viwili ambavyo haviwezi kutokea kwa wakati mmoja. Na hii ni sahihi sana hasa kwenye maisha yako na mahusiano yako na watu wengine.

Ni vigumu sana wewe kuonesha kwamba upo sahihi na wakati huo huo ukawa na furaha.

Hii inatokea sana kwenye mahusiano yetu na watu wengine. Mtu anaweza kuwa anafanya jambo ambalo huenda hukubaliani nalo, au sio sahihi kwa upande wako. Kwa kumpinga na kumwambia yeye hayupo sahihi ila wewe ndio upo sahihi, kutamfanya atetee sana upande wake. Katika hali hii mahusiano yanakuwa mabovu na wote mnakosa furaha.

SOMA; Siri Kubwa Unayotakiwa Kujua Kwenye Mahusiano Ya Kibiashara.

Kutaka kuwa sahihi bila ya kujali furaha inayotokana na mahusiano mazuri imekuwa ndio chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano mengi ya kirafiki na hata ndoa pia.

Badala ya kutaka kuonekana kwamba wewe ndio sahihi sana, hebu wape wengine nafasi ya kukosea, hebu wape wengine nafasi ya kufanya kile wanachoona ni sahihi kwao na furahia mahusiano mazuri mnayoendelea kuwa nayo.

SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Kinachokurudisha Nyuma.

Mara nyingi vitu ambavyo watu wanabishania kuonekana sahihi ni vidogo sana na havistahili kukuzwa kiasi hiko mpaka kupelekea mahusiano kuwa mabaya na hata kuvunjika.

TAMKO LA LEO;

Najua kwenye mahusiano niliyonayo na watu wengine, ni vigumu sana kuwa sahihi na wakati huo huo kuwa na furaha. Najua vita ya kutaka kuonekana nipo sahihi zaidi itaniondolea furaha yangu kwa kuvunja mahusiano niliyonayo. Nitawapa wengine nafasi ya kujiona wapo sahihi, nitawapa nafasi ya kukosea na nafasi ya kufanya kile ambacho ni sahihi kwao.

SOMA; NENO LA LEO; Ufunguo Muhimu Wa Ufunguo Wa Mafanikio.

Tukutane kwenye ukurasa wa 84 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment