Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, March 3, 2015

UKURASA WA 62; Sifia Kilicho Kizuri Na Utaona Vilivyo Vizuri Zaidi.

Kile unachosifia kinakua zaidi.

Kile unachokazana kuangalia ndio utazidi kukiona zaidi na zaidi.

Hii ina maana gani basi.

Kama utaona maisha ni magumu, na kukazana kuangalia ugumu wa maisha yataenelea kuwa magumu kila siku.

Kama utaona maisha ni mazuri ila yana changamoto za hapa na pale ambazo zinayafanya yawe mazuri zaidi utayafurahia kila siku.

SOMA; UKURASA WA 14; Kataa Kupokea Chochote Kizuri, Na Kubali Hiki…

Inakwenda mbali zaidi, kama una mwenza, mke au mume na ukawa unakazana kumsema kwa mabaya yake tu, utazidi kuyaona hayo mabaya kila siku. Ila kama utaamua kuangalia yale mazuri na ukamsifia kwa mazuri hayo, utaona mazuri kila siku.

Kama unamfanyakazi, au mfanyakazi mwenzako na ukakazana kuangalia mabaya yake tu, utayaona zaidi, ila ukiangalia yale mazuri uhusiano wenuutaimarika zaidi.

Katika maisha yako, katika mahusiano yako, kazana kuangalia kile kilicho bora, kazana kuangalia upande mzuri na achana na yale mabaya. Sio kwamba unakimbia matatizo, ila kama tatizo huwezi kulitatua mara moja, kama hali ya maisha au tabia ya mtu, kuendelea kuliangalia hakutakusaidia zaidi ya kuyafanya maisha kuwa magumu zaidi.

SOMA; Hii Ndio Faida Ya Kuboresha Maisha Yako...

TAMKO LA LEO;

Nitasifia kile ambacho ni kizuri. Katika maisha yangu na katika mahusiano yangu nitaangalia kile kilicho kizuri na kukisifia zaidi ili niweze kupata uzuri huo zaidi na zaidi. Najua kukazana kuangalia kilicho kibaya nitazidi kupata kibaya zaidi, ambacho hakitanisaidia.

Tukutane kwenye ukurasa wa 63 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; SIRI YA 21 YA MAFANIKIO; Tegemea Kilicho Bora.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment