Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, March 9, 2015

UKURASA WA 68; Furaha Ya Leo Ni Kikwazo Maisha Yako Yote…

Mara zote unajua ni kitu gani ambacho unatakiwa kufanya ili uwe na maisha bora, ili ufanikiwe.

Ila kufanya kitu au vitu hivyo ndio changamoto kubwa.

Unajua ili uwe na afya bora unahitaji kufanya mazoezi, kula vyakula vya afya na kuepuka vyakula vya haraka au vinavyoonekana ni vitamu. Lakini inapofika muda wa kufanya mazoezi unaona leo huwezi, utafanya kesho. Unapofika wakati wa kula, unafurahia kula chipsi leo, bila ya kujali baadae zitakuwa na madhara gani.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kutatua Changamoto Ya Usimamizi Kwenye Kilimo Na Jinsi Ya Kupata Mtaji.

Unajua ili ufikie mafanikio makubwa unahitaji kujijengea nidhamu nzuri ya fedha. Lakini kuna vitu vizuri vinavyokutamanisha utumie fedha sasa bila ya kujali maisha yako ya baadae.

Mara nyingi tumekuwa watu wa kutaka kupata raha sasa, kujisikia vizuri leo, bila ya kujali kama hali hii itaathiri maisha yetu ya baadae.

Unapoacha kufanya kazi leo na kusema utafanya kesho maana yake unajipa raha au kuridhika leo ila kesho utakuwa na kazi nyingi na muda mdogo.

Epuka hali hii ya kutaka kujiridhisha leo bila kujali madhara ya kesho. Chochote unachokwepa kufanya leo jua kabisa kitakuwa kikwazo kwako kufikia malengo uliyojiwekea. Usijidekeze, mambo sio rahisi kama unavyofikiria, unahitaji kujisukuma mpaka tone la mwisho.

SOMA; Mambo Matatu Ya Kuzingatia Katika Msamaha.

TAMKO LA LEO;

Sitakubali tena kujiridhisha leo na kuharibu kesho yangu. Sitakubali kupata raha leo na kuharibu mipango ya kufikia malengo yangu. Nitafanya kile nilichopanga kufanya na sitakubali kuchukuliwa na vishawishi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 69 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment