Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, February 11, 2015

UKURASA WA 42; Usitafute Sababu, Chukua Hatua…

Katika jambo moja ambalo tunaweza kukubaliana wote ni kwamba kwa chochote unachofanya ni lazima utakutana na changamoto.

Kama tulivyowahi kujifunza, kitu pekee ambacho tuna uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika. Unapanga vizuri jinsi biashara yako itakuletea faida, unaishia kupata hasara. Unapanga vizuri jinsi utafanya kilimo chako na upate mazao mazuri unaishia kukosa mazao kabisa.

Changamoto ni sehemu ya maisha yetu, hakuna njia ya kuzikwepa ila kuna njia ya kuzivuka na kuendelea mbele.

SOMA; Matatizo Yote Kwenye Maisha Yako Yanatokana Na Kitu Hiki.

Unapokutana na changamoto yoyote una mambo mawili ya kufanya;

Jambo la kwanza na ambalo ni rahisi kufanya ni kutafuta sababu kwa nini imetokea na jinsi gani wewe huhusiki na changamoto hii. Kama ni hasara basi utapata sababu kwamba uchumi sio mzuri, wateja hawanunui na kadhalika. Kama ni kilimo utasema hakukuwa na mvua, uliowapa kazi hawakufanya vizuri n.k. Baada ya sababu hizi kinachotokea ni wewe kukata tamaa, mwisho wa mchezo.

Jambo la pili unaloweza kufanya ambalo ni gumu na ndio linatofautisha wanaofanikiwa na wanaojaribu tu ni kuangalia ni wapi ulikosea. Baada ya kuona mchango wako kwenye changamoto hiyo unaamua kuchukua hatua na wakati huu ukiwa na funzo tayari kutoka kwenye changamoto uliyopitia.

TAMKO LA LEO;

Najua changamoto yoyote ninayopitia inaweza kunifanya niwe imara zaidi au inaweza kunipoteza kabisa. Nachagua kuwa imara kw akila changamoto ninayopitia. Sitotafuta sababu za kuniridhisha kwamba changamoto ninayopitia sikutengeneza mimi, bali nitajifunza kutokana na mchango wangu kwenye changamoto hiyo na baadae nitafanya kwa ubora zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 43 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; UKURASA WA 20; Geuza Changamoto Kuwa Fursa.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment