Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Showing posts with label SIRI 50 ZA MAFANIKIO. Show all posts
Showing posts with label SIRI 50 ZA MAFANIKIO. Show all posts

Friday, March 13, 2015

SIRI YA 50 YA MAFANIKIO; Kuwa Mtu Wa Vitendo. Fanya Vitendo Vingi.

Unacho kila unachohitaji ili kufikia mafanikio. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua hatua, kufanya vitendo. Fanya vitendo vingi sana. Hivyo ndivyo watu wenye mafanikio wanavyofanya. Wanapanga ni wapi wanataka kufika na wanaanza kuchukua hatua mara moja. Mbele ya safari wanajiendeleza ili kuwa bora zaidi.
Ndoto yako ni nini? Je upo tayari kuiendea thahabu?  Je upo tayari kuchukua hatua na kuyafanya maisha yako kuwa bora?
Kama ndio basi unasubiri nini?
Anza sasa kuchukua hatua, usisubiri uwe tayari...
JUST DO IT na mengine utaendelea kujifunza kadiri unavyokwenda.

  “You miss 100% of all the shots you don’t take.”  - Michael Jordan

SIRI YA 49 YA MAFANIKIO; Tengeneza Maana Nyingine Ya Kushindwa..

Kama unajua ndani ya nafsi yako kwamba umefanya kwa ubora wako wote hakuna kitu kinaitwa kushindwa. Hii ndio maana kuweka juhudi zako zote ni muhimu sana. Mara zote unashinda pale unapoweka juhudi zako zote.

“In great attempts it is glorious even to fail.”  - Wilfred Peterson

SIRI YA 48 YA MAFANIKIO; Mara Zote Tumia Uwezo Wako Wote...

Juhudi zako zote ndio zinahesabika. Kama utafanya kwa ubora wako wote, hakuna aibu. Iwe ni kwenye kazi yako au kwenye jamii, au kwenye maisha yako binafsi, mara zote fanya kwa uwezo wako wote.
Huwezi kujigakikishia kuwa bora zaidi ya wengine, ila unaweza kujihakikishia kuwa bora kwa uwezo wako mkubwa ulionao.
Mafanikio binafsi yanatokana na juhudi kubwa. Kama utafanya chini ya uwezo wako umejiangusha mwenyewe.

“Peace of mind comes from knowing you did your best.”  - John Wooden

Thursday, March 12, 2015

SIRI YA 47 YA MAFANIKIO; Jiandae Ili Kushinda.

Angalia lengho lako lakini wekeza muda mwingi kwenye kujiandaa kwa kile unachotakiwa kufanya ili kufikia lengo lako. Kushinda ni zao la maandalizi mazuri na juhudi.
Wekeza kwenye kujiandaa na kuweka juhudi na mafanikio yatakuja yenyewe.

“Failing to prepare is preparing to fail.”  - Unknown

Wednesday, March 11, 2015

SIRI YA 46 YA MAFANIKIO; Usiwe Na Wasiwasi Na Nafsi Yako.

Ni rahisi kuangalia nyuma na kuona sehemu ambayo ulikosea. Kama unaangalia nyuma ili kuona ni jinsi gani unaweza kuwa bora zaidi hapo sawa. Ila usipoteze muda wako kujiona kama huwezi. Majibu uliyopata zamani yanatokana na uzoefu wako wa zamani. Kama mambo hayatakwenda kama ulivyopanga tumia uzoefu wako wa sasa kuboresha zaidi.

“Self- confidence is the first requirement for great undertakings.”  - Samuel Johnson

SIRI YA 45 YA MAFANIKIO; Mbinu Muhimu Za Kufanikiwa.

1. Usimuogope mshindani wako. Mheshimu mshindani wako.
2. Jinsi unavyofanya kazi kwa juhudi zaidi ndivyo unavyozidi kuwa na bahati.
3. Jua vizuri kile unachokifanya.
4. Jijue wewe mwenyewe. Tumia ubora wako.
5. Kupambana na juhudi zitafidia makosa.
6. Kuwa mkweli kwako binafsi. Fuata moyo wako.

“I don’t know the key to success, but the key to failure  is trying to please everybody.”  - Bill Cosby

Tuesday, March 10, 2015

SIRI YA 44 YA MAFANIKIO; Uvumilivu Unalipa Sana. Angalia Maisha Ya Mtu Huyu Yalivyokuwa Ya Kukatisha Tamaa.

Akiwa na miaka 21 alishindwa kwenye biashara.
Akiwa na miaka 22 alishindwa kwenye uchaguzi wa uwakikishi.
Akiwa na miaka 23 alishindwa kwenye biashara ya pili.
Akiwa na miaka 25 mchumba wake alikufa.
Akiwa na miaka 26 alipata ugonjwa wa akili(kichaa)
Akiwa na miaka 28 alishindwa kwenye uchaguzi wa uwakilishi.
Akiwa na miaka 30 alishindwa uchaguzi mwingine.
Akiwa na miaka 33 alishindwa tena uchaguzi mwingine.
Akiwa na miaka 38 alishindwa tena uchaguzi mwingine wa uwakilishi.
Akiwa na miaka 45 alishindwa kwenye uchaguzi wa useneta.
Akiwa na miaka 46 alishindwa kwenye uchaguzi wa makamu wa raisi.
Akiwa na miaka 49 alishimdwa tena kwenye uchaguzi wa useneta.
Akiwa na miaka 50 alichaguliwa kuwa raisi wa marekani.
Maisha yake ya kushindwa yalimfanya awe bora zaidi na kuweza kupambana mpaka akafanikiwa kuwa raisi wa marekani na kuweza kuiongoza nchi hiyo kwenye vita vya kiraia.
Kama unapitia magumu jua kwamba unaandaliwa kwa ajili ya mambo makubwa zaidi.

“Character is forged whenever we struggle.” - Ruben Gonzalez

SIRI YA 43 YA MAFANIKIO; Anza Kufanya Maamuzi Mengi Zaidi.

Viongozi hufanya maamuzi - kila mara.
Wafuasi wanatoa mapendekezo.
Kutoa mapendekezo ni rahisi kwa sababu hayahitaji wewe kufanyia kazi na hakuna hofu ya kusindwa.
Kugpfanya maamuzi ni kugumu. Inahitaji ujasiri kwa sababu mara zote kunakuwa na changamoto.
Anza kufanya maamuzi zaidi. Anza kufanya matendo zaidi.
Jinsi unavyofanya zaidi ndivyo unavyojitengeneza kuwa kiongozi mzuri ja ndivyo utakavyofanikiwa zaidi kwenye maisha.

  “Great decision making comes from trusting and following  your intuition and your gut feelings.”  - Ruben Gonzalez

Sunday, March 8, 2015

SIRI YA 42 YA MAFANIKIO; Mtazamo Wako Utapima Mafanikio Yako.

Tafiti za watu waliofanikiwa zinaonesha kwamba mtazamo unachangia asilimian80 ya mafanikio na asilimia 20 ndio inacangiwa na vitu vingine kama juhudi na maarifa.
Mtazamo maana yake nini? Maana yake ni kufikiri kama mshindi. Kutegemea kushinda. Kuwa tayari kulipa gharama ya mafanikio. Kuamua ni lazima ufikie mafanikio. Kuamini unaweza kufanikiwa. Kuwa na matarajio chanya. Kujiamini na kuwa na misingi mizuri ya kazi.

  “What happens to a man is less significant than what happens within him.”  - Louis Mann

Friday, March 6, 2015

SIRI YA 41 YA MAFANIKIO; Shirikiana Na Watu Muhimu Kufikia Ndoto Zako.

Usikubali ukosefu wa ujuzi au rasilimali kukuzuia wewe kufikia ndoto zako. Kama kuna kitu hujui, au kuna kitu huna tafuta mtu kwenye kujua au mwenye nacho ambaye utaweza kushirikiana nae.
Tafuta watu wa kushirikiana nao ambao wana vitu muhimu ambavyo wewe huna. Na ushirikiano wenu utawawezesha wote kufikia mafanikio makubwa.

   “Teamwork makes the dream work.”  - Ruben Gonzalez

Thursday, March 5, 2015

SIRI YA 40 YA MAFANIKIO; Chagua Uwanja Sahihi Wa Mapambano

Utafanikiwa pale utqkapojua uwanja wa mapambano ambao ni bora kwako. Uwanja ambao unaweza kushinda na kufanikiwa.
Watu wengi wanacheza kwenye uwanja ambao sio bora kwao. Wanajikuta kwenye kazi wasizozipenda, mahusiano mabovu na hata miungano isiyo na faida kwao.
Kama wewe ni mmoja wa watu hawa basi unahitaji kujiweka huru. Unahitaji kuvunja minyonyoro inayokushikilia na kukurudisha nyuma na uanze kucheza kwenye uwanja wako.

  “The test of a vocation is the love for the drudgery it involves.”  - Logan Pearsall Smith

Wednesday, March 4, 2015

SIRI YA 39 YA MAFANIKIO; Zitumie Vizuri Fursa Zinazojitokeza.

Fursa ni kama mawimbi ya bahari. Inabidi uanze kulifuata wimbi la sivyo unalikosa. Washidi hawasiti, wanatumia kila fursa inayojitokeza.
Ukisita kutumia fursa unaikosa.

“There is a tide in the affairs of men, which, taken at the flood, leads on to fortune; omitted, all the voyage of their life is bound in shallows and in miseries… and we must take the current when it serves,  or lose our ventures.”  - William Shakespeare, Julius Caesar

Tuesday, March 3, 2015

SIRI YA 38 YA MAFANIKIO; Upende Mchakato Wote.

Mafanikio hayatatokea mara moja.
Kuna mchakato mrefu ambao utaupitia mpaka ufikie mafanikio.
Unahitaji kufanya kazi kwa juhudi ja maarifa, kuwa mbunifu na hata kuwa mvumilivu.
Kama utachkua hatua yoyote ya mchakato huu utashindwa kufikia mafanikio.
Furahia kila hatua unayopitia ya kukufikisha kwenye mafanikio. Maana kila kitu ni muhimu sana kwako.

“If you will trust the process, fall in love with the process, and consistently and persistently work the process, you will realize your dream.” - Ruben Gonzalez

Monday, March 2, 2015

SIRI YA 37 YA MAFANIKIO; Imani Nakupa Nguvu Ya Kuchukua Hatua

Imani ndio hatua ya kwanza ya kufikia mafanikio. Kuamini tu kitu kinawezekana ni jambonzuri sana.
Baada ya kuamini unaweza kuanza kufanya kazi na kujua utawezaje kufikia lengo lako. Kutamani tu hakuna nguvu yoyote. Ile hali ya NITAWEZAJE KUFANYA inatokana na imani.
Unapoamini unawakaribisha watu wengi wakusaidie kwa sababu wanaanza kuwa na imani na wewe. Imani yako inaamua ni vitu gani utafanikiwa kwenye maisha yako.

  “Man is literally what he thinks.”  - James Allen

SIRI YA 36 YA MAFANIKIO; Usitengeneze Sababu.

Watu waliofanikiwa hawatengenezi sababu. Wangeweza kufanya hivyo ila hawataki.
Sababu ni kisingizio kinachomsaidia mtu kufia uso wake pale ambapo hazalishi kile alichotarajia kuzalisha. Hakuna mtu anayetaka kusikia sababu zako. Wanataka kujua ni kipi umejipanga kufanya ili kuzalisha kile unachotarajiwa kuzalisha.

   “Excuses are a waste of time. Successful people don’t waste time.  They use their time trying to figure out ways to be more successful.”  - Ruben Gonzalez

Sunday, March 1, 2015

SIRI YA 35 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujijengea Kujiamini.

1 - Fikiria mawazo chanya tu.
2 – Yabadilishe mawazo hasi kwa mawazo chanya.
3 – Tembea haraka. Tembea kwa dhumuni.
4 – Simama katika hali ya kujiamini, kichwa kiwe juu, angalia mbele, mabega yawe nyuma na tumbo liwe ndani.
5 – Waangalie watu usoni na tabasamu.
6 – Jitambulishe kwa wengine. Usisubiri wao wajitambulishe kwako.
7 – Ongea kilichopo kwenye akili yako.

“You gain strength, courage and confidence every time  you look fear in the face.”  - Eleanor Roosevelt

Friday, February 27, 2015

SIRI YA 34 YA MAFANIKIO; Unakuwa Kile Unachofikiria.

Unapata kile unachofikiri unastahili kupata kwa sababu wengine wanakuona wewe kama unavyojiona mwenyewe. Kama unafikiria wewe ni wa chini, utafanya hivyo hivyo na watu watakuchukulia wewe ni wa chini.
Jinsi unavyofikiri kunaamua jinsi unavyotenda na jinsi unavyotenda kutaamua wengine wakuchukulieje. Jinsi unavyojiheshimu mwenyewe ndivyo na wengine watakavyokuheshimu.

  “Change your thoughts and you’ll change your world.”  - Dr. Norman Vincent Peale

Thursday, February 26, 2015

SIRI YA 33 YA MAFANIKIO; Kuwa Mtu Wa Vitendo.

1 – Lenga kile unachoweza kufanya sasa.
2 – Usisubiri mpaka mambo yote yawe sawa. Kufanya ni bora kuliko kusubiri kila kitu kiwe tayari.
3 – Mawazo tu yenyewe hayana thamani. Mawazo yanayofanyiwa kazi yana thamani kubwa sana.
4 – Kama utatenda sasa na kuzikabili hofu zako, hofu zitapotea.
5 – Usisubiri mpaka ujisikie kufanya kitu. Chukua hatua mara moja na utaanza kujisikia kuendelea kufanya.
6 – Usipoteze muda mwingi kujiandaa kufanya kitu, anza kufanya mara moja.

   “Anyone can do nothing.”  - Ruben Gonzalez

Wednesday, February 25, 2015

SIRI YA 32 YA MAFANIKIO; Zishinde Changamoto.

Watu waliokata tamaa na maisha yao wana kitu kimoja kinachofanana. Wote walikutana na changamoto ambayo iliwafanya waache kile wanachofanya na watakuwa tayari kukuambia ni jinsi gani hali waliyokutana nayo ilikuwa ngumu kwao. Mara zote wanaendelea kulisha hofu zao.
Watu waliofanikiwa wanatenda tofauti wakati wanapokutana na changamoto. Wanaamka, wanajifunza kwa kilichowaangusha , wanasahau kilichotokea na kuendelea kusonga mbele.

   “It’s not what happens to you. It’s how you handle it.”  - Ruben Gonzalez

SIRI YA 31 YA MAFANIKIO; Inuka Ushinde Mbio.

Maisha ni kama mbio ambapo kila siku unakimbia ili kufikia mafanikio.
Katika mbio hizi kuna kuchoka na hata kuanguka.
Haijalishi umeanguka mara ngapi, unahitaji kujikaza na kuendelea na mbio ili uweze kufikia ushindi.