Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, July 3, 2015

UKURASA WA 184; Ni Ruhusa Kwako Kubadili Mawazo.

Kwa mfano umeshakubaliana na mtu mtafanya kitu fulani halafu dakika za mwisho anakuambia nimebadili mawazo, sitafanya tena kama nilivyokuambia. Unajisikiaje? Unachukuliaje hali kama hiyo?
Labda ni biashara na umeshakubaliana na mteja ila baadae anakuambia nimebadili mawazo. Au ni kwenye ajira na umeshakubaliana kitu fulani na mwajiri wako, umeshajiandaa kabisa na anakuambia nimebadili mawazo, hutafanya tena hivyo. Au ni kwenye maisha yako ya kawaida, ulipanga muoane na mtu na dakika za mwisho anakuambia nimebadili mawazo? Au umeshaona na mtu na kati kati ya safari anakuambia nimebadili mawazo?
Najua kama wewe ndio umeambiwa hivi unaweza kujisikia vibaya sana. Unaweza kuona aliyebadili mawazo hafai na ameharibu maisha yako. Lakini ukweli ni kwamba yeye ametumia haki yake ya msingi, kuruhusu mawazo yake yamchagulie kile ambacho anaona ni bora kwake. Hakuna jinsi unaweza kuzuia hilo.
SOMA; Kabla Hujakubali Kila Unachoambiwa, Kumbuka Jambo Hili Moja Muhimu Sana.
Badala ya wewe kulalamika kwamba kwa nini hakukwambia mapema au kwa nini alikubali mwanzoni, furahi kwamba umejua mapema kabla hata hujapoteza muda mwingi. Shukuru kwamba umejua ni mtu wa aina gani na jifunze wakati mwingine kuangalia vitu muhimu kabla hujaingia kwenye makubaliano na mtu ambayo ni muhimu.
Jipe ruhusa ya kubadili mawazo, wape wengine ruhusa ya kubadili mawazo na usitake kuishi maisha ya kufungwa au kuwafunga wengine kwa sababu tu wanaogopa kubadili mawazo. Maisha yanapaswa kufurahiwa na sio kuishi kwa ajili ya kuwaridhisha wengine.
TAMKO LA LEO;
Najua nina ruhusa ya kubadili mawazo hata kama nilishakubaliana na mtu. Najua pia kwamba watu wana ruhusa ya kubadili mawazo yao hata kama walishaniahidi kitu. Naheshimu uhuru wangu na wa kila mtu na ni kwa uhuru huu ndio naweza kuishi maisha ninayoyafurahia na yenye faida kwa wengine pia.
Tukutane kwenye ukurasa wa 185 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment