Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, July 5, 2015

UKURASA WA 186; Kama Utashindwa Kufanya Chochote Utakachojifunza, Basi Fanya Hiki Kimoja Tu, Na Maisha Yako Yatagusa Wengine.

Nimekuwa nakushirikisha mambo mengi sana ambayo unahitaji kuyafanya ili kuboresha maisha yako. Mambo haya yanahitaji wewe ubadilike, uanze kufanya tofauti na ulivyozoea kufanya na sio kitu rahisi sana.
Kuacha kuangalia tv na kujisomea mambo yatakayokuweka mbele zaidiinahitaji kujitoa kweli.
Kuacha kukaa na jamaa zako kila jioni mkipata moja moto na moja baridi ili upate muda mwingi zaidi wa kuweka kwenye kazi au biashara yako sio kitu rahisi.
Kuacha kulalamika pale unapoona kabisa kwamba umeonewa au umeumizwa inahitaji nguvu ya ziada.
Kuacha usingizi na kuamka asubuhi na mapema sana ili uweze kujifunza na kuipangilia siku yako sio kitu rahisi kama unavyoweza kufikiria.
Tuseme labda wewe umeona kwamba mambo haya yote huwezi, kwa sababu tu una uvivu uliopitiliza au kwa kifupi basi tu hutaki kujihangaisha. Leo nataka nikuambie kitu kimoja muhimu sana cha kufanya.
SOMA; Kauli KUMI Za Marcus Aurelius Zitakazokufanya Uyaone Maisha Kwa Utofauti.
Tafadhali sana hata kama una uvivu kiasi gani, jitahidi ufanye kitu hiki kimoja na maisha yako yatagusa wengine kwa kiasi kikubwa sana.
Kitu chenyewe ni kuishi maisha mazuri kwako na kwa wanaokuzunguka. Kuwa mtu mwema, usimwibie mtu, usisengenye mtu, usijihusishe na majungu. Saidia wengine kadiri ya uwezo wako. Yaani kuwa tu mtu mwema na wengine waone wewe ni mfano wa kuigwa. Na hata kama kuna mtu amekosa tumaini kwa kuyaona maisha yako atapata tumaini kwamba dunia bado ina watu wema waliomo.
Hili ni jambo muhimu kwetu sote kufanya hata kama unafanya hayo mengine yote unayojifunza kila siku.
TAMKO LA LEO;
Nitahakikisha naishi maisha ambayo yatakuwa mfano mzuri kwa watu wengine. Nitajiepusha na mambo ambayo sio mazuri kwangu na kwa wale wanaonizunguka. Sitoiba wala kumdhulumu mtu, sitosengenya wala kushiriki majungu na nitasaidia wengine kadiri ya uwezo wangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment