Bila chakula kuchanganyika na mate huwezi kupata ladha yake.
Mate yanalainisha chakula na kukisambaza kwenye sehemu za ulimi zinazopima ladha.
Lisha Ubongo Wako, Badili Fikra Zako, Boresha Maisha yako.
We'll not spam mate! We promise.
Bila chakula kuchanganyika na mate huwezi kupata ladha yake.
Mate yanalainisha chakula na kukisambaza kwenye sehemu za ulimi zinazopima ladha.
Binadamu huzaliwa na mifupa 300, lakini mpaka anapokuwa mtu mzima anakuwa amebaki na mifupa 206 tu.
Kinachosababisha mifupa ipungue ni kwamba baadhi ya mifupa huungana na kutengeneza mfupa mmoja.
Pia ndani ya sikio lako kuna mifupa midogo sana kama ulikuwa hujui pia.
Baadhi ya wanyama jamii ya Mamba humeza mawe na kukaa nayo tumboni kwa muda mrefu. Mawe haya huitwa gasrolith.
Mawe haya humsaidia mamba mambo yafuatayo;
1. Humsaidia aweze kuwa na uzito utakaowafanya wazame kina kirefu zaidi kwenye maji.
2. Humsaidia kusaga chakula tumboni.
3. Hufanya tumbo liwe na uzito na kujisikia ameshiba hata kama hajala.
Almasi ndio kitu kigumu kuliko vitu vyote vinavyojulikana na binadamu.
Ndio inayotumika katika ncha za vifaa vya uchimbaji ja upasuaji miamba.
1. Ni nchi kamili yenye mamlaka kamili. Ina mfumo wake wa posta, fedha na ulinzi.
2. Iko ndani ya mji wa Roma kwenye nchi ya Itali,
3. Utawala wa Vatican ni wa kidini na mkuu wa nchi ni papa.
4. Vatican imezungukwa na ukuta.
5. Ni nchi yenye watu wachache zaidi duniani. Ina wananchi wapatao 800, wengi wao ni viongozi wa kidini.
6. Asilimia kubwa ya wananchi wa Vatican wanaishi nje ya nchi, kama mabalozi na wawakilishi.
7. Kuna jeshi maalumu la ulinzi linaloitwa Swiss guard, wanajeshi wake wana uwezo mkubwa sana.
8. Ni nchi yenye eneo dogo zaidi, takribani ukubwa wa hekari 100.
9. Vatican haina mfumo wa kodi.
10. Kuna njia ya siri ya papa kutoroka ikiwa kuna tatizo la usalama.
Wakati wa utawala wa Nazi chini ya Adolf Hitler, ujerumani ilianzisha sera ya kuua watu wote ambao walionekana ni dhaifu.
Katika sera hii inasemekana watu zaidi ya laki mbili waliuawa kati ya mwaka 1940 mpaka mwaka 1945.
Waliouawa walikuwa ni wagonjwa wasiopona na walemavu.
Madaktari walitumika katika zoezi hili.
Tukio hili pia limewahi kutokea nchini Uganda ambapo mtawala wa kipindi hiko Idd Amin alishutumiwa kukusanya walemavu na kwenda kuwatupa kwenye mto.
Libya ndio nchi ya kwanza Africa Kupata uhuru, na ilipata uhuru wake mwaka 1951, kutoka kwa Witali.
Misri ilipata uhuru wake mwaka 1952 kutoka kwa waingereza.
Na Ghana ndio nchi ya kwanza kusini mwa jangwa la sahara kupata uhuru wake. Ilipata uhuru mwaka 1957 kutoka kwa waingereza.
Je unajua nchi ya Africa ambayo haikuwahi kutawaliwa kipindi cha ukoloni?
Na je unajua nchi ya africa ambayo ilikuwa ya mwisho kupata uhuru?
Kama unajua weka maoni yako hapo chini, kama hujui weka maoni kwamba unataka kujuzwa.
TUPO PAMOJA.
Saturn ndio sayari kubwa inayoweza kuelea kwenye maji. Yaani density yake ni ndogo kuliko ya maji.
Kuna bacteria wengi wanaoishi kwenye kinywa chako zaidi ya idadi wa watu wanaoishi duniani.
Bacteria pia wapo kwenye ngozi yako, utumbo mpana na hata sehemu ya uke.
Kwa bahati nzuri bacteria hawa hawana madhara na wapo hapo kukukinga na bacteria wabaya.
Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA
Sasa unajua kwamba sio bacteria wote wanaoishi kwenye mwili wako ni hatari.
1. Mtu mzima anapumua mara 23,000 kwa siku.
2. Kazi kubwa ya kupumua sio kupata oxygen, bali kuondoa kabon dayoksaidi.
3. Kupumua kwa kutumia mdomo ni hatari kwa afya yako.
4. Unavyopumua kwa kasi ndivyo inavyozidisha njaa na acid kwenye mwili wako.
5. Unatakiwa kufanya mazoezi kwa kiwango ambacho utaweza kupumua ukiwa umefunga mdomo.
6. Pua ina ngazi nne za kuchuja hewa inayoingia, ukipumua kwa mdogo unenda moja kwa moja kwenye ngazi ya nne.
7. Kama mapafu yako yangetandazwa yanafiki ukubwa wa uwanja wa tennis.
8. Kupumua kunaendeshwa na mfumo wa fahamu usio wa hiari(involuntary).
9. Ukijizuia kupumua unaongeza kabon dayoksaidi kwenye mwili.
10. Ukijizuia kupumua unatibu kwi kwi.
Sasa umeshajua mambo muhimu kuhusu kupumua, pumua vyema.
Nakutakia kila la kheri.
Copyright © 2013 Makirita Amani.