Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, January 31, 2015

Huu Ni Mwaka Wa Kuacha Unafiki...

Umefika wakati wa kuacha unafiki..
Maana kuendelea na unafiki huu hakuwezi kukusaidia tena.
Swali la msingi; wakati unazaliwa au unakua ni nani alikuambia maisha yatakuwa rahisi? Kwamba utapata kila kitu kwa urahisi? Kwamba kutakuwa na njia za mkato za wewe kupata unachotaka?
Hakuna popote umewahi kuambiwa hivi.
Lakini kwa unafiki umeamua kulalamikia mambo hayo.
Kwamba maisha ni magumu, kwamba hupati njia ya mkato ya kufikia mafanikio.
Achana na unafiki huu,
Maisha ni magumu ndio, lakini ugumu wa maisha ndio unayafanya yawe mazuri kuishi.
Hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio, na kutokuwepo kwa njia hii ndio kunafanya safari ya kuelekea kwenye mafanikio kuwa nzuri.
Furahia kila hatua ya maisha yako.
Jifunze kutokana na changamoto unazopitia.
Acha kulalamika.

UKURASA WA 31; Umetoka Wapi, Upo Wapi Na Unaelekea Wapi?

Ili kufikia mafanikio makubw akwenye maisha yako ni lazima uwe na njia ya kuweza kujipima. Ni lazima uweze kujipima kama kweli upo kwenye njia sahihi ya kukufikisha kwenye mafanikio.

Ni muhimu sana kujua unakotoka, hii itakufanya ujue ni kazi kiasi gani unahitaji kufanya ili kufika unakotaka.

Ni muhimu pia kujua ulipo, hii itakusaidia kuweza kupanga na kutekeleza mipango ya kukutoa hapo ulipo na kukufikiahsa unakotaka.

Ni muhimu sana kujua kule unakokwenda ili malengo na mipango utakayoweka iweze kukufikisha huko.

Pamoja na kujua unakotoka, ulipo na unapokwenda ni lazima uwe na njia ya kujipima. Katika wakati wowote ule ni lazima uweze kujifanyia tathmini kama kweli uko kwenye njia sahihi na itakayokufikisha kwenye malengo yako.

SOMA; Njia KUMI Za Kuboresha Maisha Yako Ya Kibiashara.

Kama leo ni siku ya 31 ambayo ni siku ya mwisho ya mwezi wa kwanza. Tumia siku ya leo kufanya tathmini ya mwezi mzima. Ni vitu gani ambavyo umefanikiwa kuvifanya, ni vitu gani ambavyo umeshindwa kufanya na ni changamoto gani umekutana nazo.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba ni muhimu sana kupima kile ninachofanya na kule ninakokwenda. Kitu chochote ambacho hakiwezi kupimwa hakiwezi kufanyika kwa ukamilifu. Kila mara nitakuwa najitathmini ili kujua kama nipo kwenye njia sahihi na nafanya jambo sahihi la kunifikisha kwenye mafanikio. Leo nitafanya tathmini ya siku 30 za mwezi huu wa kwanz ana kuweka au kubadili baadhi ya mipango ambayo haiendi vizuri.

Tukutane kwenye ukurasa wa 32 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

ADUI NAMBA MOJA WA MAFANIKIO YAKO...

NENO LA LEO; Njaa Ndio Itakupatia Unachotaka…

“Wanting something is not enough. You must hunger for it. Your motivation must be absolutely compelling in order to overcome the obstacles that will invariably come your way.” Les Brown

Kutaka kitu haitoshi, ni lazima uwe na njaa ya kukipaya. Hamasa yako ni lazima iwe kubwa sana ili kushinda vikwazo vitakavyokuja kwenye njia yako.

Unahitaji kuwa na njaa kubwa sana ya kupata kile unachotaka ili uweze kukipata. Hii ni kwa sababu lazima utakutana na vikwazo kwa chochote utakachotaka kufanya. Kama utakuwa unataka tu kawaida, ni rahisi kukata tamaa pale unapokutana na vikwazo.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Hii ndio faida ya kushindwa.

Friday, January 30, 2015

Je Upo Tayari Kupata Unachotaka? Siri Ni Hii Moja…

Unataka nini kwenye maisha yako?

Maana kama hujui unachotaka tayari umeshakikosa.

Je upo tayari kupata hiko unachotaka?

Ni nini kinakuzuia mpaka sasa hujakipata?

Haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza. Maana kuna kitu ambacho kimekufanya mpaka sasa hujapata unachotaka na kushindwa kujua kitu hiko kitaendelea kukuzuia.

Jua kikwazo ni nini na anza kukishughulikia.

Anza na vikwazo hivi;

Kwa watanzania waliowengi, vikwazo vinafanana na baadhi ya vikwazo hivyo ni;

1. Kutokujiamini.

2. Hofu

3. Kulalamika

4. Kutegemea kuna mtu atakuja kukutoa hapo ulipo.

5. Matumizi mabaya ya hela.

6. Uvivu, kutokuwa na ubunifu. Kuiga

7. Kukosa uvumilivu na kukata tamaa mapema.

8. Kutafuta njia ya mkato

9. Kukosa uaminifu

10. Kupanga malengo na mipango ila kushindwa kuchukua hatua.

Anza kufanyia kazi mambo hayo kumi na utaona ilivyo rahisi kupata chochote unachotaka.

Kauli KUMI Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Robert Mugabe.

Robert Mugabe (kuzaliwa 21 February 1924) ni mwanamapinduzi na raisi wa Zimbabwe. Robert Mugabe aliweza kupambana na kuondoa walowezi ambao walikuwa wanashikilia sehemu kubwa ya ardhi ya zimbabwe. Ni kiongozi shujaa sana ambaye ameweza kushindana na vikwazo vya mataifa makubwa.

Leo tutapata kauli kumi kutoka kwake ambazo zitatuhamasisha na kutufanya tuchukue hatua kwenye maisha yetu.

1. There are things one must do for oneself.

Kuna vitu ambavyo mtu anahitaji kufanya kwa ajili yake mwenyewe.

2. We of Africa protest that, in this day and age, we should continue to be treated as lesser human beings than other races.

Sisi waafrika tunakataa kwamba, mpaka sasa tunaendelea kuchukuliwa kama watu wa hali ya chini ukilinganisha na watu wengine.

SOMA; Dalili Kumi Kwamba Tayari Wewe Ni Kiongozi.

3. We don't mind having sanctions banning us from Europe. We are not Europeans.
Hatujali kama ulaya wanatuwekea vikwazo, sisi sio wazungu.

4. Countries such as the U.S. and Britain have taken it upon themselves to decide for us in the developing world, even to interfere in our domestic affairs and to bring about what they call regime change.
Nchi kama marekani na uingereza wamechukua nafasi ya kutuamulia sisi nchi zinazoendelea, wanadiriki hata kuingilia mambo yetu ya ndani kwa kile wanachodai ni mabadiliko.

5. It may be necessary to use methods other than constitutional ones.
Kuna wakati inakuwa muhimu kutumia njia nyingine tofauti na za kikatiba.

6. Our party must continue to strike fear in the heart of the white man, our real enemy!
Chama chetu lazima kiendelee kuingiza hofu kwenye mioyo ya wazungu, ambao ndio maadui zetu.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

7. The white man is not indigenous to Africa. Africa is for Africans. Zimbabwe is for Zimbabweans.
Watu weupe sio wazawa wa Africa, Africa ni ya waafrika, Zimbabwe ni ya wazimbabwe.

8. The only white man you can trust is a dead white man.

Mtu mweupe pekee unayeweza kumwamini ni yule aliyekufa.

9. We are no longer going to ask for the land, but we are going to take it without negotiating.

Hatutaendelea tena kuomba ardhi, tunakwenda kuichukua bila ya kukubaliana.

10. If the choice were made, one for us to lose our sovereignty and become a member of the Commonwealth or remain with our sovereignty and lose the membership of the Commonwealth, I would say let the Commonwealth go.

Ni maamuzi tumefanya, kama ni kupoteza utaifa wetu ili kuwa wanachama wa jumuia ya madola au kubaki na utaifa wetu na kupoteza uanachama wa jumuia ya madola, tuko tayari kuacha uanachama wa jumuia ya madola.

Tumia kauli hizi kufikiri zaidi na kuhamsika kuchukua hatua ya kuboresha maisha yako na ya wale wanaokuzunguka.

SOMA;  Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.

Hakuna Kitu Chenye Maana...

Hakuna kitu chenye maana duniani,
Ila sisi wenyewe ndio tunavipa vitu maana.
Ukiweza kulijua hili, utajipunguzia matatizo mengi sana.
Kwa mfano kama unaona dhahabu ina maana, kuliko shaba, kumbuka vyote hivi ni madini ambayo yanapatikana kwenye ardhi. Tumeweka maana kubwa kwenye dhahabu kwa sababu haipatikani kirahisi kama shaba.
Kama nyama choma ni chakula cha maana, kumbuka huyu ni mnyama ambaye ameuawa na kuchomwa, hiyo maana nyingine tumeweka wenyewe.
Kama unaona pombe na mivinyo ya bei kali ni vitu vya maana, kumbuka haya ni matunda yaliyochachishwa, lakini sisi tumevipa maana.
Kitu chochote ambacho kina maana au kina thamani kubwa, hakijajipa thamani hiyo chenyewe.
Thamani hiyo tumevipa sisi wenyewe, hivyo usikubali kuteseka kwa sababu unaona huna vitu hivyo.
Chagua ni vitu gani cya maana kwako na vifanyie kazi.

UKURASA WA 30; Nenda Hatua Ya Ziada…

Mafanikio yana upendeleo mmoja, yanaenda kwa watu ambao wanafanya mambo kwa ubora wa hali ya juu sana.

Hawa ni watu wameamua kwenda hatua ya ziada kwenye jambo lolote wanalofanya. Hawakubali tu kufanya kama kila mtu anavyofanya. Watu hawa wanajua unapokwenda hatua ya ziada unajijengea nafasi kubwa ya kufikia mafanikio makubwa.

SOMA; Kuwa Kawaida Ni Kupoteza Muda Wako Na Siri Moja Ya Mafanikio Mwaka 2015

Fanya zaidi ya unavyolipwa, kama umeajiriwa timiza majukumu yako na nenda hatua ya ziada. Fanya mambo mazuri na bora ambayo wengine hawafanyi.

Kama upo kwenye biashara, fanya zaidi ya mteja anavyotegemea. Nenda mbali zaidi, mshangaze mteja na aone huduma aliyoipata hawezi kuipata sehemu nyingine yoyote. Kwa hali hii utatengeneza wateja wengi sana.

Mafanikio yote yapo kwenye hatua ya ziada. Kama ilivyo kwenye kupanda ngazi au mlima. Chini kunakuwa na watu wengi na hivyo kunakuwa na kelele nyingi. Ila unavyozidi kwenda juu unakuta watu wachache na hewa ni nzuri sana.

SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba ili kufikia mafanikio nahitaji kwenda hatua ya ziada, nahitaji kufanya tofauti na wengine wanavyofanya na kufanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Kazi yoyote nitakayoifanya, biashara yoyote nitakayoifanya na hata maisha yangu kwa ujumla nitafanya kwa ubora wa hali ya juu na kwa upekee. Nitafanya zaidi ya ninavyotegemewa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 31 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Maisha Yanapokosa Maana…

“Without faith, hope and trust, there is no promise for the future, and without a promising future, life has no direction, no meaning and no justification.” Adlin Sinclair

Bila ya imani, matumaini na uaminifu, hakuna ahadi ya baadae, na kama hakuna ahadi ya baadae, maisha hayana muelekeo, hayana maana na hayana uhalali.

Chagua maisha unayotaka kuishi wewe kwa kuw ana imani na matumaini kwamba unaweza kuyafanya bora kama unavyotaka.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Mambo KUMI Ya Kufanya Ili Usiishi Maisha Ya Majuto.

Thursday, January 29, 2015

Nafasi Ya Wewe Kuwa Bora Kila Siku… NA ZAWADI YA TSH 365,000/=

Kama mpaka sasa huna utaratibu wa kujifunza kila siku, tayari upo nyuma sana katika kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako.

Kujifunza kila siku ni hitaji la chini sana la wewe kuweza kufikia mafanikio. Na tunaposema kujifunza kila siku ni kila siku kweli, jumatatu mpaka jumapili na kurudia tena na tena na tena.

Pamoja na umuhimu wa kujifunza kila siku, bado tunaishi kwenye jamii ambayo haitupi nafasi kubwa ya kujifunza. Hii ni kutokana na kuzungukwa na mazingira yenye changamoto nyingi zinazozuia kujifunza kila siku.

Kutokana na changamoto hizi ndio kulikonisukuma kutumia muda wangu kukupatia wewe nafasi ya kujifunza zaidi. Kupitia blog ya MAKIRITA AMANI utaweza kupata nafasi ya kujifunza kila siku, jumatatu mpaka jumapili.

Kila siku utaianza siku yako kwa neno la siku, hili ni neno ambalo litakupa hamasa ya kuweza kuifanya siku yako kuwa bora zaidi. Na pia kila siku kwa mwaka huu 2015 utapata ukurasa mmoja katika safu ya kurasa 365 za mwaka 2015. Kama bado hii haitoshi, unapata nafasi ya kupata kauli za kuhamasisha kutoka kwa viongozi na watu mashuhuri ambao wamefanikiwa sana. Na pia utaweza kupata hadithi za mafunzo ambapo utawez akujifunz akupitia visa mbalimbali.

Pamoja na haya yote utakuwa ukipata makala zenye fikra za kukuchokoza. Hizi ni zile ambazo zinaniingia kwenye fikra zangu kutokana na mawazo mbalimbali yanayonifikia katika kutafuta njia za kufanya maisha yangu na ya wewe msomaji kuwa bora zaidi kila siku.

Kwa kifupi wewe kutembelea blog hii ni sawa na kuwa na mimi pembeni yako, kwani utapata kitu kizuri kutoaka kwangu pale unapokihitaji.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za mbalimbali za kukufundisha na kukuhamasisha kila siku bonyeza hapa na uweke email. Kila siku kwenye email yako utapata mambo haya moja kw amoja.

Siku yako itakuwa bora sana kwa kuwa karibu na blog hii nzuri kwako.

Kama ningekuwa natoza wasomaji fedha kulingana na elimu ninayoitoa hapa, kila msomaji angetakiw akulipa tsh elfu moja kila siku. Hivyo kwa mwaka ungetakiw akulipa tsh 365,000/= ili kupata elimu hii muhimu sana kwako. Lakini sijataka wewe uingie gharama yoyote, gharama yako ni wewe kufungua blog, kusoma makala na kufanyia kazi yale unayojifunza.

Ombi moja muhimu sana kwako ni wewe kuwaalika watu wengi zaidi kusoma blog hii. Haina gharama yoyote na wala haitakuja kuw ana gharama yoyote. Tafadhali tuma makala hii kwenye email za watu watano, itume kama ilivyo halafu nikopy kwenye email hiyo utakayotuma, tumia email makirita@kisimachamaarifa.co.tz kama hujui jinsi ya kukopi, wakati unaweka email ya unayemtumia chini yake kuna cc, hapo weka email yangu. Na mimi nitakupa zawadi nzuri sana ya kitabu cha mabadiliko ambacho bado nakiandika.

Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya kuboresha maisha yako.

TUPO PAMOJA SANA.

 

#HADITHI_FUNZO; Jinsi Ya Kuondokana Na Mzimu.

Bwana mmoja alikuwa na mke wake ambaye walipendana sana. Ilitokea yule mwanamke akawa anaumwa sana na asingeweza kupona. Wakati anakaribia kukata roho alimwambia mume wake nakupenda sana, tafadhali niahidi kwamba hata kama nikifa hutampenda mwanamke mwingine. Na kama ukivunja ahadi hiyo mzimu wangu utakujia na utakutesa sana.

SOMA; Sehemu Tano Unazoweza Kupata Mtaji Wa Kuanzia Biashara.

Mume wake alikubaliana nae na akaweka ahadi hiyo. Muda ulipita baada ya mwanamke yule kufa na mwanaume yule aliepuka kuwa na mwanamke mwingine. Baadae ilitokea akakutana na mwanamke ambaye walipendana sana na waliamua kuoana. Wakati wanakaribia kufungua ndoa mzimu wa mwanamke yule ulianza kumtokea yule mwanaume kila siku usiku. Mzimu ule ulimlalamikia kwa kutokutunza ahadi na kila siku usiku ulikuwa ukimtokea na kumwambia kila kitu ambacho mwanaume yule aliongea na mke wake mtarajiwa siku hiyo.

Hali hii ilimchosha yule mwanaume na akaamua kuomba ushauri kutoka kwa mzee mwenye busara. Mzee yule alimwambia inaonekana mzimu huu una akili sana. Mwanaume yule alimjibu ndio, maana unaweza kuniambia kila kitu kinachoendelea. yule mzee alimwambia nitakupa dawa moja ambayo utaitumia mzimu huo ukija.

SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Kufikia MAFANIKIO MAKUBWA.

Usiku uliofuata mzimu ule ulikuja tena, yule mwanaume aliuambia, wewe ni mzimu ambao una akili sana, na unajua siwezi kukuficha chochote, kama utaweza kunijibu swali hili moja, nitaahirisha ndoa yangu na sitaoa tena.  Mzimu ukamjibu uliza swali lako. Yule bwana aliingiza mkono wake kwenye mfuko na kuchukua maharage na kufungua mkono, kisha akauuliza mzimu ule, niambie ni maharage mangapi yako kwenye mkono wangu. Kwanzia pale mzimu ule ulipotea na haukurudi tena.

Tunajifunza nini kwenye hadithi hii?

Mzimu ni kitu ambacho tunajitengenezea kwenye akili zetu, hauwezi kujua kitu ambacho hatukijui. Kama unafikiria wewe umelogwa, umechezewa, una kisirani, ni wa kushindwa hayo yote umejenga mwenyewe kwenye kichwa chako. Ondokana na mawazo hayo na utaweza kufanya chochote unachotaka kwenye maisha yako.

Nakutakia kila la kheri.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

SOMA; Mambo Matano(5) Ambayo Ni Marufuku Kufanya Kwenye Eneo La Kazi.

KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

Huwa tuna utaratibu wa kupunguza ukali wa maneno, kwa kiswahili tunaita tafsida.

Yaani badala ya kusema mtu amezaa tunasema amejifungua, japokuwa yote ni yale yale tu, ila kujifungua linapunguza ukali wa uhalisia wenyewe.

Maneno kama kujisaidia, kufanya tendo la ndoa na mengine mengi ni maneno mazuri yanayotumika badala ya maneno halisi ya vitendo hivi. Uzuri wa maneno haya ni kwamba yanapotumika kila mtu anajua maana ni ile ambayo unafichwa.

SOMA; Ushauri Kwa Wajasiriamali Kutoka Kwa Mwanzilishi Wa Facebook.

Sasa kuna neno moja ambalo lina tafsida yake, ila watu huwa wahaielewi kabisa hii tafsida. Neno hilo ni KAWAIDA.

KAWAIDA ni neno ambalo linatumika kuficha ukweli halisi ambao ni HOVYO.

Ukisema unafanya kazi kawaida maana yake unafanya HOVYO, kwa kiwango cha chini sana ambacho hakuna anayeweza kuvutiwa.

Ukisema wewe ni mfanya biashara wa kawaida maana yake wewe ni mfanyabiashara wa HOVYO ambae hujui unakoelekea na unafuata tu upepo.

SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Kinachokurudisha Nyuma.

Usikubali kabisa kuwa wa kawaida, namaanisha kuwa hovyo.

Chochote unachofanya, kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana ili yeyote atakayeona avutiwe, ashawishike kujua zaidi na hapa ndio thamani yako inaongezeka. Hata kama unafanya kazi ambayo unaona haiwezi kufanywa kwa kipekee wewe ibadili na ifanye kwa kiwango cha hali ya juu sana. Utaona mabadiliko makubw akwenye kazi yako na hata maisha yako kwa ujumla.

Ukikubwali kuwa wa kawaida, yaani kuwa HOVYO, umeamua kutopata mafanikio ambayo yanakusubiri. kuwa bora, kuwa tofauti, kuwa wa kipekee na utaona mafanikio yakikufuata wenyewe.

Kuanzia leo jiwekee marufuku kuwa HOVYO.

SOMA; Mambo 10 Unayotakiwa Kujua Kuhusu Uwekezaji.

UKURASA WA 29; Kitu Pekee Unachoweza Kuwa Na Uhakika Nacho…

Kitu pekee unachoweza kuwa na uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika.

Hujanielewa? Tumia mifano hii;

Unapanga kwamba utakwenda kwenye mkutano, umeambiwa mkutano utaanza saa sita na kumalizika saa nane. Wewe unapanga baada ya mkutano wa saa nane, saa nane na nusu utakutana na mtu muhimu sana. Unapanga mambo yako vizuri kabisa na unakuwa na uhakika utamaliza mkutano wako saa nane na saa nane na nusu utakutana na mtu muhimu.

Unakuja kupata changamoto pale ambapo mkutano uliotakiwa kuisha saa nane unaendelea mpaka saa nane na nusu na hauna dalili z akumalizika. Huku mtu muhimu uliyepanga kuonana naye akikutafuta kwamba tayari amefika na anakusubiri. Mkutano huwezi kuondoka kabla haujaisha na mtu muhimu anakusubiri. Unafanya nini?

Hapa ndipo mtu unaanza kupata msongo wa mawazo, kukasirika, na hatimaye kukosa vyote viwili.

Hakuna mtu ambaye ana uhakika na jambo lolote. Unapanga utawahi mahali kwa mwendo wa nusu saa, unafika njiani unakutana na ajali na magari hayawezi kupita. Unapanga utawahi ndege kwamuda uliopangwa ili uweze kuwahi kitu muhimu, dakika za mwisho unaambiwa safari imeahirishwa.

Hakuna mwenye uhakika, na hili pekee ndio tuna uhakika nalo.

SOMA; Sababu TATU Kwa Nini Watu Wengi Wanashinda Kufikia Mafanikio.

Unafanya nini sasa? Je unakubali kila kitu kiende hovyo kwa sababu huna uhakika?

Hapana, huwezi kuacha kila kitu kiende hovyo kwa sababu huna uhakika. Badala yake unahitaji kujiandaa mapema kabla ya kitu. Na pia jipe nafasi ya kuweza kurekebisha chochote kitakachokea katikati.

Kwenye mfano wa mkutano hapo juu, unaweza kutenga saa moja ya ziada ili usipange ratiba ambazo zitaingiliana.

TAMKO LA LEO;

Kitu pekee ambacho nina uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika. Kuna mambo mengi sana yatakayotokea saa moja ijayo ambayo sikutarajia kama yangetokea. Kila mara nitajiandaa mapema ili kuepuka mambo yangu kuvurugika kutokana na kutokuwa na uhakika.

Tukutane kwenye ukurasa wa 30 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Hiki Ndio Kitakachotokea Miaka 100 Ijayo..

NENO LA LEO; Chakula Cha Akili…

“Motivation is like food for the brain. You cannot get enough in one sitting. It needs continual and regular top ups.” Peter Davies

Hamasa ni kama chakula cha akili. Huwezi kupata ya kutosha mara moja. Unahitaji kuendelea kuongeza kila siku.

Hakuna siku utasema kwamba sasa nimehamasika kiasi cha kutosha na hivyo sihitaji tena hamasa. Hapo utakuwa unapotea.

Hamasa ni kitu ambacho unatakiwa kukipata kila siku. Na kwa bahati nzuri wewe unayo nafasi ya kupata hamasa kila siku kwa makala fupi unazosoma hapa kwenye blog hii MAKIRITA AMANI.

Pia unawez akuhamasika na makala nzuri kwenye blog zifuatazo;

AMKA MTANZANIA kuhusu maisha, biashara, ujasiriamali,, mafanikio.

JIONGEZE UFAHAMU kuhusu mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kuwa bora zaidi kila siku.

VORACIOUS READERS ambapo unapata nafasi ya kusoma vitabu viwili kila wiki.

KISIMA CHA MAARIFA hapa kama unataka mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya ndio nyumbani kwako.

Hakikisha unaweka email yako hapo juu na kusubscribe ili uendelee kupata makala za kukufundisha na kukuhamasisha kila siku.

Nakutakia siku njema.

Wednesday, January 28, 2015

Kauli Kumi Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Abraham Lincoln

Abraham Lincoln (February 12, 1809 – April 15, 1865) alikuwa raisi wa 15 wa marekani. alianza kipindi chake cha uraisi March 1861 mpaka alipouawa April 1865. Lincoln aliongoza marekani katika kipindi cha vita ambayo ilikuwa changamoto kubwa kwake. Katika vita hii aliweza kuimarisha muungano wa majimbo ya marekani, kutokomeza utumwa na kuimarisha uchumu.

Leo utajifunza kauli kumi kutoka kwake ambazo zitakuhamasisha wewe kuchukua hatua na kuboresha zaidi maisha yako na ya wale ambao wanakuzunguka.

1. In the end, it's not the years in your life that count. It's the life in your years.
Mwishoni sio miaka ya maisha yetu itakayohesabika bali maisha ya miaka yetu ndio itakayohesabika.

SOMA; Viongozi 100 Walioibadili Dunia.

2. Most folks are as happy as they make up their minds to be.
Watu wengi wanafuraha kama walivyozifanya akili zao kuwa hivyo.

3. Nearly all men can stand adversity, but if you want to test a man's character, give him power.
Karibu kila mtu anaweza kuvumilia matatizo, ila kama unataka kupima tabia ya mtu, mpe nguvu(uongozi)

4. Always bear in mind that your own resolution to succeed is more important than any other.
Kila mara kumbuka kwamba uamuzi wako wa kufanikiwa ni muhimu kuliko kitu kingine chochote.

abraham-lincoln-quote-5

SOMA; Watu Watatu(3) Waliofukuzwa Kwenye Kampuni Walizoanzisha Wenyewe.

5. The best thing about the future is that it comes one day at a time.
Uzuri wa baadae ni kwamba inakuja siku baada ya siku.

6. Give me six hours to chop down a tree and I will spend the first four sharpening the axe.
Nipe masaa sita ya kukata mti na nitatumia masaa manne ya mwanzo kunoa shoka langu.

7. Whatever you are, be a good one.
Chochote utakachoamua kuwa, kuwa bora.

SOMA; Mambo 10 Usiyojua Kuhusu Vatican.

8. No man is good enough to govern another man without the other's consent.
Hakuna mtu mwenye uwezo wa kumtawala mwingine bila ya uamuzi wake.

9. Better to remain silent and be thought a fool than to speak out and remove all doubt.
Ni bora kukaa kimya na kufikiriwa kwamba ni mpumbavu, kuliko kuongea na kudhihirisha kwamba kweli ni mpumbavu.

10. Things may come to those who wait, but only the things left by those who hustle.
Vitu vinaweza kuja kwa kwa wale wanaosubiri, ila vitakuwa ni vitu ambavyo vimeachwa na wale wanaopambana.

NYONGEZA… NA AMBAYO NAIPENDA SANA…

The things I want to know are in books; my best friend is the man who'll get me a book I ain't read.
Vitu ninavyotaka vipo kwenye vitabu; rafiki yangu wa kweli ni yule atakayenipa kitabu ambacho sijakisoma.

Fanyia kazi kauli hizi kumi na uweze kuboresha maisha yako zaidi.

SOMA; Mambo Matano Yatakayotokea Utakapoanza Tabia Ya Kujisomea.

Hii Ndio Sababu Kwa Nini Watu Wanafurahia Pale Unapoanguka...

Ukweli ni kwamba, pale unapoanguka au kushindwa watu wanafurahia sana.
Unaweza kuona sio kweli lakini ndio hali halisi ilivyo.
Watu wengi wanaokuzunguka wanaweza kufurahia sana pale unapofanikiwa. Lakini pia unapoanguka kuna watu wanaofurahia sana.
Hawafurahii kwa sababu wanakuchukia wewe ila maisha yao ndio yanawalazimisha kufurahia hali hiyo.
Watu wengi wana maisha magumu sana, hivyo wakiona kuna mtu mwingine ana maisha magumu zaidi yao wanapata ahueni, kwamba angalau na wao hawako wenyewe.
Hii inawafanya wafurahi na hii inatokea kisaikolojia bila hata ya kulazimisha.
Hujawahi kuona mtu anamweleza mwenzake mataizo halafu wanaanza kushindana ni nani mwenye matatizo mengi?
Unamwambia mtu mimi nina matatizo kweli, sina fedha, nina mgonjwa, na kazi/biashara haziendi vizuri. Yeye anakwambia hunifikii mimi, sina hela kabisa, watoto wanahitaji ada na kazi sina.
Ukweli ni kwamba kila mmoja kati yenu anakuwa anafurahia kwamba sio yeye tu ana matatizo.
Unapoingia kwenye matatizo, jitahidi uweze kuyatatua na usonge mbele, wengi wa watakaokuwa wanakupa moyo wanafurahia wewe kuwepo kwenye matatizo hayo.

UKURASA WA 28; Kwa Nini Nisiwe Mimi…

Kama kuna watu ambao walianzia chini sana na leo wana mafanikio makubwa, kwa nini nisiwe mimi?

Kama kuna watu ambao hawakupata elimu kubwa ila wameweza kuleta mabadiliko makubwa, kwa nini nisiwe mimi?

Kama kuna watu ambao wametoka familia za kimasikini kabisa ila leo wameweza kutengeneza biashara kubwa, kwa nini nisiwe mimi?

Kama kuna watu ambao hawana viungo vyote vya mwili, ila leo wameweza kufanya mambo makubwa, kwa nini nisiwe mimi?

Kama kuna watu ambao waliweza kufungwa jela miaka mingi, ila walipotoka wakaleta mabadiliko, kwa nini nisiwe mimi?

Husemi hivi kwa sababu unawaonea wivu wale ambao wameweza kufanya makubwa, ila unawatumia wao kama chachu ya wewe kufikia mafanikio.

SOMA; Unataka Kujifunza Kitu Chochote Unachoona Ni Kigumu? Fanya Hivi...

Kuwepo kwa watu ambao wameweza kufanya makubwa licha ya kuwa na changamoto, inatudhibitishia kwamba hakuna kisichowezekana.

TAMKO LA LEO;

Kama kuna watu ambao wameanzia chini zaidi yangu, wameanza na hali mbaya zaidi yangu na wamepitia changamoto nyingi zaidi yangu ila wameweza kufikia mafanikio makubwa, ni ushahidi tosha kwamba inawezekana. Najua nikiweka juhudi na maarifa na kama sitakata tamaa lazima na mimi nitafikia mafanikio makubwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 29 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; USHAURI ADIMU; Usijenge Nyumba Kwenye Uwanja Wa Kukodi.

NENO LA LEO; Dawa Ya Kuondoa Wasi wasi…

”Action will remove the doubt that theory cannot solve” Pehyl Hsieh

Vitendo vitaondoa wasiwasi ambao nadharia haiwezi kutatua.

Unapokuwa na mpango wowote kwenye maisha yako, kuna wakati ambapo unakuwa na wasiwasi kama kweli itawezekana kwenda kama ulivyopanga.

SOMA; Vitu VITATU Vinavyoathiri Kipato Chako Na Jinsi Ya Kukiongeza.

Dawa ya kuondoa wasiwasi huu ni vitendo, yaani kuanza kufanyia kazi mipango yako. Usipofanya vitendo utaendelea kuwa na wasi wasi ambao hauwezi kukusaidia chochote.

Kumbuka; JUST DO IT, anza kufanya na wasiwasi utakimbia wenyewe.

SOMA; Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu; JUST DO IT.

Nakutakia siku njema.

Tuesday, January 27, 2015

Hii Ndio Faida Ya Kuboresha Maisha Yako...

Unapoboresha maisha yako, kila kitu kinachokuzunguka nacho kinakuwa bora.
Hii ni sheria ya asili.
Kazana kila siku kuboresha maisha yako na utajikuta unazungukwa na kila kilicho bora.
Kumbuka hili ni zoezi la kila siku, hakikisha leo unakuwa bora kuliko ulivyokuwa jana.

Unataka Kujifunza Kitu Chochote Unachoona Ni Kigumu? Fanya Hivi...

Njia bora kabisa ya kujifunza ni kufanya, kutenda.
Utasoma vitabu vyote, utafundishwa na walimu waliobobea ila kama hutatendea kazi yale uliyojifunza ni kazi bure.
Hakuna mtu aliyewahi kujifunza na akajua kuendesha baiskeli kwa kusoma vitabu tu. Hata baada ya maelekezo ulihitaji kuipanda baiskeli, kuanguka na hata kuumia ndio ukajua kuendesha baiskeli.
Sasa nini kinakuzuia wewe kuchukua hatua sasa? Hujajifunza? Anza kufanya.
Unataka kujifunza biashara, anza kufanya biashara, anza kidogo kidogo.
Unataka kujifunza kuandika makala nzuri anza kuandika, anza maneno matano nenda kumi, ishirini, mia...
Unataka kujifunza kilimo, nenda tafuta shamba, anza kulima.
Unataka kujifunza maisha, anza kuishi, sio kuishi kama kila mtu anavyoishi, bali kuishi kama ambavyo unataka kuishi.
Mwaka huu ni JUST DO IT.
Chochote unachotaka kwenye maisha yako, anza kukifanyia kazi. Hakuna kitakachokushinda.

#HADITHI_FUNZO; Kijana Aliyeiba Shoka..

Mtu mmoja alipoteza shoka lake na akawa anahisi mtoto wa jirani yake ndio amemuibia. Kila alipokuwa anamwangalia kijana yule, jinsi alivyotembea, jinsi alivyoongea alionekana kabisa ndiye mwizi wa shoka lake.

SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

Siku moja mtu yule akiwa anafanya usafi kwenye banda lake aliliona shoka alilofikiri limeibiwa. Alipomuona kijana yule tena hakuna tabia yake yoyote ambayo ilimuonesha kwamba ni mwizi.

Tunajifunza nini hapa?

Ukishahukumu mtu au kitu, utajitengenezea mazingira ya kukushawishi wewe ukubaliane na hukumu yako. Ni vyema kuangalia jambo katika uhalisia wake badala ya kuongozwa na hisia ambazo mara nyingi sio za kweli.

SOMA; Hizi Ndio Siri 21 Za Mafanikio

USHAURI ADIMU; Usijenge Nyumba Kwenye Uwanja Wa Kukodi.

Usijenge nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi.
Inaonekana rahisi sana kusema hivyo, na hivi kweli unaweza kufanya hivyo?
Yaani mtu kakudoshishia uwanja wake, ufanyie shughuli zako kwa siku chache wewe ukaamua kujenga kabisa nyumba ya kudumu?
Kwa akili ya kawaida huwezi kufanya hivyo, kwa sababu unajua unakaribisha matatizo. Mwenye uwanja wake akiutaka nyumba yako inakuwa haina thamani tena. Na hata ukisema utaununua uwanja huo, wakati umeshajenga atakutajia bei anayotaka yeye kwa sababu anajua huna yena ujanja.
Sasa ni wapi ambapo unajenga nyumba kwenye uwanja wa kukodi?
1. Unapofanya biashara na mteja wako akawa mmoja, mteja huyu anaweza kuitikisa biashara muda wowote.
2. Unapoajiriwa na kutegemea ajira kwa maisha yako yote. Hata kama ajira itakusumbua hutaweza kuondoka maana maisha yako yanategemea hapo.
Usikubali kabisa kujenga nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi.
Unafanyaje sasa kama tayari umeshajenga nyumba kwenye uwanja wa kukodi?
Rahisi, nunua uwanja mwingine na anza kujenga nyumba yako.
Kama unafanya biashara inayokufunga anza kuipanua biashara hiyo.
Kama upo kwenye ajira unayoitegemea kwa asilimia 100 kwa kipato, anza kutengeneza vyanzo vingine vya kipato.
Bado hujui unawezaje kutanua biasara yako zaidi? Au hujui ni jinsi gani unaweza kutengeneza kipato cha ziada nje ya mshahara? Haya unaweza kujifunza kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Tembekea www.kisimachamaarifa.co.tz
Nakutakia kila la kheri.
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Unataka Kuiona Dunia? Vua Miwani…

Unachokiona sasa hivi sio dunia halisi, bali ni dunia unayotaka kuiona wewe.

Hii ni kwa sababu kila mtu ni kama amevaa miwani yake ambayo inamuonesha kile anachotaka kuona.

Umewahi kuvaa miwani ya rangi? Unaonaje kitu unapokiangalia? Je unaonaje kitu kile unapovua miwani?

Hiko ndio kinachotokea kweye maisha yako ya kila siku. Unaona vitu kutokana na mtazamo wako, mawazo yako na hata matamanio yako.

SOMA; Njia Kumu(10) Za Kupata Utajiri Na Mafanikio.

Hali yoyote inayotokea, jinsi unavyoichukulia na jinsi utakavyokwenda nayo itategemea wewe unaionaje dunia .

Kama unataka kuiona dunia ya uhalisia, vua miwani, ondoa matarajio yote, ondoa hisia zinazoegemea upande mmoja na iangalie dunia kama vile ilivyo.

Utajifunza mengi na utaona fursa nyingi ambazo kwa sasa huzioni.

SOMA; Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.

UKURASA WA 27; Jaribu Mambo Mapya…

Kama unafanya kile ambacho kila siku unafanya, utapata matokeo ambayo kila siku uayapata.

Kama kuna kitu kipya ambacho unataka kupata, unahitaji kujaribu kufanya mambo mapya.

Kufanya mambo mapya sio kitu rahisi, inahitaji ujasiri wa kuweza kujihoji na kudhubutu kuchukua. Hii ni kwa sababu binadamu hatupendi mabadiliko.

SOMA; Kozi 1100 Unazoweza Kujifunza Bure Kupitia Mtandao.

Ili uweze kufikia mafanikio, unahitaji kujaribu mambo mengi mapya. Kuna ambayo utashindwa, lakini utajifunza na kujua njia bora za kufanya.

Kwa kujaribu mambo mapya utaweza kuziona fursa nyingi zinazokuzunguka na kuweza kuzitumia vizuri.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba ili niweze kupata matokeo mapya nahitaji kufanya mambo mapya. Kila mara nitakuwa nafanya mambo mapya kwenye maisha yangu ili kuweza kugundua fursa nyingi zinazonizunguka.

Tukutane kwenye ukurasa wa 28 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

NENO LA LEO; Faida Ya Kufanya Kile Unachosema…

“Walking your talk is a great way to motivate yourself. No one likes to live a lie. Be honest with yourself, and you will find the motivation to do what you advise others to do.” Vince Poscente

Kufanya kile unachosema ni njia kubwa ya kujihamasisha. Hakunamtu anayependa kuishi uongo. Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe na utapata hamasa ya kufanya kile unachoshauri wengine wafanye.

Kuwaambia wengine wafanye kitu ambacho wewe mwenyewe hufanyi ni kitu ambacho kinaweza kukuondolea uaminifu na pia kukukosesha fursa ya wewe kunufaika na kile unachowashauri wengine wafanye.

Anza sasa kutenda kile unachohubiri.

SOMA; Sababu TATU Kwa Nini Watu Wengi Wanashinda Kufikia Mafanikio.

Monday, January 26, 2015

Kauli Kumi Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Mahatma Gandhi.

Mahatma Gandhi alikuwa mpigania uhuru wa nchi ya India. Aliweza kuongoza harakati za kuipatia India uhuru kutoka kwa waingereza na alikuwa akitumia njia za amani katika harakati zake.

Mahatma Gandhi amekuwa akiwahamasisha wengi sana kwa maisha aliyoishi na harakati alizofanya na jinsi alivyoleta mabadiliko makubw akwenye nchi yake na dunia kwa ujumla.

Leo hapa utazipitia kauli kumi za kukuhamasisha kutoka kwake.

1. Happiness is when what you think, what you say, and what you do are in harmony.
Furaha ni pale ambapo mawazo yako, maneno yako na matendo yako yanaendana.

2. You must be the change you wish to see in the world.
Kuwa mabadiliko unayotaka kuyaona duniani.

SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

3. We may stumble and fall but shall rise again; it should be enough if we did not run away from the battle.

Tunaweza kukwama na kuanguka lakini tutainuka tena; na inatosha kama hatutayakimbia mapambano.

4. It is health that is real wealth and not pieces of gold and silver.

Afya ndio utajiri wa kweli, sio sarafu na dhahabu.

5. First they ignore you, then they laugh at you, then they fight you, then you win.

Kwanza wanakudharau, kisha wanakucheka, halafu wanakupinga, mwisho unashinda.

6. I suppose leadership at one time meant muscles; but today it means getting along with people.

Kuna kipindi uongozi ulikuwa ni nguvu; ila leo uongozi ni uwezo wa kuweza kushurikiana na watu.

SOMA; Dalili Kumi Kwamba Tayari Wewe Ni Kiongozi. 

7. You can chain me, you can torture me, you can even destroy this body, but you will never imprison my mind.

Unaweza kunifunga, unaweza kuniumiza, unaweza kuharibu mwili wangu, lakini huwezi kufunga akili yangu.

8. Live as if you were to die tomorrow. Learn as if you were to live forever.

Ishi kama utakufa kesho. jifunze kama utaishi milele.

9. You must not lose faith in humanity. Humanity is an ocean; if a few drops of the ocean are dirty, the ocean does not become dirty.

Usipoteze imani kwenye ubinadamu. Ubinadamu ni bahari, kama matone machache ya bahari hii ni machafu haimaanishi bahari nzima ni chafu.

10. The best way to find yourself is to lose yourself in the service of others.

Njia bora ya kujijua ni kujipoteza kwenye kuwahudumia wengine.

Soma kauli hizo kumi na zitumie katika maisha yako na shughuli zako za kila siku ili uweze kuboresha maisha yako.

SOMA;
Vitu VITATU Vinavyoathiri Kipato Chako Na Jinsi Ya Kukiongeza.

Yako Wapi Yale Maisha? Ni Wakati Wa Kulipa Deni Sasa.

Kila mtu alipokuwa mdogo alikuwa na picha kubwa sana ya maisha yake.

Ulipokuwa mdogo mtu akikuuliza unataka kuwa nani ulikuwa unajibu bila ya wasi wasi wowote kile unachotaka kuwa.

Ulikuw ana picha kubwa ya maisha yako, vile unataka yawe na kile unachotaka kutoa.

Safari ikaendelea na mahala fulani mambo yakabadilika.

Ukaanza kuambiwa hiki hakiwezekani, huwezi hiki, huna hiki, acha kuota na kadhalika.

Maneno haya uliyapuuza mwanzoni, ila yaliendelea kila siku, ukajaribu kufanya licha ya maneno haya, ukashindwa.

Na hapa ndio kitu kibaya sana kilichotokea, baada ya kushindwa tu, ukakubaliana nao, kwamba walikuwa sahihi, kwamba wewe huwezi, kwamba wewe huna, kwamba wewe unaota ndoto za mchana.

SOMA; Njia 12 za kurahisisha maisha yako.

Na sasa hatimaye unaishi maisha anayoishi kila mtu, huyafurahii lakini unaenda nayo tu, kwa sababu wanazidi kukuambia kwamba hiki ndio ulichopata, shukuru, huwezi kupata zaidi ya hiko.

Huu wote umekuwa ni uongo mkubwa sana uliojazwa kwenye kichwa chako. Wazazi na jamii zimejitahidi kukujengea uwezo huo, mfumo wa elimu ukamalizia kabisa na sasa unaona ndivyo mambo yalivyo.

Sasa leo jiulize swali moja…

Yako wapi yale maisha?

Tatizo letu binadamu ni kwamba kama hatujapata kile tunachokitaka kweli mioyo yetu haiwezi kutulia. Utafanya kila kitu ili kujiridhisha kwamba maisha ni mazuri lakini bado utakuwa na deni. Utajaribu kujiweka kwenye mazingira ya kuonekana una mafanikio kwenye maisha, lakini unapokaa chini na kutafakari maisha yako, utaona kuna deni fulani lipo ndani yako.

Sasa ni wakati wa wewe kulipa deni hilo.

SOMA; Kama Ulikuwa Hujui Bahati Inavyopatikana Soma Hapa.

Maswali muhimu wewe kujiuliza ni;

Je naridhishwa na kazi au biashara ninayofanya sasa?

Je naridhishwa na aina ya maisha ninayoishi sasa?

Je natoa mchango wa maana kwa kile ninachofanya kwenye jamii yangu na dunia kwa ujumla?

Je ningekuwa na uhakika nina mwezi mmoja tu wa kuishi, ningeutumia mwezi huo kufanya nini?

Maswali hayo yatakufungua ujue deni ambalo bado unadaiwa. Ukiweza kulipa deni hili maisha yako yatakuwa ya furaha hata kama huna utajiri mkubwa.

Huu ni wakati wa wewe kulipa deni. Jibu maswali hayo na chukua hatua.

Uzuri ni kwamba kwenye maisha hakuna kuchelewa. Katika wakati wowote ambao umegundua kwamba njia uliyokuwa unaenda siyo, unaweza kuibadili na ukaboresha maisha yako.

Nakutakia kile la kheri,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

SOMA; Hii Hapa Ni Tsh 604,000/= Utakayokabidhiwa Leo Usiku. Utaitumiaje?

UKURASA WA 26; Lazima Kuna Atakayekuwa Zaidi Yako.

Katika jambo lolote unalofanya kwenye maisha, lazima kuna mtu ambaye anafanya zaidi yako.

Kama ni biashara kuna ambaye atakuwa anafanya zaidi yako. Kama ni kazi kuna ambaye atakuwa anafanya zaidi yako.

SOMA; Mambo Matatu Muhimu Ya Kufanya Siku Ya Jumapili Ili Kuwa Na Wiki Yenye Mafanikio

Ukinunua gari utakutana na wengine wenye magari mazuri zaidi yako.

Kitu kibaya sana kwenye maisha ni kujilinganisha na wengine. Ukifanya hivi kila siku utaishia kuumia kwa sababu utaona watu ambao wanacho zaidi ya ulicho nacho.

Wewe ni wa tofauti, wewe ni wa pekee na una uwezo ambao hakuna mtu mwingine anao.

Badala ya kupoteza nguvu nyingi kujilinganisha na wengine, tumia nguvu hizo kujiboresha zaidi. Hakikisha siku ya leo unakuwa bora zaidi ya ulivyokuwa jana.

Hakikisha kazi unayofanya leo ni bora kuliko uliyofanya jana.

Kwa njia hii utaona mabadiliko makubwa kila siku kwenye maisha yako.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba katika jambo lolote ninalofanya kuna mtu anayefanya zaidi yangu. Najua mimi ni wa pekee na hakuna mtu ninayefanana naye kwa kila kitu. Sitajilinganisha na mtu yeyote. Nitahakikisha nakuwa bora kila siku inayokuja.

Tukutane kwenye ukurasa wa 27 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Hii Hapa Ni Tsh 604,000/= Utakayokabidhiwa Leo Usiku. Utaitumiaje?

NENO LA LEO; Jinsi Ya Kuimarisha Ujasiri Wako.

”Courage is like a muscle strenghthened by its use.” Ruth Gordon

Ujasiri ni kama msuli, unakuwa imara kadiri unavyotumika.

Ujasiri unao ila inawezekana umeufanya kuwa dhaifu kwa kuacha kuutumia kwa muda mrefu.

Ili kuimarisha ujasiri wako anza kuutumia. Pata hofu ila tumia ujasiri wako kufanya licha ya hofu unayoipata. Anza hivi kwa vitu vidogo na endelea hivyo kwa mambo makubwa zaidi.

Nakutakia simu njema.

SOMA; Mambo Matatu Muhimu Ya Kufanya Siku Ya Jumapili Ili Kuwa Na Wiki Yenye Mafanikio

Hii Hapa Ni Tsh 604,000/= Utakayokabidhiwa Leo Usiku. Utaitumiaje?

Sunday, January 25, 2015

Mambo Matatu Muhimu Ya Kufanya Siku Ya Jumapili Ili Kuwa Na Wiki Yenye Mafanikio

Jumapili ni siku muhimu sana kama unataka kuwa na wiki yenye ufanisi mkubwa.
Ni siku ambayo kama ukiitumia vizuri utakuwa na wiki yenye mafanikio na kama ukiitumia vibaya utakuwa na wiki mbaya na ya kupoteza muda.
Kuna vitu vitatu unavyoweza kufanya siku ya jumapili ili kuwa na wiki yenye ufanisi mkubwa na mafanikio makubwa.
1. Tafakari wiki inayoisha.
Fikiria jinsi ambavyo wiki yako ilikwenda. Angalia ni mambo gani ulifanikiwa kufanya na yakakusogeza mbele. Na pia angalia ni mambo gani ulishindwa kufanya na nini kilisababisha ukashindwa.
2. Panga wiki inayoanza.
Angalia wiki inayoanza na panga ni vitu gani unataka kukamilisha kwenye wiki hiyo. Panga mambo muhimu na weka vipaumbele kwenye matumizi ya muda wako.
3. Pata muda wa kupumzika.
Kama unafanya kazi wiki nzima, angalau tenga siku ya jumapili upumzike. Hata kama sio siku nzima, pata masaa machache ambayo utapumzisha mwili wako. Pia lala mapema ili uamke ukiwa na nguvu za kuanza vyema wiki yako.
Fanya mambo hayo matatu kila jumapili na utaona jinsi wiki yako itakavyokuwa bora.
Usipofanya hayo utajikuta kila jumatatu kwako ni BLUE MONDAY, jumanne ni hovyo, jumatano haisomeki, alhamisi angalau na ijumaa unafurahia maana wikiendi imekaribia tena.
Maisha ya aina hii hayatakufikisha kwenye mafanikio.

Hii Hapa Ni Tsh 604,000/= Utakayokabidhiwa Leo Usiku. Utaitumiaje?

Leo ni mwisho wa wiki na leo hii pia utakuwa mwanzo wa wiki.
Wiki ina siku saba na siku moja ina masaa 24, hivyo ukichukua siku saba ukazidisha kwa masaa 24 unapata masaa 168 kwa wiki.
Hivyo wiki moja ina masaa 168.
Ukichukua masaa hayo 168 ukazidisha kwa dakika 60 na ukazidisha tena kwa sekunde 60 unapata sekunde 604800.
Kwa maana hii wiki moja ina sekunde 604,800.
Sasa chukulia kila sekunde ni sawa na tsh moja, kwa hivyo kwa wiki moja una tsh 604,800/=.
Swali ni je unatumiaje fedha hizi?
Na swali makini ni je unaweza kutengeneza matumizi mazuri ya kila sekunde yako ili usipoteze thamani hiyo kubwa?
Inawezekana sana kwako wewe kutengeneza tsh moja kwa kila sekunde moja.
Kama unajua matumizi sahihi ya muda wako.

Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutumia Muda Au Fedha.

Muda una thamani kubwa sana kuliko fedha, hii ni kwa sababu ukipoteza fedha unaweza kupata nyingine ila ukipoteza muda huwezi kuupata tena.
Ila muda na fedha vina tabia moja inayofanana, ukivitumia bila ya kuandika kwenye karatasi unavipoteza.
Kitu muhimu cha kufanya kabla ya kutumia fedha au muda ni kupangilia matumizi hayo kwa kuandika kwenye karatasi au kitabu.
Usipopangilia kwa kuandika, utajikuta umetumia hovyo na hivyo kupoteza muda wako au fedha zako.
Weka mipango kabla ya kutumia muda au fedha.
Itakusaidia kuvitumia vitu hivyo viwili kwa makini.

Kama Unataka Kupata Unachotaka Fanya Hivi…

Kama kuna kitu ambacho unakitaka kweli, na upo tayari kufanya chochote ili kukipata, ulimwengu mzima utakusaidia kupata kitu hiko.

Hivyo kupata chochote unachotaka, hakikisha unakitaka kweli na unaamini kwamba unaweza kukipata.

SOMA; Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.

Kama utaamini bila kuyumbishwa na kufanyia kazi kile unachotaka hakuna kitakachokuzuia kukipata.

Anza sasa kufanyia kazi matakwa yako na usikubali mtu yeyote akuyumbishe kutoka kwenye lengo hilo.

SOMA; UMUHIMU WA KUSOMA ZAIDI NA KUSOMA KILA MARA;

UKURASA WA 25; Hakuna Njia Ya Mkato…

Akija mtu na kukuambia kuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio, kimbia haraka sana na usiendelee kusikiliza. Maana ukiendelea kusikiliza unaweza kujikuta umeshaanza kushawishika.

Hakuna nia ya mkato ya kufikia mafanikio, na kama ipo mafanikio utakayoyapata hayatadumu.

SOMA; Sheria 12 Kwa Wanaoanza Biashara Kutoka Kwa Bilionea Mark Cuban.

Kila kitu kinahitaji muda wa kukua ndio kiweze kufikia mafanikio. ukilazimisha kitu kabla ya muda wake utatengeneza madhara makubwa sana.

Kama jinsi ilivyo kwamba huwezi kuwapa wanawake tisa mimba moja ili waibebe kwenye mwezi mmoja, ni lazima mimba ikae miezi tisa ndio aweze kuzaliwa mtoto mwenye afya njema na atakayeweza kumudu maisha ya kawaida. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye kufikia mafanikio. Vitu vyote vizuri kwenye maisha vinahitaji muda.

Usikate tamaa pale unapoona unafanya kila kitu lakini bado huoni mafanikio. Jua kwamba muda muafaka bado, endelea kuweka juhudi. Muda muafaka utakapofika utashangaa kuona mafanikio yanatokea kila kona mpaka utajiuliza yalikuwa yamejificha wapi.

SOMA; Maswali Matatu Kwa Anayetaka Kuwa Mjasiriamali Kujiuliza Kutoka Kwa Richard Branson.

Unapoweka malengo na mipango yako, hakikisha unakomaa nayo na acha kuangalia vishawishi vya pembeni. Hivi vitakuchelewesha wewe kufikia malengo yako. Badala ya kupoteza muda wako kutafuta njia ya mkato, tumia muda huo kuimarisha njia yako ya kufikia mafanikio.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio. Kila kitu kizuri kwenye maisha kinahitaji muda ili kuweza kukifikia. Nitaendelea na malengo na mipango yangu hata pale nitapokuwa sioni mabadiliko. Najua siku muafaka ikifika mafanikio yatakuja kama mvua. Na nitakuwa tayari kuyapokea.

Tukutane kwenye ukurasa wa 26 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Mambo Matano Ya Kushangaza Kuhusu Siku Ya Jumatatu

NENO LA LEO; Usiache Jiwe Lolote Halijageuzwa…

“Leave no stone unturned.” Euripides

Usiache jiwe lolote halijageuzwa.

Katika kufikia mafanikio ni lazima ujaribu kila njia inayowezekana. Usiwe rahisi kukata tamaa baada ya kushundwa mara chache. Komaa na hakikisha kila njia inayowezekana umeifanyia kazi.

Usiache hata jiwe moja halijageuzwa, huenda jiwe hilo ndio lina hazina yako.

Nakutakia siku njema.

SOMA;  Vitu VITATU Vinavyoathiri Kipato Chako Na Jinsi Ya Kukiongeza.

Saturday, January 24, 2015

Bado Huzioni Fursa Zinazokuzunguka? Jiulize Maswali Haya Matatu.

Maswali matatu muhimu ya kukusaidia kugundua fursa zinazokuzunguka.
i. Ni kitu gani ambacho kinakupa msukumo mkubwa.
Katika vitu vyote unavyofanya au unavyofuatilia kuna kimoja ambacho kinakupa hamasa kubwa.
Ni kipi hiko?
ii. Je una vipaji gani?
Ni vitu gani ambavyo umekuwa unapendelea kufanya tangu ukiwa mdogo. Ni kitu gani ukikifanya watu wanakusifia umefanya vizuri?
iii. Ni kitu gani ambacho kinaweza kuwa na mchango mkubwa duniani?
Je ni matatizo gani ambayo yanawasumbua watu ambayo unaweza kuyapatia suluhisho? Ni kitu gani ambacho ukikifanya kitaleta mchango mkubwa kwenye jamii yako na dunia kwa ujumla.
Jibu maswali hayo na anza kufanyia kazi kile utakachopata.
Kumbuka JUST DO IT.

Jambo Moja La Kushangaza Kuhusu Maisha.

Jambo la kushangaza kuhusu maisha ni kwamba kila mtu anajua ni jinsi gani maisha ya mwenzake inabidi yawe ila hajui yakwake yanatakiwa kuwaje.
Ndio maana ni rahisi sana mtu kutoa maoni kwa mtu kwamba anakosea au hajui anachofanya, wakati maisha ya huyo mtoa maoni pia yanahitaji marekebisho.
Usianguke kwenye hili, hakikisha maisha yako yanakuwa kipaumbele kwako.

UKURASA WA 24; Kila Kitu Kina Gharama…

Mtu mmoja mwenye mafanikio aliwahi kuulizwa ni ipi siri ya mafanikio ambayo unaweza kumshauri mtu yeyote na yeye akafanikiwa?

Mtu yule alijibu ili kuwa na mafanikio kwenye maisha, bila ya kujali unaanzia wapi unahitaji vitu viwili;

1. Kujua ni nini unataka.

2. Kujua gharama unayotakiw akulipa na kuwa tayari kuilipa.

SOMA; Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Maisha

Kama umekuwa ukifuatilia kurasa hizi tokea siku ya kwanza, tayari unajua ni nini unataka kwenye maisha yako. Najua mpaka sasa una malengo yako na hivyo unayafanyia kazi. Kama mpaka sasa hujui ni nini unataka kwenye maisha yako au hujaweka malengo yoyote nakushauri uachie kusoma hapa na ufanye mambo mengine yatakayoendana na maisha magumu utakayoendelea kuwa nayo.

Kitu cha pili muhimu ili uweze kufikia malengo yako na mafanikio ni lazima ujue gharama ya mafanikio unayotaka. Na ukishaijua uwe tayari kuilipa. Gharama inaweza kuwa muda, nguvu, kusema hapana kwa mambo mengine na kadhalika.

Wewe jua gharama unayotakiwa kulipa na anza kuilipa, usichelewe hata sekunde moja.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba chochote ninachotaka kupata kwenye maisha yangu kuna gharama ninayotakiwa kulipa. Ili kufikia malengo niliyojiwekea niko tayari kulipa gharama zifuatazo(ziorodheshe kulingana na malengo yako na hali uliyonayo). Nitatumia muda wangu vizuri katika kulipa gharama hizi ili niweze kupata kile ninachotaka.

Tukutane kwenye ukurasa wa 25 hapo kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Kitu Hiki Kimoja Kitakufanya Uweze Kujiajiri, Uishie Kuwa Mwajiriwa Au Uishie Jela.

NENO LA LEO; Unachohitaji Ili Kusonga Mbele.

”To move ahead you need to believe in yourself...have conviction in your beliefs and the confidence to execute those beliefs.” Adlin Sinclair

Ili kusonga mbele unahitaji kuwa na imani kwako mwenyewe,  kuwa na uhakika juu ya imani zako na kudhubutu kufanyia kazi imani zako.

Mafanikio yoyote yanaanza na imani.

Kama unaamini inawezekana hakika itawezekana.

Kama unaamini haiwezekani, hakuna atakayeweza kufanya iwezekane.

Anza kujiamini na anza kufanyia kazi imani zako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Okoa Muda Huu Muhimu Ambao Unaupoteza Kila Siku Na Kukuchelewesha Kufikia Mafanikio.

Friday, January 23, 2015

Kitu Muhimu...

KITU MUHIMU NI KUKIFANYA KITU MUHIMU KUWA KITU MUHIMU...
Unaweza kuona sentensi hiyo ni rahisi sana ila pale unapojikuta umezama kati kati ya vitu ambavyo sio muhimu hapo ndio pa kuanzia.
Na mara kwa mara utajikuta unafanya kitu ambacho sio muhimu kwako.
Gundua haraka na fanya kitu muhimu.

Jibu Swali Hili Na Fanyia Kazi Jibu Lako, Maisha Yako Yatabadilika Sana.

Hili ni swali la msingi sana ambalo kama ukiweza kujiuliza na ukajijibu kwa uaminifu basi maisha yako yatabadilika na kuwa bora sana.
Msisitizo ni jibu kwa uaminifu na fanyia kazi majibu yako.
Swali lenyewe ni hili;
KAMA UNGEWEZA KUWA BORA SANA DUNIANI KWENYE KITU KIMOJA TU, UNGECHAGUA KITU GANI?
Andika jibu lako mara moja na anza leo hii kufanyia kazi na siku moja utaikumbuka siku ya leo na kushukuru sana hatua uliyochukua.
Kama umekwama na hujui wapi pa kuanzia niandikie email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz
KILA LA KHERI.

#HADITHI_FUNZO; Mto Unaotiririsha Watoto.

Kulikuwa na kundi la watu ambao walikuwa wamesimama kando kando ya mto. Mara watu wale walisikia sauti ya mtoto akilia kwenye maji. Walistuka sana kuona mtoto analia na kuzama kwenye maji. Mtu mmoja kwenye kundi lile aliruka haraka na kwenda kumwokoa mtu yule.

Wakati akiwa kwenye maji, mara wakasikia sauti ya mtoto mwingine akilia kwenye maji, mtu mwingine tena akaruka kuingia kwenye maji kumuokoa mtoto yule. Wakasikia tena mwingine na mwingine na mwingine, watu wote wakawa wameshaingia kwenye maji na wanahangaika kuokoa watoto wale.

SOMA; Kauli KUMI Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Nelson Mandela.

Akawa amebaki mtu mmoja ambaye hakuingia kwenye maji na akawa anaanza kuondoka. Wenzake walimuuliza kwa hasira unaenda wapi badala ya kuokoa watoto? Akawajibu nafuata mto huu kujua ni nani anayetupa hawa watoto kwenye maji.

Tunajifunza nini hapa?

Kuna mengi ya kujifunza; kwanza badala ya kukimbilia tu kutatua tatizo unaloliona ni vyema kujua chanzo cha tatizo ni nini. Maana unawez akung’ang’ania kutatua tatizo na ndio yakaongezeka.

Pia unapoona mtu hajihusishi na tatizo kwa wakati usikimbilie kumlaumu, anaweza kuwa anatafuta nini chanzo cha tatizo.

Tushirikishe ulichojifunza kweye hadithi hii kwa kuweka maoni hapo chini.

SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

JICHO KWA JICHO; Tutabaki Na Dunia Ya Vipofu.

Kama tunakubaliana ni JICHO KWA JICHO basi tukubaliane kwamba dunia nzima tutabaki vipofu.

Kama tunakubaliana ni JINO KWA JINO, tukubali pia kubaki vibogoyo dunia nzima.

Kama tutakubaliana UPANGA KWA UPANGA pia tujiandae kwa mafuriko ya damu duniani.

Tukisema CHUKI KWA CHUKI tujiandae kuishi dunia yenye simanzi kubwa.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

Kama ilivyo kwamba giza haliwezi kuondoa giza, bali mwanga ndio unaondoa giza.

Ndivyo ilivyo kwmaba chuki haiwezi kuondoa chuki, bali upendo ndio utaondoa chuki.

TUPENDANE.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

UKURASA WA 23; Pata Muda Wa Kupumzika…

Kijana mmoja alikwenda kwa mtu aliyefanikiwa kumuomba ushauri.

Kijana; Naomba uniambie itanichukua muda gani kufikia mafanikio makubwa kwa hiki ninachofanya?

Mshauri; Itakuchukua miaka kumi.

Kijana; Nipo tayari kufanya kazi usiku na mchana, je itanichukua muda gani?

Mshauri; Miaka ishirini.

Ukweli ni kwamba katika safari yetu ya kufikia mafanikio tunaweza kufikiri kwamba tukifanya kazi kwa muda mrefu itafupisha safari yetu. Hii sio kweli, miili yetu na akili zetu zinachoka. Na ili ziweze kufanya kazi vizuri zinahitaji kupata muda wa kupumzika.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Pata muda wa kutosha wa kulala na pata muda wa kupumzika pia. Utaweza kufanya majukumu yako kwa ufanisi mkubwa kama mwili wako una nguvu za kutosha na akili yako imechangamka.

TAMKO LA LEO;

Najua mwili wangu ndio rasilimali muhimu ya mimi kufikia mafanikio makubwa. Na ili mwili wangu uweze kufanya vizuri unahitaji kupumzika. Nitahakikisha napata muda wa kutosha wa kulala na wa kupumzika pia.

Tukutane kwenye ukurasa wa 24 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; UKURASA WA 21; Weka Vipaumbele Kwenye Maisha Yako.

NENO LA LEO; Acha Kujiandaa Kuishi…

“Stop acting as if life is a rehearsal. Live this day as if it were your last. The past is over and gone. The future is not guaranteed.” Wayne Dyer

Acha kuendesha maisha yako kama unajiandaa kuishi. Ishi siku hii ya leo kama vile ndio siku yako ya mwisho kuishi. Jana imeshapita. Kesho huna uhakika nayo.

Usipoteze maisha yako ya leo kwa kufikiria sana kuhusu jana na kesho.

Jana imeshapita na hivyo huwezi kuibadili.

Kesho badi haujafika na huwezi kuibadili pia.

SOMA; UKURASA WA 19; Ishi Leo..

Furahia muda ulioko nao sasa, na jifunze kwa yaliyopita na kujiandaa kwa yajayo, ila yasikuzuia kuishi na kufurahia maisha yako sasa.

Nakutakia siku njema.

Thursday, January 22, 2015

Kauli KUMI Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Nelson Mandela.

Nelson Mandela alikuwa mpingaji wa sera za kibaguzi nchini Afrika ya kusini. Pia alikuwa raisi wa Afrika kusini kati ya mwaka 1994 mpaka mwaka 1999. Alifungwa jela miaka 27 kutokana na harakati zake ila hakukata tamaa, alipotoka jela aliendelea na harakati na hatimaye kuweza kuwa raisi wa taifa ambalo halina ubaguzi.

mandela

Leo tutajifunza kauli kumi kutoka kwake ambazo zitatuhamasisha kuboresha maisha yetu na ya jamii inayotuzunguka.

1. To deny people their human rights is to challenge their very humanity.

Kuwanyima watu haki zao ni kutoa changamoto kwa ubinadamu wao.

2. It always seems impossible until its done.

3. Money won't create success, the freedom to make it will.
Fedha haitatengeneza mafanikio, uhuru wa kutengeneza fedha ndio utakaoleta mafanikio.

SOMA; Kauli KUMI Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Martin Luther King

4. If you want to make peace with your enemy, you have to work with your enemy. Then he becomes your partner.
Kama unataka kuleta amani na adui yako, unahitaji kufanya naye kazi na hapo mnakuwa washirika.

5. There is no passion to be found playing small - in settling for a life that is less than the one you are capable of living.
Hakuna hamasa kwenye kufanya vitu vidogo, kwa kukubali maisha ya chini kuliko ambayo una uwezo wa kuyaishi.

6. We must use time wisely and forever realize that the time is always ripe to do right.

Ni lazima tutumie muda kwa akili na tuelewe kwamba mara zote ni muda sahihi kufanya jambo sahihi.

SOMA; Lengo Langu Kubwa Kwenye Maisha; Kuwa Rais wa Tanzania.

7. Even if you have a terminal disease, you don't have to sit down and mope. Enjoy life and challenge the illness that you have.

Hata kama una ugonjwa ambao hauwezi kupona, hutakiwi kukaa chini na kukata tamaa. Furahia maisha na toa changamoto kwa ugonjwa ulionao.

8. No country can really develop unless its citizens are educated.
Hakuna nchi inayoweza kuendelea kweli mpaka wananchi wake wawe wameelimika.

9. When the water starts boiling it is foolish to turn off the heat.
Wakati maji yanaanza kuchemka ni upumbavu kuzima moto.

10. Only free men can negotiate. A prisoner cannot enter into contracts.

Ni mtu huru pekee anayeweza kujadili. Mfungwa hawezi kuingia mkataba.

Pitia kauli hizi kumi na zitakuhamasisha kufanya zaidi ili uweze kufikia mafanikio.

SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

UKURASA WA 22; Usiogope Kufanya Makosa…

Katika maisha, kazi na hata biashara kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho. Kitu hiko ni kwamba ni lazima utafanya makosa. Hata uwe umejiandaa kwa kiasi gani, hata uweke mambo vizuri kiasi gani bado utafanya makosa.

Hii ni kwa sababu hakuna mtu aliyezaliwa na kitabu cha matumizi kwamba maisha yako utayatumiaje. Ukinunua friji leo utapewa kitabu cha matumizi, ila unapopata mtoto haji na kitabu cha matumizi.

SOMA; USHAURI ADIMU; Unapokutana Na Tatizo Jiulize Jambo Hili Moja La Msingi.

Kuna kitu kizuri sana kuhusu makosa. Na kitu chenyewe ni kwamba makosa yanatufanya tujifunze zaidi ili kuwa bora zaidi. Bila makosa huwezi kujua ni njia ipi bora na ipi sio bora. Bila makosa huwezi kujua kama upo tayari au bado.

Makosa ndio njia nzuri ya wewe kujifunza, maana ukifanya makosa leo na ukaja ukarudia tena, mara ya pili inakuwa sio kosa bali umeamua.

Hivyo usiogope kufanya makosa, bali penda kujifunza kupitia makosa yako ili usiyarudie tena.

TAMKO LA LEO;

Najua makosa ni sehemu ya maisha yangu. Sitaogopa kufanya makosa maana nisipofanya makosa sitajifunza kitu chochote. Nitatumia makosa yangu kama sehemu ya kujifunza. Sitarudia tena kosa ambalo nimeshalifanya kwenye maisha yangu, kwa sababu mara ya pili litakuwa sio kosa tena bali ni uamuzi wangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 23 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Sheria NANE Za Kufanikiwa Kwenye Biashara Kutoka Kwa Warren Buffett.

NENO LA LEO; Chagua Kitu Hiki Kizuri…

“Life is change. Growth is optional. Choose wisely.” Karen Kaiser Clark

Maisha ni mabadiliko. Kukua ni uamuzi. Chagua kwa makini.

Maisha yanabadilika kila siku, ila kuamua kubadilika na kukua hiyo ni juu yako mwenyewe.

Kama ukichagua kwa mwakini na ukaendana na mabadiliko utaboresha maisha yako.

Chagua leo kukabiliana na mabadiliko na kuboresha maisha yako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Habari Za Kusikitisha; Kila Kitu Kinabadilika…

Wednesday, January 21, 2015

USHAURI ADIMU; Unapokutana Na Tatizo Jiulize Jambo Hili Moja La Msingi.

Tukubaliane kwamba lazima utakutana na matatizo.
Katika jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako, iwe ni kazi au biashara kuna wakati utakutana na matatizo.
Iwe matatizo hayo umesababisha wewe au hujasababisha una swali hili muhimu la kujiuliza?
Je kuna suluhisho la tatizo hili?
Kama suluhisho lipo huna haja ya kuhofu anza kufanyia kazi suluhisho hilo.
Kama suluhisho halipo pia huna haja ya kuhofu maana kuhofu hakutakusaidia kutatua tatizo hilo. Badala yake tumia muda wako kutafuta suluhisho la tatizo lako.
Kila la kheri.

#HADITHI_FUNZO; Aliyenusurika Kufa Kutokana Na Tabia Yake Nzuri.

Kulikuwa na mtu mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda cha kutengeneza mabarafu.

Siku moja jioni watu wakiwa wameshajiandaa kuondoka kulitokea tatizo na hivyo ikadibi arudi kulishughulikia. Alipomaliza kushughulikia tatizo lile alikuwa ameshachelewa, milango ilikuwa imefungwa na taa zimezimwa.

Alikuwa amenasa ndani ya kiwanda kile na hakukuwa na mwanga wala hewa. Na pia kwa baridi iliyokuwepo ni hakika kwamba asingefika asubuhi yake, lazima angekufa.

SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

Masaa yalienda huku akiwa ameshakata tamaa,  mara akasikia mtu anafungua milango.

Alishngaa sana nakuona kwamba huu ni muujiza kwake.

Alipoangalia alikuwa ni mlinzi ameingia na tochi yake na akamsaidia kutoka nje.

Wakati wanatoka mtu yule alimuuliza mlinzi walijuaje kwamba yupo ndani kule? Nani alimwambia?

Mlinzi alimjibu hakuna aliyeniambia, kiwanda hiki kina wafanyakazi wapatao 50, lakini ni wewe pekee ambaye huwa unanisalimia asubuhi na kuniaga jioni . Leo asubuhi ulinisalimia, ila jioni sikusikia ukiniaga hivyo nilipata wasiwasi utakuwa humu ndani.

Hakuwahi kufikiri kwamba tabia ndogo tu ya kusalimia mtu ingeweza kuokoa maisha yake.

Tunajifunza nini hapa?

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo unaweza kuvifanya kuwajali wengine, usipoteze chochote na pia siku moja vikakusaidia sana. Usipuuzie vitu hivi, huwezi kujua ni siku gani utahitaji msaada kwa vitu hivi.

MUHIMU; Kama una hadithi yoyote ambayo unaona watu wanaweza kujifunza tafadhali nitumie kwa wasap +255 717 396 253, hata kama ipo kwa kiingereza nitumie nitaiandaa vizuri na kuwashirikisha wengine. Isiwe ndefu sana.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Kama Sio Wewe Nani? Kama Sio Sasa Lini?

Kama sio wewe utakayebadili maisha yako unafikiri ni nani atakayefanya hivyo?
Kama sio sasa utabadili maisha yako umafikiri ni lini utafanya hivyo?
Usijidanganye kwamba kuna mtu atakayekuja kukutoa hapo ulipo, ni lazima nia hii itoke ndani yako.
Usijidanganye kwamba utabadili maisha yako kesho, kesho haijawahi kufika.
NI WEWE, NI SASA,
CHUKUA HATUA YA KUBADILI NA KUBORESHA MAISHA YAKO SASA.

UKURASA WA 21; Weka Vipaumbele Kwenye Maisha Yako.

Kuna mambo mengi sana ambayo unatamani kuyafanya kwenye maisha yako, ila kwa bahati mbaya sana huwezi kuyafanya yote.

Huwezi kufanya mambo yote unayotamani kufanya kwa sababu kuu mbili;

1. Huna muda wa kuweza kuyafanya yote hayo, una masaa 24 tu kwa siku na bado una malengo ya kuyafanyia kazi.

2. Huwezi kuwa ma nguvu ya kufanya kila kitu, una mwili ambao unachoka pia hivyo huwezi kufanya kila kitu.

Njia pekee ya kutumia muda wako na nguvu zako vizuri ni kufanya yale ambayo ni muhimu kwako kufikia malengo yako, kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa.

Ili uweze kujua ni yapi muhimu ya wewe kufanya tengeneza vipaumbele vyako na kisha vifanyie kazi.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia leo vipaumbele vyangu ni hivi(orodhesha vipaumbele hivyo). Sitatumia muda na nguvu zangu kufanya jambo lolote ambalo halitaniletea mafanikio ninayotarajia. Nitawekeza muda, nguvu na akili zangu zote kwenye vipaumbele hivi mpka pale nitakapopata ninachotaka.

Tukutane kwenye ukurasa wa 22 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Mambo Yanapokuwa Magumu Usiache Kitu Hiki Muhimu.

”When it is obvious that the goals cannot be reached, don't adjust the goals, adjust the action steps.”

Pale unapoona wazi kwamba huwezi kufikia malengo yako, usibadili malengo yako bali badili mipangilio yako.

Lengo lako sio kitu cha kubadili kwa sababu umekutana na kikwazo, angalia ni jinsi gani unaweza kuboresha mipango yako ili uweze kufikia lengo lako.

SOMA; Kama Huyu Ndio Mshindi, Fikiria Mshindwa Atakuwaje!!

Ukiona unataka kubadili lengo lako kwa sababu umeshindwa kulifikia basi hapo umeamua mwenyewe kushindwa.

Endelea kupambana mpaka ufikie lengo lako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; NENO LA LEO; Mafanikio Sio Mwisho, Kushindwa Sio Kiyama…

Tuesday, January 20, 2015

Kauli KUMI Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Martin Luther King

Martin Luther King Jr alikuwa mpigania haki za watu weusi nchini marekani. Huyu ni mmoja wa watu ambao walikufa wakipigania usawa baina ya binadamu wote. Kazi yake kubwa liyoifanya imeacha alama kubwa na leo tunaishi kwenye dunia ambayo ubaguzi wa rangi sio tatizo kubwa tena.

images

Hapa nimekukusanyia kauli Kumi za Martin Luther King ambazo zitakuhamasisha kuchukua hatua;

1. Darkness cannot drive out darkness; only light can do that. Hate cannot drive out hate; only love can do that.

Giza haliwezi kuondoa giza; ni mwanga pekee unaoweza kuondoa giza. Chuki haiwezi kuondoa chuki; upendo ndio unaoweza kuondoa chuku.

2. Faith is taking the first step even when you don't see the whole staircase.

Imani ni kupiga hatua ya kwanza hata kama huoni ngazi nzima.

SOMA; UKURASA WA 18; Hakuna Anayejali Maisha Yako Zaidi Yako Mwenyewe.

3. The ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort and convenience, but where he stands at times of challenge and controversy.

Kipimo kizuri cha mtu sio pale aliposimama wakati wa raha na mafanikio bali pale aliposimama wakati wa shida na kushindwa.

4. The time is always right to do what is right.

Mara zote muda ni sahihi kufanya kile ambacho ni sahihi.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

5. In the End, we will remember not the words of our enemies, but the silence of our friends.

Mwisho hatutakumbuka maneno ya maadui zetu, bali ukimya wa rafiki zetu.

6. I have decided to stick with love. Hate is too great a burden to bear.
Nimeamua kung’ang’ania upendo. Chuku ni mzigo mzito sana ambao siwezi kuvumilia.

7. We must learn to live together as brothers or perish together as fools.

Ni lazima tujifunze kuishi pamoja kama ndugu au tuangamia pamoja kama wapumbavu.

8. Our lives begin to end the day we become silent about things that matter.

Maisha yetu yanaanza kuisha pale tunapokaa kimya kwa mambo ambayo ni muhimu kwetu.

SOMA; Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.

9. Freedom is never voluntarily given by the oppressor; it must be demanded by the oppressed.

Uhuru kamwe hautolewi kwa hiari na mkandamizaji; bali unachukuliwa kwa kutaka kwa kandamizwaji.

10. Law and order exist for the purpose of establishing justice and when they fail in this purpose they become the dangerously structured dams that block the flow of social progress.

Sheria na taratibu zimewekwa kwa ajili ya kuanzisha haki na usawa na zinaposhindwa kutimiza lengo hilo zinakuwa hatari na kuzuia maendeleo ya kijamii.

Naamini umejifunza vitu muhimu kuhusu maisha kupitia kauli hizi kumi. Anza kufanyia kazi ili kuboresha maisha yako.

Makirita Amani,

makirita@gmail.com