Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, January 10, 2015

UKURASA WA 10; Umetengeneza Ulimwengu Wako Mwenyewe.

Upo hapo ulipo leo sio kwa sababu ya bahati au ajali, bali kwa sababu ndicho kitu ulichoamua kutengeneza mwenyewe. Maisha unayoishi leo ndio maisha uliyoamua kutengeneza mwenyewe, hujatengenezewa na wazazi wako, wala ndugu zako wala serikali yako. Ni wewe mwenyewe.

Kila unachokifikiria kwa muda mrefu kwenye maisha yako ndio kinachotokea. Kama unafikiria kwamba wewe ni mtu wa mikosi, visirani na kushindwa, kila kitu utakachokifanya kitatokea hivyo hivyo, hata kama utafanikiwa bado utaona kuna kitu umeshindwa.

Kama utaamini wewe ni mtu wa kufanikiwa na mwenye maisha mazuri hiko ndio kitakachotokea. Hata kama maisha yako yatakuwa magumu bado kuna vitu utaviona ni vizuri na hii itakufanya uendelee kukaribisha vitu vizuri zaidi.

Mawazo yako yanakutengenezea ulimwengu wako, iwe unajua au hujui na hivyo njia bora ya kuanza kubadilika ni kubadilisha mawazo yako na kubadilisha imani yako.

Kama unafuatilia siku hizi 365 na kufanya yale ambayo tunaelekezana tayari utakuwa na malengo yako. sasa tumia muda wako mwingi kufikiria jinsi gani unaweza kufikia malengo hayo na sio kufikiria kwa nini hutaweza kufikia malengo yako.

TAMKO LA LEO;

Maisha ninayoishi sasa nimeyatengeneza mwenyewe kutokana na fikra ambazo nimeruhusu zitawale akili yangu. Nitaweza kubadili maisha haya kama nitabadili fikra zangu na imani yangu pia. Kuanzia leo nachagua kuwaza ni jinsi gani naweza kufikia malengo yangu na ni jinsi gani naweza kuboresha maisha yangu. Naamini nawez akufanya chochote ninachoamua kufanya na ninaamini naweza kufanikiwa na kuboresha maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa kumi na moja kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment