Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, January 14, 2015

UKURASA WA 14; Kataa Kupokea Chochote Kizuri, Na Kubali Hiki…

Unapoamua kuboresha maisha yako, hakikisha kila kitu kinakuwa bora.

Jambo moja la kushangaza kuhusu maisha ni kwamba unapokataa kupokea ambacho sio bora, lazima unapata kilicho bora. Unapokataa kupokea kile unachokiona kizuri sasa, utapigana kupata kile kilichobora zaidi.

Kataa kufanya kazi ambayo sio bora na hatimaye utaongeza juhudi ili kuifanya iwe bora zaidi.

Kataa kuishi maisha yasiyo bora, maana hapa ndio utapata nguvu ya kuendelea kupambana ili kuyabadili.

Kataa kuwa na mahusiano au familia isiyo bora, kwa kufanya hivi utakazana kuiboresha zaidi.

Usikubali kupokea kitu chochote ambacho sio bora kwenye maisha yako, usiridhike na vitu vizuri, pambana kupata vile vilivyobora.

Nzuri itakufanya uwe na maisha ya kawaida ambayo kila mtu anayo. Bora itakufanya uwe na maisha unayotaka wewe na unayoyafurahia.

Kataa KIZURI, kubali kilicho BORA.

TAMKO LA LEO.

Kuanzia leo nakataa vitu vyote ninavyoona ni vizuri na nitakubali vile vilivyo bora tu. Sitakubaliana na hali yoyote ambayo hainiridhishi hata kama wengine wanaridhika nayo. Nitaendelea kupambana kila siku ili kuboresha kila eneo la maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa kumi na tano hapo kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment