Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, January 11, 2015

UKURASA WA 11; Watu Hawa Wanakurudisha Nyuma.

Hatimaye tupo ukurasa wa kumi na moja, kitabu chetu bado sana ila mabadiliko inabidi yaanze kuonekana mara moja.

Mpaka sasa umeshakubali kwamba maisha yako yako chini yako, umeshaweka malengo makubwa ambayo unayapigania, umeshakubali kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na unabadili imani zako ili uweze kuwa na imani ya kuona unaweza kufikia kile unachotaka.

Kwa yote haya hakuna tena cha kukuzuia kufikia mafanikio? Hapana bado vipo vinavyoweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio. Kimoja na kikubwa sana unachotakiwa kukiangalia leo ni watu wanaokuzunguka.

Watu wanaokuzunguka wanaweza kuwa maadui zako wakubwa sana hasa linapokuja swala la mafanikio. Kama watu wanaokuzunguka hawana mpango wa kubadili maisha yako nasikitika kukuambia kwamba hata wewe hutaweza kubadili maisha yako. Utajaribu na kukazana sana lakini utashindwa. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu maisha yako ni wastani wa maisha ya watu watano wanaokuzunguka.

Kama umezungukwa na watu watano wazembe, wewe utakuwa mzembe wa sita. Kama umezungukwa na wakata tamaa watano wewe utakuwa wa sita. Unaweza kujidanganya kwamba mimi nakaa nao tu lakini hawawezi kunibadilisha dhamira zangu, uongo, watakubadilisha tu na wala hawatumii nguvu kubwa.

Hivyo ni muhimu sana kuwachunguza wale wanaokuzunguka je watakufikisha kule unakotaka kufika? Kama jibu ni hapana unajua nini cha kufanya.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba watu wangu wa karibu wanaweza kunisaidia kufanikiwa au wakanifanya nishindwe. Leo nayapitia mahusiano yangu yote, kuangalia ni watu gani ambao wana mawazo ya mabadiliko na wapi ambao hawana. Kuanzia leo nitapunguza muda wangu ninaotumia na watu wote ambao hawana mpango wa kubadili maisha yao na kufikia mafanikio makubwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa kumi na mbili kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment