Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Showing posts with label USHAURI ADIMU. Show all posts
Showing posts with label USHAURI ADIMU. Show all posts

Tuesday, April 7, 2015

Faida kumi za kuwa na MAONO kama nilivyojifunza kwenye kitabu THE PRINCIPLES AND POWER OF VISION.

Rafiki yangu Meshack Maganga​​ alinipa zawadi ya kitabu hiki. Aliniambia ni kitabu kizuri sana. Nikawa na shauku kubwa ya kukisoma na hatimaye nimekisoma na kwa kweli ni kitabu ambacho sijui kwa nini nimechelewa kukisoma. Ni kitabu chenye misingi yote ya kukuwezesha kufikia kile unachotaka kwenye maisha. Na hata kama hukijui basi utapata mwanga na utajua uliletwa duniani kufanya nini.
Kwa ufupi sana nikushirikishe mambo kumi muhimu kuhusu MAONO...
1. Kama hakuna MAONO watu wanaangamia.
2. Kesho yako haipo mbele yako, ipo ndani yako.
3. Unaweza kuwa unaona lakini huna maono.
4. Hukuzaliwa ili ufuate mbio za panga, shule - kazi - kuoa/kuolewa - watoto - kubadilu kazi - kustaafu - kufa. Maisha ni zaidi ya hapo.
5. Mtu masikini kuliko wote duniani ni mtu ambaye hana MAONO.
6. Mtu aliyevurugwa kuliko wote duniani ni yule mwenye ndoto ila hajui afikieje ndoto zako.
7. Haijalishi ni jambo dogo kiasi gani unafanya, kama utaweka moyo wako wote na maisha yako yote kwenye jambo hilo halitasahaulika kamwe.
8. Kama upo tayari kuweka nguvu zako zote kwenye kitu, hakuna anayeweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio.
9. Haijalishi dunia ni kubwa kiasi gani, kuna sehemu yako kama utajua zawadi iliyopo ndani yako.
10. ELIMU SIO UFUNGUO WA MAISHA.(nimeiweka hii kwa herufi kubwa kama msisitizo)
Hiki nilichokushirikisha hapa ni punje tu ya mambo mengi utakayojifunza kwenye kitabu hiki. Kama hujakisoma nakusihi sana ukisome. Na kama huna mpango wa kusoma kitabu chochote kwenye maisha yako soma kitabu hiki tu basi. Utapata hazina kubwa sana ya kubadili na kuboresha maisha yako.
Kitabu kinapatikana house of wisdom bookshop nhc house, posta dar. Na bei yake ni ths 26,000/= tu.
Meshack anasema GO BIG OR GO HOME, na mimi naongeza kwamba BEFORE YOU GO HOME READ THIS BOOK, YOU MAY CHANGE YOUR MIND AND GO BIG.
TUPO PAMOJA.
www.amkamtanzania.com

Saturday, March 28, 2015

Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuishinda Hofu.

Ili kuishinda hofu, rudisha mawazo yako kwenye wakati uliopo sasa. Maana hofu kubwa unaipata pale unapofikiri mambo yaliyopita ambayo huwezi kuyabadili na kuwaza mambo yajayo ambayo huwezi kuyabadili pia.
Acha kuwaza mambo ambayo yameshapita, huwezi kuyabadili. Yatakuumiza na kukupa hofu kubwa.
Acha kufikiria mambo yajayo na kuyahofia. Bado hujayafikia na mambo hayatakuwa mabaya kama unavyofikiria sasa.
Weka mawazo yako sasa, kwenye wakati uliopo na utapata ujasiri mkubwa wa kufanya kile unachotaka kufanya.
Kumbuka ili kuwa na maisha mazuri ya kesho unatakiwa kuwa na maisha mazuri leo. Hivyo badala ya kuhofia kesho itakuwaje, tumia muda huo kuishi vizuri leo na kesho mambo yatakwenda vizuri.

Saturday, March 14, 2015

USHAURI ADIMU; Tangaza Kazi Yako, Usione Aibu Wala Kujali Wengine Watakuonaje.

Katika moja ya changamoto kubwa sana ambayo watu wanaipata na inawazuia kufikia mafanikio ni kushindwa kutangaza kazi zao.
Na hii inakwenda sana kwa wale ambao wanafanya kazi binafsi.
Kwa mfano kama unapika mandazi matamu sana, ila anayejua kuhusu mandazi hayo ni wewe na familia yako tu, je nafikiri unabiashara hapo?
Hata kama una kitu kizuri kiasi gani, kama watu hawajui kipo hawawezi kukifikia.
Kuna ile dhana kwamba kizuri chajiuza na kibaya chajitangaza, nakutangazia kuanzia leo kwamba sio kweli, na usiamini tena usemi huu.
Dunia ya sasa ina kelele nyingi sana, ni vigumu sana watu kujua kama upo kama hutowatangazia na wakajua kinapatikana wapi.
Kwa kazi yoyote unayofanya hakikisha unaitangaza kwa wale watu ambao wanafaa kuwa wateja wako.
Tahafhari ni kwamba usijaribu kutangaza kwa kila mtu, maana wengine hawawezi kuwa wateja wako na wewe huna muda wa kupoteza kwa kila mtu.
TANGAZA KAZI YAKO, NENDA KIFUA MBELE UKIJIVUNIA KAZI YAKO. JINSI UTAKAVYOKUWA NA HAMASA NA KAZI YAKO, NDIVYO UNAVYOWEZA KUWASHAWISHI WENGI ZAIDI.
ILA KAMA UNAONA AIBU, UNASUBIRI WATU WAJUE WENYEWE UNAJICHIMBIA SHIMO LAKO MWENYEWE, MAANA HAWATAJUA.

Wednesday, March 11, 2015

Hii Ndio Hatari Kubwa Ya Zama Hizi Tunazoishi..

Kama ulisoma historia wakati upo shuleni utakuwa unakumbuka kwamba binadamu amepitia vipindi vingi sana mpaka kufikia hapa tulipo sasa.

Kwanza kabisa binadamu alianza kwa kula mizizi na majani, baadae akawa anawinda, baadae akaanza kulima ikaendelea hivyo mpaka sasa maisha yanaonekana kuwa bora zaidi.

Binadamu tumepitia zama nyingi sana. Tumepita zama za mawe ambapo mawe ndio yalikuwa kifaa muhimu cha kufanyia kazi, zikaja zama za chuma, baadae mapinduzi ya viwanda na sasa tupo kwenye zama za taarifa.

SOMA; Kauli KUMI Za Marcus Aurelius Zitakazokufanya Uyaone Maisha Kwa Utofauti.

Katika kila zama kulikuwepo na hatari zake. Zamani sana katika zama za mawe binadamu alikuwa na hatari kubwa yakuliwa na wanyama wakali kama simba. Baadae zikaja hatari nyingine za magonjwa hatari, zikaja hatari nyingine za kuyumba kwa uchumi na kadhalika. Hapo ulipo huna hofu yoyote ya kuliwa na simba, lakini kuna simba wengine wakali ambao wanakunyemelea kila siku.

Hatari ya zama hizi ni nini basi?

Zama hizi zina hatari kubwa kuliko zama zote zilizopita. Na hatari hii ni mbaya sana kwa sababu watu hawaijui kama ni hatari. Hatari hii inatokana na faida ya zama hizi pia ambayo ni TAARIFA.

Taarifa imekuwa hatari sana kwenye zama hizi za taarifa. Sasa hivi unaweza kupata taarifa masaa 24 kwa siku siku saba kwa wiki na mwaka mzima. Tatizo kubwa ni kwamba taarifa hizi ziko hasi sana na ziakukatisha tamaa, kukujaza hofu na kukurudisha nyuma.

SOMA; Unataka Kuiona Dunia? Vua Miwani…

Zama hizi tumekuwa na vifaa ambavyo vinatuwezesha kupata taarifa popote pale tulipo, hata kitandani. Vifaa hivi ni simu zenye uwezo mkubwa au kwa jina lingine smartphones. Hizi zimetuunganisha na mitandao mingi sana ambayo wka silimia 90 haina manufa amakubwa kwetu. Lakini tumeng’ang’ania vitu hivi na vinaendelea kuturusisha nyuma.

Unahitaji kujichunguza sana ni aina gani ya tarifa unazopokea kila siku. Ni aina gani ya mitandao unayotembelea kila siku. Maana kila kinachoingia na kukaa kwenye akili yako wka muda mrefu ndio kinatokea kwenye maisha yako.

Jilinde na hatari hii kubwa. Jua ni taarifa gani utahitaji kuchukua na zipi unahitaji kuziepuka.

Nakutakia siku njema.

SOMA; SIRI YA 42 YA MAFANIKIO; Mtazamo Wako Utapima Mafanikio Yako.

Sunday, March 1, 2015

Kama Una Vipaumbele Huna Kipaumbele...

Kama una vipaumbele maana yake ni huna kipaumbele.
Kama una vitu vingi ambavyo ni muhimu kwako maana yake huna ambacho ni muhimu kwako.
Kipaumbele maana yake ni kitu kimoja unachokipa upendeleo na kukifanya kabla ya kufanya kitu kingine.
Sasa kama una kipaumbele zaidi ya kimoja, maana yake hakuna ambacho ni muhimu sana kwako.
Chagua kitu kimoja muhimu sana na kifanyie kazi, ukimaliza chagua kingine ndio ufanyie kazi.
Usiwe na vipaumbele, kuwa na kipaumbele.

Wednesday, February 25, 2015

USHAURI ADIMU; Kwa Sababu Umelipia Haimaanishi Utumie Yote.

Siku hizi ukinunua kifurushi cha mawasiliano kwenye mitandao ya simu, unapewa meseji 250 kwa siku.
Ukisema utume meseji zote hizi, hata kama utatumia dakika moja kutuma meseji itakuchukua dakika 250 ambazo ni sawa na masaa manne.
Sasa kama utatumia masaa manne kutuma meseji kwa siku kila siku inabidi uwe unafaidika sana na zoezi hilo.
Lakini vinginevyo hutumi meseji zako zote kwa sababu umezilipia, unatuma zile unazohitaji.
Ukienda kula hotelini, mezani utakuta kuna chumvi, iko pale na unaweza kutumia vyovyote utakavyo. Lakini huwezi kuweka chumvi yote kwenye chakula kwa sababu ipo pale na umeshailipia kwenye chakula.
Chochote unachofanya kwenye maisha usifanye kwa sababu kipo, au kwa sababu kila mtu anafanya. Ila fanya kwa sababu ndicho unachohitaji kufanya.
Nakutakia kila la kheri.

Tuesday, February 24, 2015

USHAURI ADIMU; Chukua Ushauri Kwa Mtu Huyu Tu, Achana Na Wengine Wote.

MSOMAJI; Nimekuwa nikisoma baadhi ya makala zako. Naomba nikuulize. Je, mtu unapoamua kufanya biashara fulani,ukaomba ushauri kwa watu,hao watu kwa uoga wao wakakuvunja moyo kuwa utakuwa kwenye risk zaidi. Unaionaje hii?asante,naamini utanijibu niweze kuelewa.

MIMI; Usiombe ushauri kwa mtu ambaye hafanyi biashara, atakudanganya. Usiombe ushauri kwa mtu aliyepata hasara kwenye biashara, atakufundisha makosa yake. Omba ushauri kwa mtu anayefanya biashara yenye mafanikio, na mtu huyo awe tayari kutoa ushirikiano.

Moja ya mawasiliano yangu na msomaji leo. Nimeona inaweza kukusaidia na wewe.
Kila la kheri.

Saturday, February 21, 2015

Sababu Namba Moja Kwa Nini Hufanikiwi Kwenye Kazi Unayofanya.

Sababu namba moja kwa nini hufanikiwi kwenye kazi unayofanya ni kwa sababu unaangalia fedha tu.
Yaani wewe kinachokusukuma ufanye kazi ni kwa sababu unapata fedha.
Sasa fedha inapokuwa ndio hamasa kwako utafanya kile tu ambacho kinakuletea fedhq, hutataka kwenda hatua ya ziada na hivyo kujinyima fedha nyinhi zaidi baadae.
Ufanyeje sasa?
Hamasa yako kubwa isiwe fedha bali iwe mapenzi ya dhati kwa kile unachofanya.
Penda sana kile unachofanya na kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana.
Kuwa mbunifu na mara zote penda kwenda hatua ya ziada.
Kwa hali hii fedha zitakuja mpaka utashangaa zilikuwa zimejificha wapi. Amini hilo, nakuambia kwa uzoefu.

Do not hire a man who does your work for money, but him who does it for love of it.—Henry David Thoreau,

Thursday, February 19, 2015

Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.

Naweza kusema sasa hivi nimekuwa mlevi wa kitu kimoja, kusoma. Na sio kusoma tu, bali kusoma vitu vizuri ambavyo vinanifanya kuwa tofauti, kufikiri tofauti na hata kupata maarifa zaidi.

Naweza kusema kw akujivunia kwamba chochote ninachofanya sasa kinatokana na maarifa makubwa ninayoyapata kwa kusoma vitabu. Nasoma vitabu vingi na kwa sasa nasoma angalau vitabu viwili kwa wiki, wiki nyingine nasoma zaidi ya hapo ila nahakikisha kila wiki sishuko chini ya hapo.

Mwaka huu 2015 lengo langu ni kusoma vitabu visivyopungua 150, ukichanganya na vingine zaidi ya 200 nimesoma kwa miaka miwili iliyopita, maarifa yangu yataongezeka maradufu.

Leo siandiki haya kukuonesha kwamba nasoma sana ila nataka nikushirikishe faida kumi ninazozipata kwa kusoma, ukiacha kuongeza maarifa ambacho ndio kila mtu anafikiria.

SOMA; Mambo Yamebadilika, Hatari Sio Hatari Tena, Salama Ndio Hatari...

1. Burudani.

Kusoma ni burudani na ni burudani ambayo haina madhara yoyote kwenye mwili wako au maisha yako. Kuna baadhi ya vitabu unapovisoma unapata hisia nzuri za kiburudani na unaona uzuri na utamu wa maisha.

2. Kuhamasika.

Tunaishi kwenye dunia ambayo inakatisha tamaa sana. Kila jambo ambalo unajaribu kufanya kuna watu watakuambia haiwezekani au kuna watu watajaribu kukuwekea vikwazo. Unapokuwa unasoma vitabu unapata hamasa kubwa sana ya kufanya kile unachotaka kufanya. Unaposoma maisha ya wengine na kuona jinsi walivyopitia magumu, unapata moyo kwamba inawezekana.

SOMA; USHAURI ADIMU; Usijenge Nyumba Kwenye Uwanja Wa Kukodi.

3. Mshauri(mentor)

Ni muhimu sana kuwa na mshauri wako, ambaye anakuonesha wapi pa kupita ili uweze kupata kile unachotaka. Mara nyingi mshauri huyu inabidi awe ameshapitia unakopitia wewe. Katika mazingira yetu ya kitanzania ni vigumu sana kupata mtu wa aina hii, na hata ukimpata anaweza asipate muda mwingi wa kwenda na wewe sawa. Ila vitabu, vitabu ni mentor mzuri sana. Unaweza kusoma maisha ya watu ambao wamefanikiwa kwenye kile unachofanya na wakakupa mwongozo mzuri sana.

4. Kuwa bora zaidi.

Licha ya kuongeza tu maarifa, kusoma kuna kufanya unakowa bora zaidi katika kila eneo la maisha yako. Kabla sijajingea tabia ya kujisomea nilikuwa mtu wa kuhukumu, kukwazika, kuchukia, kubishana na mengine mengi. Lakini yote hayo nimeyaacha sasa, sina tena muda wa kuhukumu kwa sababu najua kila mtu ana matatizo yake, kila mtu anachagua maisha yake. Sikwaziki tena wala kukasirishwa na mtu kwa sababu najua anayetaka kukukasirisha anataka na wewe uwe na matatizo kama aliyonayo yeye, nishakuwa mjanja, sinunui tena matatizo ya watu. Na kilicho bora zaidi sibishani, zamani nilikuwa nikiwa na wazo langu na mtu akalipinga, nabishana nae mpaka nihakikishe amekubaliana nami, lakini sasa sibishani tena, kwa sababu nimejifunza kama wazo lako ni sahihi huna haja ya kulipigania, maana mwisho wa siku ukweli utashinda. Na kama wazo lako sio sahihi pia huna haja ya kubishana maana hakuna atakayekusikiliza au kujali.

5. Kuishi maisha tofauti tofauti.

Mtu anayesoma vitabu anaishi maisha zaidi ya 1000 kabla hajafa, mtu asiyesoma vitabu anaishi maisha mamoja tu mpaka anakufa. Sasa unafikiri ni yupi ambaye anakuwa na maisha mazuri kati ya hawa wawili? Kitabu kinaweza kukutoa hapa na kukupeleka kwenye mapiramidi ya misri, kikakupeleka marekani, kikakupeleka china na kadhalika.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

6. Kuandika.

Moja ya faida kubwa ninazopata kwa kusoma vitabu ni kuandika. Ndio huwezi kuandika kama husomi, nazungumzia kitu ambacho kinaweza kuwasaidia wengine. Huwa naandika kila siku, zamani ilikuwa maneno 1000 ninapoamka asubuhi lakini sasa ni zaidi ya maneno 2000. Fikiria pale unapohitaji kuandika kila siku, jumatatu mpaka jumatatu, mwaka mzima, ni kazi ngumu eh? Kuna siku naweza kuamka sijisikii kabis akuandika, nachukua kitabu na kuanza kusoma, nusu saa baadae nakuwa nimepata mawazo zaidi ya matano ya kitu ninachotaka kuandika. Mara nyingi mawazo hayo hayatoki kwenye kitabu hiko ninachosoma, ila kile kitendo cha kukaa na kuanza kusoma ni kama milango ya akili inafunguka na kuanza kumwaga mawazo mazuri. Napenda sana hii hali.

7. Kutunza muda.

Unapoanz akujijengea tabia ya kujisomea, moja kwa moja unaanza kujijengea tabia ya kutunza muda. Hutapoteza tu muda na kuona huna cha kufanya kwa sababu muda wote una kitabu cha kusoma. Na pale ambapo una kitu cha kukusukuma umalize kitabu haraka kila dakika chache utakazopata utazitumia vizuri kusoma.

8. Kupunguza gharama.

Unapojijengea tabia ya kujisomea, muda wako mwingi unautumia kusoma hivyo hutapata mawazo ya nifanye nini sasa na kujikuta umeenda kufanya jambo ambalo linakuingiza kwenye gharama ambazo sio za msingi. Naweza kuhitaji kubadili mazingira nikachagua kwenda kwenye hoteli kubwa, nikiwa na kitabu nasoma, naagiza maji ya kunywa. Natulia na kusoma hata kwa masaa mawili bila ya kufanya kingine chochote. Ila ukiend akwenye hoteli ya aina hii na huna kitu cha muhimu cha kufanya, utajikuta unatumia gharama kubwa sana.

SOMA; Acha Kuifanya Hali Mbaya Kuwa Mbaya Zaidi.

9. Kuepuka umbea na majungu.

Angalau watanzania tumebobea kwa hili. Kama unapenda kufuatilia umbea na majungu sikulaumu kwa sababu kama huna kingine cha kufanya utafanya nini sasa? Yaani umeamka asubuhi huna ratiba yoyote ya siku zaidi ya kwenda kazini kama ulivyoenda jana. Utaanza kuangalia I nini kinaendelea, Diamond ana mpenzi gani mpya, kampa mimba nani, kavaa viatu vya shilingi ngapi au valentine alitumia kiasi gani cha fedha. Sawa, sikukatazi kufuatilia, ni burudani, lakini kabla ya kuipa burudani hii kipaumbele je maisha yako umeyapa kipaumbele?

10. Kuongeza kipato.

Hii ipo karibu sana na kupata maarifa maana maarifa ndio yanafanya kipato chako kuongezeka. Lakini nimetaka niiweke yenyewe ili kuonesha msisitizo zaidi. Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, nilisoma kitabu cha Robin Sharma, na moja ya vitu alivyoshauri ni hiki; KUONGEZA KIPATO CHAKO MARA MBILI, ONGEZA KUSOMA KWAKO MARA TATU. Nikasema nafanyia kazi hilo, kadiri ninavyojisomea ndivyo kipato changu kinaongezeka, mpaka wakati mwingine nashangaa nilichelewa wapi sikuanza mapema kama miaka kumi iliyopita.

Hizo ndio faida kumi za kujijengea tabia ya kujisomea. Anza kujisomea leo, na utaanza kunufaika na hayo na mengine mengi ambayo sijayaandika hapa. Nina uhakika na haya ninayokuambia hapa, hebu anza kufanya na lazima utaona mabadiliko.

SOMA; Habari Za Kusikitisha; Kila Kitu Kinabadilika…

KARIBU KWENYE KUNDI LA KUJISOMEA;

Kama unataka kujijengea tabia ya kujisomea na ungependa kupata kitu cha kukusukuma uweze kusoma nakukaribisha kwenye kundi la kusoma vitabu. Kundi hili linaitwa VORACIOUS READERS, katika kundi hili tunasoma vitabu viwili kwa wiki na ni muhimu kila mwanachama kusoma na kujadili angalau kitabu kimoja. Kupata maelezo zaidi ya kundi hili bonyeza maandishi haya.

MUHIMU; Usitake kujiunga na kundi hili kwa sababu tu umehamasika, ni muhimu sana utenge muda wa kujisomea na usome kweli, usipofanya hivyo unaondoka kwenye kundi.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.

TUPO PAMOJA.

Wednesday, February 11, 2015

Mambo Yamebadilika, Hatari Sio Hatari Tena, Salama Ndio Hatari...

Kuna wakati ambapo ilikuwa inaonekana kuacha kazi na kuingia kwenye ujasiriamali ni hatari kubwa sana.
Ajira zilikuwa na usalama, angalau mtu alikuwa na uhakika wa kupata kipato cha kumtosha kuendesha maisha yake.
Ila sasa hivi mambo yamebadilika kabisa, hatari sio hatari tena, na salama imekuwa hatari, tena hatari kweli kweli.
Sasa hivi kukaa kwenye ajira na kuitegemea ajira tu ni hatari kubwa saba.
Kwanza kipato hakitoshelezi, gharama za maisha zinaongezeka kila siku.
Pili nafasi zenyewe ni finyu hivyo hakuna wa kukung'ang'ania.
Tatu hata ukiongeza juhudi kipato chako bado kinaamukiwa na mtu mwingine.
Nne unaweza kufukuzwa na ukabaki mikono mitupu.,,
Lakini ujasiriamali umekuwa salama sana.
Kwanza unakuwa na uhuru kwenye matumizi ya muda wako
Pilu unafanya kitu unachokipenda
Tatu ukiongeza juhudi na maarifa na kipato chako nacho kinaongezeka.
Nne, hakuna wa kukufukuza, labda uamue kujifukuza mwenyewe.
Je unaamua kuchagua hatari au salama?
Jibu unalo mwenyewe,
Nakutakia kila la kheri kwenye kuchagua ili uchague kilicho chema kwako.
TUPO PAMOJA.

Tuesday, January 27, 2015

USHAURI ADIMU; Usijenge Nyumba Kwenye Uwanja Wa Kukodi.

Usijenge nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi.
Inaonekana rahisi sana kusema hivyo, na hivi kweli unaweza kufanya hivyo?
Yaani mtu kakudoshishia uwanja wake, ufanyie shughuli zako kwa siku chache wewe ukaamua kujenga kabisa nyumba ya kudumu?
Kwa akili ya kawaida huwezi kufanya hivyo, kwa sababu unajua unakaribisha matatizo. Mwenye uwanja wake akiutaka nyumba yako inakuwa haina thamani tena. Na hata ukisema utaununua uwanja huo, wakati umeshajenga atakutajia bei anayotaka yeye kwa sababu anajua huna yena ujanja.
Sasa ni wapi ambapo unajenga nyumba kwenye uwanja wa kukodi?
1. Unapofanya biashara na mteja wako akawa mmoja, mteja huyu anaweza kuitikisa biashara muda wowote.
2. Unapoajiriwa na kutegemea ajira kwa maisha yako yote. Hata kama ajira itakusumbua hutaweza kuondoka maana maisha yako yanategemea hapo.
Usikubali kabisa kujenga nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi.
Unafanyaje sasa kama tayari umeshajenga nyumba kwenye uwanja wa kukodi?
Rahisi, nunua uwanja mwingine na anza kujenga nyumba yako.
Kama unafanya biashara inayokufunga anza kuipanua biashara hiyo.
Kama upo kwenye ajira unayoitegemea kwa asilimia 100 kwa kipato, anza kutengeneza vyanzo vingine vya kipato.
Bado hujui unawezaje kutanua biasara yako zaidi? Au hujui ni jinsi gani unaweza kutengeneza kipato cha ziada nje ya mshahara? Haya unaweza kujifunza kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Tembekea www.kisimachamaarifa.co.tz
Nakutakia kila la kheri.
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Wednesday, January 21, 2015

USHAURI ADIMU; Unapokutana Na Tatizo Jiulize Jambo Hili Moja La Msingi.

Tukubaliane kwamba lazima utakutana na matatizo.
Katika jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako, iwe ni kazi au biashara kuna wakati utakutana na matatizo.
Iwe matatizo hayo umesababisha wewe au hujasababisha una swali hili muhimu la kujiuliza?
Je kuna suluhisho la tatizo hili?
Kama suluhisho lipo huna haja ya kuhofu anza kufanyia kazi suluhisho hilo.
Kama suluhisho halipo pia huna haja ya kuhofu maana kuhofu hakutakusaidia kutatua tatizo hilo. Badala yake tumia muda wako kutafuta suluhisho la tatizo lako.
Kila la kheri.

Monday, January 19, 2015

Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Binadamu tunapenda kulalamika sana na hata kuwalaumu wengine. Hakuna mtu anayependa aonekane kwamba yeye ndio amechangia kusindwa kwa jambo fulani. Hivyo katika jambo lolote lile linalotokea watu hukimbilia kumtafuta mchawi, yaani mtu wa kulaumu.

SOMA; Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku.

Sasa kwa tabia hii ya kulalamika na kulaumu inakurudisha sana wewe nyuma katika maendeleo ya maisha yako.

Huwezi kufikia mafanikio kama kila mara wewe ni mtu wa kulalamika na kulaumu wengine.

Leo hii nataka ufanye changamoto moja ambayo itakuwezesha kuondokana na tabia hii ili uweze kufikia mafanikio.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Kwa siku kumi kuanzia leo, jiepushe kulalamika au kumlaumu yeyote. Hakikisha siku nzima imesiha bila ya kulalamika au kulaumu. Ikitokea umefanya siku ya kwanz aila ya pili ukajisahau na kulalamika, unafuta na kuanz atena upya. Endelea hivi mpaka siku kumi ziishe bila ya kulalamikia kitu chochote.

Pia katika siku hizi kumi usimseme mtu kwa jambo lolote baya, yaani usisengenye, usishiriki majungu na wala usifanye umbea. Hizi ni tabia ambazo zinakurudisha sana nyuma.

SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Fanya changamoto hii na kama ukifanikiwa kukamilisha siku kumi nitumie email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz kunijulisha umeionaje hali hiyo na pia nitakuwa na zawadi nzuri kwako.

Na changamoto ianze, tutakutana upande wa pili, KARIBU SANA.

Sunday, January 18, 2015

Acha Kuifanya Hali Mbaya Kuwa Mbaya Zaidi.

Mara kwa mara kwenye maisha tunakutana na matatizo.
Baadhi ya matatizo haya yanaweza kuwa makubwa sana kiasi cha kutukatisha tamaa.
Lakini mara nyingi matatizo haya huanza kidogo na sisi wenyewe kuyafanya kuwa makubwa zaidi.
Moja ya njia tunayotumia kufanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi ni kutumia hisia wakati unapokutana na hali mbaya.
Hisia hutufanya tuache kuangalia ukweli ni upi na kuishia kuona kwamba kwa nini sisi tunapata matatizo.
Acha sasa kutumia hisia pale unapokutana na matatizo. Tatizo lolote linapotokea, tulia na chambua tatizo hilo kwa kina kujua nini chanzo na unawezaje kulitatua.
Ila ukiingiza hisia utaona njia rahisi kwako ni kukata tamaa au hata kujiua.

USHAURI ADIMU; Najua Kitu Kimoja….

Najua kitu kimoja… kwamba sijui chochote.

Kauli hii tatanishi ilitolewa na mwanafalsafa Socrates.

Kauli hii inaushauri muhimu sana kwetu;

1. Kama kuna kitu kimoja muhimu ambacho unatakiwa kujua ni kwamba hujui chochote.

2. Jiulize kwa kile ambacho unafikiri unakijua, na utagundua kwamba hukijui maka ulivyofikiri unakijua.

3. Huwezi kujua kila kitu.

4. Ni muhimu sana kujifunza kila siku.

Yafanyie kazi hayo.

Friday, January 16, 2015

Habari Za Kusikitisha; Kila Kitu Kinabadilika…

Leo nilipanda dala dala ambapo nilikaa kiti cha nyuma ya dereva, dereva alikuwa na mazungumzo na mtu mmoja aliyekaa mbele, anaonekana ni kondakta au dereva ila sio wa gari hiyo niliyopanda. Hivyo kwa sehemu yote ya safari walikuwa wakihadithiana ni jinsi gani anzi hizo kazi ya daladala inalipa. Waliongea sana kwamba kabla ya ujio wa madaladala makubwa ya kampuni ya uda hapa dar, walikuwa wakipata fedha nyingi sana. Wakawa wanalalamika vile mabasi ya uda yanavyobeba watu wengi na yanavyoweza kutumia bara bara nyingi kushinda daladala za kawaida

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Kwa muda ambao nilifuatilia maongezi yao, walionekana kukatishwa tamaa sana na mabadiliko haya makubwa yaliyotokea na yanayoendelea kutokea.

Ukweli ni kwamba mabadiliko yanatokea kila sehemu sasa. Hata zile sehemu ambazo watu walifikiri wataendelea kunufaika milele mambo ni magumu sana. Na huu ni mwanzo tu wa mabadiliko, mabadiliko yataendelea kuja na kwa kasi ya ajabu sana.

SOMA; Vitu Vitatu Vinavyoathiri Kipato chako Kwenye Chochote Unachofanya.

Nasema hizi ni habari za kusikitisha kwa sababu watu wengi hawapendi mabadiliko. Watu wanapenda kuendele akufanya kile alichkuwa wanafanya, wapate kile walichokuwa wanapata. Lakini dunia haiendi hivi, dunia inabadilika kila siku.

Na katika mabadiliko haya ya dunia yanatengeneza makundi matatu ya watu.

1. Kuna wale ambao wanabadilika haraka na hivyo kunufaika sana na mabadiliko.

2. Kuna wale ambao hawajui kama mabadiliko yanatokea na hivyo kuburuzwa na mabadiliko', hawa huendelea kuwa na maisha magumu.

3. Kuna wale ambao wanayagomea mabadiliko na hivyo wanaachwa nyuma.

Je wewe unataka kuwa katika kundi lipi?

Maisha ni yako, Chaguo ni lako.

Najikuta nikikusanya hadithi nyingi sana zinazohusiana na mabadiliko kwa sababu sasa hivi naandika kitabu cha jinsi ya kukabiliana na mabadiliko yanayotokea kwa kasi. Kama ungependa kuwa wa kwanza kukipata(katika softcopy) tuma ujumbe huu kwa watu wa tano kwenye email zao halafu nikopy mimi kwenye email hizo, tumia email makirita@kisimachamaarifa.co.tz kama hujui jinsi ya kukopi, wakati unaweka email ya unayemtumia chini yake kuna cc, hapo weka email yangu. Nitakupa zawadi ya kitabu hiki pale kitakapokamilika.

SOMA; Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.

Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Kama utaamua kupuuza ushauri mwingine wowote ambao unausoma sehemu mbalimbali basi shika ushauri huu mmoja tu. Shikilia ushauri huu na kila siku jikumbushe maana ni muhimu sana kwako ili kuweza kufikia ndoto zako.

Hii ni kwa sababu tunaishi kwenye jamii ambayo inajaribu sana kuturudisha nyuma.

Huenda mwaka huu 2015 umeweka malengo makubwa ambayo unajua kama ukiwez akuyafikia maisha yako yatabadilika kwa kiasi kikubwa sana. Lakini nakuhakikishia ukiwaeleza watu kumi malengo yako uliyojiwekea watu saba watakuambia haiwezekani, wawili watasikiliza hawatakuambia kwamba haiwezekani kwa sababu wanaogopa kukuumiza ila ndani ya nafsi zao wanaamini huwezi kuyafikia. Mmoja atakupa moyo kwamba unaweza japo na yeye anaweza kuwa hana uhakika sana.

Ukweli ni kwaba unapokuwa na malengo makubwa watu wengi watakuambia huwezi, haiwezekani, haijawahi kufanywa, kuna wenzako walijaribu wakashindwa na utaambiwa kila aina ya hadithi ya kukuonesha ni jinsi gani haiwezekani.

Cha kushangaza watu hawa wanaokuambia haiwezekani hawajawahi kujaribu na wala hawana uhakika na wanachoongea. Na mbaya zaidi wakishakuambia hivyo wanasahau baada ya dakika tano.

Yaani dakika tano baada ya mtu kukuambia kwamba lengo lako la kuwa bilionea haliwezekani, anasahau alichokwambia na anaendelea kufikiria matatizo yake mwenyewe kwenye maisha yake.

Sasa kitu muhimu cha kukumbuka kila siku ni kwamba hakuna anayeweza kukuambia ni nini unaweza au nini huwezi. Wewe mwenyewe ndio unaamua unafanya nini na maisha yako na kisha kufanya.

Ukiendelea kuwasikiliza watu kila siku hutafanya lolote, wakati watu hao wanasumbuliwa na matatizo yao wenyewe.

Maisha ni yako uchaguzi ni wako, chagua kuwasikiliza watu na uishie kuwa na maisha ya hovyo, au chagua kujisikiliza mwenyewe na uwe na maisha unayotaka wewe mwenyewe.

Chukua hatua… JISIKILIZE.

Tuesday, January 13, 2015

Una Mdomo Mmoja Na Masikio Mawili Kwa Sababu Hii Kubwa.

Kila mtu ana mdomo mmoja na masikio mawili kwa sababu kuu moja; unatakiwa kusikiliza zaidi ya unavyoongea.
Kwa bahati mbaya sana watu tunapenda sana kuongea badala ya kusikiliza.
Unapokuwa muongeaji sana, unakosa kujifunza kutoka kwa wengine.
Unapokuwa msikilizaji unajifunza mengi sana kutoka kwa wengine.
Na kama una upumbavu mwingi ndani yako(kila mtu ana upumbavu kiasi) kwa kuongea sana utaonesha upumbavu wako wote. Ila ukiwa msikilizaji utaonekana una busara.
Pia ukiwa muongeaji sana utajikuta unaongea na ya wengine na hatimaye unaanza umbea na majungu.
Sikiliza zaidi ya unavyoongea, utajifunza mengi na pia kuficha upumnavu wako.